Dkt. Rugemeleza Nshala: Nimetishiwa maisha baada ya kutoa maoni kuhusu mkataba wa Bandari na DP World

Dkt. Rugemeleza Nshala: Nimetishiwa maisha baada ya kutoa maoni kuhusu mkataba wa Bandari na DP World

Akili yako imekuwa like tunnel vision. According to your mind and beliefs you're right.
I shouldn't argue with narrow minded people who think in one dimension or in one vector plane
Utabadilisha lugha zote na sisi kuzungu kinapanda sana lakini mimi nakupiga na lugha ya Taifa tu kizungu cha nini. shida yenu mikiwekwa kona mnaanza kuleta uzungu, babu hata ki spanish naweza kukuandikia shida yako unadhani unaongea na kilaza. Kula maisha babu lugha hainitishi mimi.
 
If they kill you, your blood will speak more than your mouth spoke.

Tutachinjana hadharani. Waache ujinga. Tanganyika yetu haiuzwi.

Walimuua Dr. Mvungi kwa katiba. Huyu hatutakubali
Sema hutokubali, usituhusishe na wengine kwenye huo upumbavu wenu.
 
Heri mtu yule asiyekwenda katika shauri la wasi haki wala hakusimama katika njia ya wakosefu,bali sheria ya Bwana ndiyo imwongozayo katika maisha yake yote.Mtegemea cha nduguye hufa angali maskini wahenga walisema kwa maana atabakia kusifu mafanikio ya wengine.
Mimi mwenzangu akifanya vizuri kwanini nisimsifie.
 
Basi mwambie askofu ajitambulishe rasmi kama mwanachama wa CHADEMA
Wanajificha nyuma udini lakini wanachuki za wazi juu ya Rais Samia inawakera sana hawakutegemea mtu kuchukua nchi bila nguvu hawajui mamlaka Mungu anatoa. JPM aliwatesa kweli lakini waliuvyata wote na dua wakamuombea 😛
 
MAISHA YANGU YAPO HATARINI;WAKILI DKT NSHALA RUGEMELEZA AZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI.

"Damu yangu kama itamwagika basi ikapalilie mapambano ya kulinda rasilimali za nchi yetu Tanzania" Wakili Dkt Nshala Rugemeleza #MkutanoWaandishiWa Habari

"Kuna maagizo kutoka ndani yanayosema,Mimi nikionekana niteketezwe,nimalizwe,niuawe,na jina langu liwe refu lianze na Marehemu Rugemeleza Albert Kamwagwa Nshala" Wakili Dkt Nshala Rugemeleza

"Kama wenye dhamana watapenda Mimi niondoke,niitwe Marehemu basi yatawapata makubwa,vizazi vyao mia nne na arobaini vitakwenda kuteseka na kujibu juu ya jambo hili" Wakili Dkt Nshala Rugemeleza #MkutanoWaandishiWaHabari.

"Siko tayari kupigishwa magoti,kunyamazishwa au kukandamizwa na mtu yeyote ambaye kikatiba na Yeye ni Raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama Mimi" Wakili Dkt. Nshala Rugemeleza.

"Nitasema kweli daima fitna kwangu mwiko,sitatishiwa na binadamu mwenzangu anayeumbwa kama Mimi,anayeenda chooni kama Mimi,anayeumwa kama Mimi,anayekufa kama Mimi"Wakili Dkt Nshala Rugemeleza #MkutanoWaandishiWaHabari.

"Nimetumia lugha nyepesi sana,na laini kwa walichotufanyia viongozi wetu,kama ingekuwa ni huru na kawaida basi viongozi wetu wangekuwa mbele ya sheria muda huu tunavyozungumza" Wakili Dkt Nshala Rugemeleza.

