Pre GE2025 Dkt. Nchimbi: Rais Samia yupo kwa mujibu wa katiba na atamaliza muda wake kwa mujibu wa katiba

Pre GE2025 Dkt. Nchimbi: Rais Samia yupo kwa mujibu wa katiba na atamaliza muda wake kwa mujibu wa katiba

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

PendoLyimo

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2014
Posts
969
Reaction score
1,055
“Kuna vitu ukisema unavyojua kabisa haviwezekani, Rais Samia yupo pale kwa mujibu wa Katiba na atamaliza muda wake kwa mujibu wa Katiba, tunaweka uchaguzi miaka mitanomitano ili wale watakaokuwa hawaridhiki ndani ya miaka mitano wapate nafasi nyingine ya kuja kuchagua sio katikati ya msimu"

“Na wanaojua demokrasia ndio maana Mbowe ni Mwenyekiti wa CHADEMA mpaka leo kila zilipoanza kelele ndani ya CHADEMA ‘Mbowe Must Go’ zimeshindikana kwasababu ni kinyume cha Katiba yao, wanaolinda Katiba ya CHADEMA wamemlinda Mbowe kwa nguvu zake zote na nyie mnajua imetokea zaidi ya mara tatu Mbowe Must Go ameenda wapi?, hajaenda popote yupo"
“Tunapokea taarifa nyingi, nilikuwa nasoma mitandao juzi na jana nimesoma maneno mazitomazito, kuna taarifa kama tatu nimesoma zinasema ndani ya CHADEMA kuna mgogoro mkubwa, kwahiyo Mbowe nae ni Mtuhumiwa wa mauaji haya, nilikuwa na Mbowe kwenye sherehe moja wakati tunaongea na Ndugu Kibao kutekwa na Mimi Walimu wangu wa saikolojia walinifundisha vizuri wakati Mbowe akiniambia kuhusu kutekwa kwa kibao nilikuwa namuangalia machoni kujua huyu anasema uongo, nikagundua anamaanisha, kwahiyo Mimi Mtu akiniambia Mbowe anahusika na utekaji nitamwambia sio kweli kwasababu nimeona akiongea na dhamira yangu inaniambia sioni Mtekaji hapa”

“Mwingine nimemsikia Mwanaharakati Uhuru sijui (Musiba) anasema Mtu wa kwanza anayetakiwa kuhojiwa ni Mnyika kwasababu ndio alikuwa wa kwanza kutoa taarifa, sasa Watu wasitoe taarifa kama Watu wametekwa?, Mnyika yule hata akiona panya anakimbia, kweli Mnyika anaweza kupanga mauaji?, maana kuna Mtu ukitaka kumsingizia tafuta cha kumsingizia lakini Mnyika masikini Mnyika, kama hamniamini siku mkutano wa CHADEMA wekeni panya apite mbele ya Mnyika”

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, akiongea na waandishi wa habari.

🗓️13 Septemba, 2024
📍Dar es salaam

#CCMImara
#VitendoVinaSauti
#TunaendeleaNaMama
#ShirikiUchaguziSerikaliZaMitaa
#KaziIendelee
 
..Sawa.

..asiwepo baada ya 2025.

..Samia must go.
 
Nikweli tutamuondoa kwa kura ndicho alichomaanisha mwenyekiti MBOWE
 
Hiyo ndio kauli ya Chama Tawala yaani CCM

Dr Nchimbi amesema Rais Samia yuko kwa mujibu wa Katiba na Mbowe ni Mwenyekiti wa Chadema kwa mujibu wa Katiba hivyo wataendelea kuwepo Hakuna wa kuwaondoa

Mlale Unono 🌹
 
Back
Top Bottom