Dkt. Philip Mpango: Tuwe na mfumo madhubuti wa kudhibiti dawa kuepuka wizi

Dkt. Philip Mpango: Tuwe na mfumo madhubuti wa kudhibiti dawa kuepuka wizi

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango, amesema utunzaji hafifu wa kumbukumbu za dawa na vifaa tiba katika hospitali na vituo vya afya unachangia kusuasua kwa usambazaji wa dawa kutoka Bohari Kuu ya Dawa (MSD), na pia kufungua mianya ya wizi na matumizi mabaya.

Akizungumza Jumamosi Julai 12, 2025, jijini Dodoma wakati wa Mkutano wa Mwaka wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri kwa mwaka 2025, Dkt. Mpango ameeleza kuwa hali ya sasa haiwezi kuvumilika tena, akisisitiza kuwa lazima kuwepo na mfumo madhubuti wa usimamizi wa dawa unaotekelezwa kwa ufanisi.

Makamu wa Rais pia ameagiza kuimarishwa kwa utoaji elimu kwa jamii kuhusu matumizi sahihi ya dawa, hasa dawa za maumivu na antibiotiki, ambazo matumizi yake holela yanaendelea kusababisha usugu wa vimelea na madhara kwa viungo muhimu vya mwili.

 
Vifaa tiba tutawawauzia tu hamna jipya
 
Back
Top Bottom