"Mfumo wetu ni ule ambao hata Rais akikukanyaga unasema ooh ahsante kwa kunikuna" Wakili Dkt Nshala Rugemeleza

"Sitasalimu amri,nitaendelea kupinga ugawaji huu wa rasilimali za nchi yetu,nitasimama na maneno yangu" Wakili Dkt Nshala Rugemeleza

"Mkataba huu mbaya kuwahi kutokea Rais anahusika Moja kwa Moja kwa sababu sahii yake ipo mwisho wa jedwali la mkataba,Marais uwa hawasaini lakini yeye kasaini"Wakili Dkt Nshala Rugemeleza#MkutanoWaWaandishiWaHabari

"Bunge la mwaka 2017 lilitunga sheria kuhusu mikataba ya rasilimali zote zipite bungeni,ila mkataba wa bandari unasema Dp World haiusiki na sheria hiyo" Wakili Dkt Nshala Rugemeleza

"Mkataba huu unalimbikiza Mali zote za nchi hii kuhusiana na bandari kwa kampuni binafsi ya DP World,sheria inasema tulinde maliasili kwa ajili ya kizazi hiki na vizazi vijavyo,hiki ndicho kilichotufanya tunyanyuke tupinge" Wakili Dkt Nshala Rugemeleza

"Kama nasema uwongo nashika biblia yangu Mimi ni mkristo,nianguke chini Mungu achukue uhai wangu" Wakili Dkt Nshala Rugemeleza #MkutanoWaandishiWaHabari.

"Nimesoma digrii yangu ya kwanza Udsm,digrii ya pili Havard,nikaenda kusoma digrii ya tatu Yale na PhD Havard baada ya kutoelewa lugha iliyozungumzwa kwenye mgogoro wa Bulyakhuru" Wakili Dkt Nshala Rugemeleza #MkutanoWaandishiWaHabari.

"Tuna haki ya kulinda maliasili za Taifa kama zipo hatarini,sio kama mkubwa hakosei,Bandari ni mali ya Watanzania wote, tuna haki kuhoji au hata ikiwezekana kwenda mahakamani kama Mali za nchi zinauzwa"Wakili Dkt Nshala Rugemeleza #MkutanoWaandishiWaHabari.

"Naipenda nchi yangu Tanzania,nipo tayari kuifia nchi yangu,na kama huu ni mwisho wangu basi nasema kwa herini tutaonana Paradiso" Wakili Dkt Nshala Rugemeleza #MkutanoWaandishiWaHabari.
Ngoja tuanze uchunguzi huyu ana passport ya USA tufanye utaratibu aende haraka hatutaki mahusiano mabaya na USA likimpata.
 
Chawa kwa kawaida hukaa kwenye "pindo/mshipi" wa nguo ya kwanza kuvaliwa inayokuwa in contact na mwili.

Sijui kama chawa hukaa mgongoni zaidi ya kiunoni kwenye nguo za ndani.

Kama wameweza kujitangaza wanakaa huko,hawa ndiyo wanatisha watu.
 
Nimecheksa sana, ingawa sio jibu nililokuwa nategemea. I truly wish to understand, angalia Mkapa hayupo, JPM na yeye hayupo, na kila kiongozi aliyepo na ajaye ataondoka. Mtu ukijua hili kwanini usihakikishe vizazi vijavyo vinakuta mambo bora zaidi? Sisi ni madudu kila siku jamani?
Haya mambo yanaanzia ngazi ya familia mkuu, ni wachache huwaandalia future nzuri watoto wao, wengi wetu ni mtoto asome. Akishindwa shule basi ajihangaikie, na akimaliza shule tunataka atusaidie na sio aanze nae maisha yake.
Unatengeneza kizazi cha kujijali chenyewe tu
 
Wasiojulikana bado wapo, kama walifanya kazi huyu msaliti akiwa msaidizi na hakuwahi kuwakemea, sitashangaa msaliti nae akiamua kuwaacha wasiojulikana wamsaidie kuwafunga watanganyika midomo wanaolilia ardhi yao iliyopewa mwarabu...
Samia Kwisha habari yake.

Ataendelea kuwepo kwa muda mfupi; lakini kuwepo huko si kwa ridhaa ya wananchi.

Hana njia yoyote anayoweza kurudisha imani ya wananchi kwake.
 
Tena ni bahati yake sana "kutishwa" miaka 3 nyuma alikuwa nao hata huo mdomoi wa kuongelea? Wenzake waliokuwa na midomo wako wapi?
 
Nimemsikia sana huyu Wakili Msomi. Naamini kama Rais Samia atasikiliza hii link ya youtube atabadili mawazo yake kuhusu mkataba wa DP WORLD!! Itakuwa ni ni NUKSI kubwa kwake kama raia wa Tanzania atapoteza maisha sababu ya kutetea raslimali za nchi...
Ushauri mzuri sana
 
Mbna mnaretemeka Kuhusu vifo awam hii, awam ilipita walikua wapi.
 
