Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
MBUNGE DKT. OSCAR KIKOYO AKICHANGIA BAJETI WIZARA YA ELIMU MWAKA WA FEDHA 2023/2024
Mhe. Dkt. Oscar Ishengoma Kikoyo, Mbunge wa Jimbo la Muleba Kusini amechangia hoja ya hotuba ya bajeti ya Wizara ya Elimu ya zaidi ya Trilioni Moja Bungeni Jijini Dodoma iliyosomwa na Waziri wa Elimu, Mhe. Profesa Adolf Mkenda
"Hivi hizo taasisi zilizoko chini ya Wizara ya elimu inafundisha nini watoto wetu, zinaendana na hali halisi ya maisha ya mtanzania kweli?" - Dkt. Oscar Kikoyo, Mbunge wa Muleba kusini.
"Unaenda kufundisha watoto historia ambayo haina tija kwa taifa badala yake tuje na kitu mahususi cha kufundisha watoto wetu" - Dkt. Oscar Kikoyo, Mbunge wa Muleba kusini.
"Kwa miaka nenda rudi Mkoa wa Kagera ni Mkoa wa elimu upende usipende, mpangilio mliouweka Bado unatuweka kwenye mentality zilizopitwa na wakati ili watoto wakue wakijua mambo ya msingi" - Mhe. Dkt. Oscar Kikoyo, Mbunge wa Muleba kusini.
"Watendaji wote wathibiti ubora walioko TAMISEMI warudishwe wizara ya elimu halafu TAMISEMI wabaki kwenye ukarabati tu bila hivyo tutakuwa tunacheza mdundiko hapa, tunakwenda wapi? Serikali ni moja na Taifa ni moja" - Dkt. Oscar Kikoyo, Mbunge wa Muleba kusini.
"Tuiangalie Sekta binafsi ya elimu ni kama mshindani wa Wizara ya Elimu! siyo kweli, mahusiano ya Wizara ya elimu na TAMISEMI hayana tija" - Dkt. Oscar Kikoyo, Mbunge wa Muleba kusini.