Dkt. Ndugulile: Tunaweza kuhakiki upya usajili wa namba za simu kwa vidole ili kuwabaini wanaomiliki isivyo halali

Dkt. Ndugulile: Tunaweza kuhakiki upya usajili wa namba za simu kwa vidole ili kuwabaini wanaomiliki isivyo halali

Waziri Ndugulile amesema wizara yake inaweza kuhakiki upya usajili wa namba za simu kwa alama za vidole ili kuwabaini wanaozimiliki isivyo halali.

Ndugulile amesema mitambo ya kubaini hayo wanayo.

Source: Swahili times
uhakiki huo utakiwa na tofauti gani na usajiri wa awali?

Hizo pesa za kufanya hiyo kazi wapeleke kwenye mambo mengine, nchi ina mambo mengi ya kufanya.
 
Waziri Ndugulile amesema wizara yake inaweza kuhakiki upya usajili wa namba za simu kwa alama za vidole ili kuwabaini wanaozimiliki isivyo halali.

Ndugulile amesema mitambo ya kubaini hayo wanayo.

Source: Swahili times
Huyu jamaa kazi imemshinda.
Anaruka ruka tu kama bisi kikaangoni. Hajamaliza lile suala la vifurushi, anarukia rukia mambo mengine.
Kuhakiki tena mara ya tatu unahakiki nini kama sio upumbavu? Wakifanya tena hayo mauhakiki yao wafanye kwa taarifa walizonazo tayari, wasitusumbue tena kwenda kubofya bofya.
Huyu ni mmoja wa mawaziri ambao nadhani hata haelewi anachotakiwa kufanya.
 
Moja kati ya Mawaziri mzigo kabisa kuwahi kutokea katika nchi yetu. Mtu amesomea udaktari wa kutibu watu, anapewa kuongoza Wizara ya Mawasiliano na teknolojia!!

Ina maana wa hakuna Watanzania wenye sifa katika fani ya Mawasiliano na teknolojia kuongoza kwa ufanisi hii Wizara? Namuamini Mama kwa kiasi fulani. Naamini atafanya jambo sikubza usoni. Amtoe huyu Ndugulile kwenye hiyo Wizara. Hana tija, wala jipya lolote lile tangu alipoteuliwa na yule Mzee aliyejiamulia kila kitu kutoka kichwani mwake.
 
Waziri Ndugulile amesema wizara yake inaweza kuhakiki upya usajili wa namba za simu kwa alama za vidole ili kuwabaini wanaozimiliki isivyo halali.

Ndugulile amesema mitambo ya kubaini hayo wanayo.

Source: Swahili times
Huyu ni vema akarudishwa wizara ya afya maana haina mtu ina mwigizaji, huku amefeli mapema sn amebaki kutoa matamko pekee.
 
Uhakiki mpya maana yake Samia yuko sahihi kushangaa kwamba kulikuwa na haja gani ya uhakiki wa kwanza.

Hii maana yake huyu waziri atumbuliwe tu.
 
Waziri Ndugulile amesema wizara yake inaweza kuhakiki upya usajili wa namba za simu kwa alama za vidole ili kuwabaini wanaozimiliki isivyo halali.

Ndugulile amesema mitambo ya kubaini hayo wanayo.

Source: Swahili times
Hivi tatizo ni uhalali wa umiliki au matumizi ya hizo laini? Mathalani mtu anatumia simu iliyosajiliwa na ndugu yake si kwa biashara ya utapeli, kusambaza habari chafu na za uongo au matusi kuna shida gani?

Hii ni sawa na mtu kutumia chombo cha moto kinachomilikiwa na ndugu yake au rafiki yake haiwezi kuwa ni jinai kama hajaiba au kuvunja sheria ya usalama barabarani kwa kutumia hicho chombo.

Huyu waziri anashindwa kumuelewa Mama Samia anapohoji mantiki ya zoezi la usajili wa line za simu kwa alama za vidole unaofanyika. Maana yake ni kuwabaini wanaofanya jinai kwa kutumia simu kwa maana kuna wizi na utapeli unaendelea kufanyika kupitia simu na hakuna anayebainika, kukamatwa wala kuzuiliwa kwa kutumia huo mtambo anaosema waziri kuwa upo.

Kwa kauli hii anayosema waziri Ndungulile ni sawa na kusema jinai ni kutumia simu iliyosajiliwa na mtu mwingine na si matumizi mabaya ya hiyo simu.

Waziri anafeli pakubwa sana!
 
Na Bado mtaambiwa zoez la vutambulisho vya TAIFA wataanza upya maana wamegundua kitambulisho kimoja kinamilikiwa na watu wawil wawil

Upigaji upigaji upigaji upigaji

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Hilo linakuja ndugu yangu maana kuna waziri kule bungeni alisema kitambulisho cha NIDA si "muhuri" wa utanzania kwavile hata wakimbizi na wageni wanavyo.

Alisema mtu ataendelea kuhojiwa uraia wake hata kama anamiliki kitambulisho hicho. Sasa unaweza kushangaa kwanini hawaku-categorize hivi vitambulisho kwa kuzingatia uraia wa mtu kama ni mtanzania, mkazi wa muda au mkimbizi wakati wa usajili kwa maana taarifa hizi zilitolewa kwenye usajili.
 
Waziri Ndugulile amesema wizara yake inaweza kuhakiki upya usajili wa namba za simu kwa alama za vidole ili kuwabaini wanaozimiliki isivyo halali.

Ndugulile amesema mitambo ya kubaini hayo wanayo.

Source: Swahili times

Usumbufu kwa wananchi, kwanini hawakufanya hilo tangu awali?
 
Nchi ya matukio hii 😀
Hawa ni wapumbavu, wanasema wana mitambo sijui wanamtishia nani, kwanini wasiitumie wawakamate hao wanaosema hawamiliki simu kihalali mpaka waje mtandaoni watishietishie watu, kwanini wasababishe usumbufu kwa mamilioni ya watu wakati wahalifu ni wachache sana na wanaweza kuwapata kwa hiyo mitambo yao.

Hii haina tofauti kabisa na yale maonyesho ya vifaru kila tarehe 9 Dec huku wageni waalikwa wakiwa ni Marais wan nchi jirani ambaoo kimsingi mnajua hawawezi kufuatilia matukio kwenye TV, mnawaalika kwenye tukio ili waone kwa lazima
 
Kama kuna namba hazijasajiliwa si wazifungie tu, maana hata wakirudia mara ngapi; udanganyifu kwenye usajili hautakwisha maana watu wengine wanatengeneza vitambulisho feki na majina feki ili mradi watimize malengo yao.
 
Hizi project ni dili za watu, nchi hii ujinga ujinga mwingi sana, unahakiki nini wakati umesajili kwa Nida,taarifa za kila mmiliki wa laini anajulikana.......sasa huu ni usumbufu kwa Watanzania
Chezea kubambika, mtihani wakumaliza la saba pambika ufaulu 97) %.walioenda form one wengine hawajui kusoma, kuandika wala kuhesabu. mtu iliapewe mkopo wa elimu ya juu kigezo ni umasikini wake na si ufaulu wake. kufanya kazi electronically hhhuleta matokeo ya haraka, usahihi na ufanisi. Almradi mfumo ujengwe kwa uweledi, utunzwe, ufanyiwe kazi na mwenye kuujua, data zinaingizwa ziwe sahihi. mifumo inakiwa iendeshwe na watu intelligent na ilishwe data sahihi ilikupata zao sahihi "gabbage in gabbage out"
 
Back
Top Bottom