Habari wasomaji na wananchi wote.

Je, tumekuwa Taifa la ovyo hivi.

Je, hili ni suluhisho la mjadala katika mambo ya Kitaifa?

Akiuawa, tunatuna ujumbe gani.

Pia soma
-
Kwa mujibu wa ibara ya 14 ya katiba ya nchi yetu kila mtu ana haki ya kuishi na kwamba anapaswa kupata hifadhi ya maisha yake kutoka kwenye jamii hiyo.

Maneno yaliyosemwa dhidi yake na watu wengine waliojiita masheikh yalikuwa yanasikitisha kwa mtu ambaye anamfahamu Profesa Issa Shivji kwa uzalendo wake na utumishi wake uliotukuka na kujitoa kwake kwa nchi yetu, wale watu walikuwa wanaongea kana kwamba ni maneno yao bali kulikuwa na watu ambao walikuwa nyuma yao.

Damu yangu kama itamwagika basi ikapalilie mapambano ya kulinda rasilimali za nchi yangu Tanzania.

Mtu hawezi kuishi katika nchi ambayo ni Jamhuri na watu wengine wakawa na leseni ya kuondoa uhai wao. Mwenye leseni, ruhusa na mamlaka pekee ya kuondoa uhai wa mtu hapa duniani ni Mwenyezi Mungu pekee.

Kiukweli kuua watu kupo na watu wamefariki, watu wamejeruhiwa na kupata matatizo makubwa. Kufuatia hilo nimeamua kuja mbele ya umma wa Watanzania kuwaambia kwamba mimi Rugemeleza Nshala maisha yangu yako hatarini. Kuna maagizo kutoka ndani kwamba nitakapopatikana niteketezwe, niangamizwe na kuitwa marehemu.

Mkataba huu wa bandari umesainiwa au umepewa kibali kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kibali hiko kinaonekana katika kiambatanisho kimojawapo katika mkataba huo ambacho kina saini ya Rais Dkt. Samia

===
Wakili wa kujitegemea Dkt.Rugemeleza Nshala amesema amepokea taarifa kutoka vyanzo vya kuaminika ndani ya mifumo kuwa anatakiwa kuuwawa kwa kile alichokieleza kuwa ni kutokana na msimamo wake dhidi ya watu waliojitokeza kumshambulia kwa maneno ya kejeli na kuudhi Prof.Issa Shivji baada ya msomi huyo wa sheria kutoa maoni yake dhidi ya sakata la uwekezaji wa Bandari linaloendelea sasa hapa nchini

Akizungumza na Wanahabari kwenye ukumbi wa Mesuma Hotel, Makumbusho Jijini Dar es Salaam, Dkt.Nshala ambaye pia amewahi kuwa Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) ameeleza kuwa hivi karibuni kupitia jukwaa la 'club house' alitoa maneno makali ambayo kiuhalisia amedai kuwa ndio msimamo wake dhidi ya watu hao ambao anaamini kuwa walichokizungumza si maneno yao bali wanatumiwa na watu wenye mamlaka nchini kutoa lugha za kashfa na kuudhi dhidi ya mtu mwenye umri mkubwa na anayestahiki heshma kubwa dhidi yao kwenye jamii

Dkt.Nshala aliyefika kwenye Kikao hicho akiwa amebeba Vitabu viwili alivyoeleza kuwa anavyoviamini zaidi (Biblia na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania) amesema anawaeleza wenye mamlaka walio nyuma ya mpango huo kuwa yuko tayari kufa kwaajili ya nchi yake

Ikumbukwe kuwa kupitia jukwaa hilo ambalo lilijadili mjadala wa kina kuhusiana na uwekezaji wa Kampuni ya DP World ya Dubai kwenye Bandari, Dkt.Nshala alitoa kauli zolizoonekana kuwashambulia zaidi viongozi waandamizi serikalini akiwemo Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof.Makame Mbarawa nk
---

Ndugu Watanzania!
Dkt. Rugemeleza Nshala ametujulisha kuwa maisha yake yako hatarini. Wakili Dkt. Nshala anasema kuwa ametaarifiwa juu ya mipango ya kutaka kumuua (assassination) inayopangwa dhidi yake! Vitisho dhidi ya maisha ya Wakili Dkt. Nshala vinakuja muda mfupi tu baada ya yeye kutoa maoni yake kwa hisia kali akipinga Mkataba wa Bandari kati Serikali ya Tanzania na Ufalme wa Dubai.

