The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango amewataka vijana nchini waliobahatika kuwa na wazazi walio hai kujenga utamaduni wa kuwatunza, kuwalea na kuwaonyesha upendo akimtaja mzazi kama kiungo muhimu katika familia na wakili wa Mwenyezi Mungu hapa duniani.
Dkt Mpango ameyasema wakati wa ibada ya misa ya mazishi ya mama wa Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Prof Adolf Mkenda,Bi Sekunda Massawe (82), misa iliyofanyika kanisa katoliki la Mtakatifu Pius wa X, Parokia ya Tarakea, wilaya ya Rombo, Mkoani Kilimanjaro.
Mama Sekunda, ambaye alifariki Januari 30, mwaka huu akisumbuliwa na ugonjwa wa saratani, amezikwa katika makaburi ya familia yaliyopo katika Kijiji cha Mbomai Juu, kata ya Tarakea Motamburu, wilayani hapa.