Dkt. Rugemeleza Nshala, ambaye alikuwa Rais wa Tanganyika Law Society (TLS) ni wakili na mwanasheria mbobevu anayejua vema mipaka yake kikatiba na kwa nafasi yake anao wajibu wa kutoa ushauri na maoni kwa Watanzania katika masuala ya sheria na katiba ya nchi.

Sisi Askofu tumepata muda wa kuomba na Dkt. Nshala na kumtia moyo kuwa asiogope kwani alitoa maoni yake kama raia anayeipenda nchi yake na hakuvunja sheria ye yote ya nchi. Kwa maoni yetu, watu wanaomtisha Dkt. Nshala au wanaotaka kuondoa uhai wake ni watu waoga ambao wanataka kumchafua Rais Dkt. Samia ili dunia ifikiri ameanza kuwaua wakosoaji wake.

Kwa hiyo, sisi Askofu Mwamakula tunatoa wito kwa watu, kikundi, vikundi hata taasisi ambao wanapanga kutoa uhai wa Dkt. Nshala pamoja na wanaharakati wengine wanaotoa maoni yao au hata kuikosoa Serikali kuhusiana na suala la Mkataba wa Bandari waache mara moja. Kama wao wanafikiri kuwa Dkt. Nshala na wenzake wamefanya kosa lo lote kisheria, wawapeleke mahakamani badala ya kuanza kuwatisha.

Kutisha watu na kutaka kuwaondoa au kuwaua watu nje ya mfumo wa kisheria ni uhaini, uuaji, unyama na ujambazi bila kujali mtu anayefanya matendo hayo. Sisi Askofu tunatoa tahadhari hii kama kukinga mapema ili watu hao wajue kuwa wanachokipanga kufanya hakikubariki. Kama Dkt. Nshala na wenzake watadhulika kwa lolote, watu waliowahi kutoa kauli zao kwa lengo la kuwatisha, hao watawajibika. Kukinga ni bora kuliko kutibu! Tumetimiza wajibu wetu!

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Dar es Salaam, 6 Julai 2023; 09:39 am.



View attachment 2680028


Dr Nshala ni mzalendo bahati nzuri mimi binafsi namjua kama Kaka. Huyu kaka ni kati ya wanasheria wenye uwezo mkubwa Duniani sio Tanzania pekee. Yaani huyu ni zaidi ya Chenge maana ni mzalendo na hajaweka mbele kujinufaisha. Mimi nilishaongea naye kuhusu kuja USA na atatengeneza zaidi ya $200K kwa mwaka lakini akangangania kubali Tanzania na kwenye jumuia yetu pale Ununio na kazi zake za kupigania mazingira......

Serikali ingetakiwa kumfanya rafiki maana sio mwanasiasa ni Mtaifa tu.
 
Pelekani watoto kusoma undergraduate degrees hizo ndio zina matter kwenye uelewa wa kawaida kushinda post graduates.

Ni sawa na mtu akasome tax law masters, halafu hana degree ya accountancy au finance. Huko kwao uwezi kusajiliwa kufanya kazi as a tax lawyer bila ya kuwa qualified accountant first au exception degree yako ya kwanza ni ya finance. Hizo ni specialisations laws huko kwao na kuna taratibu nyingi za kuwa mwanasheria bila ya kusoma sheria undergraduate ndio msingi wa hizo masters.

Ndio kama hawa wanasheria wenu it doesn’t matter ata angekuwa amesoma heaven university hana foundation ya business law halafu anakwenda kuandika mathesis na kujiita mtaalamu wa maswala ya contract umeona wapi.

Kwanza atuambie aliandika mambo gani tupime merit ya kazi yake kama ina qualify kudadavua mikataba ya kibiashara.

Pili nimemuona mpuuzi kujisifia kusoma maswala ya environmental wakati kila siku yanabadilika with COP new agendas, moreover siku hizi environmental reporting ni mandatory kwenye financial statements za mashirika makubwa dunia imepiga hatua sana kwenye nyanda hizo how they think wewe bado unazungumzia research ya mazingira na mambo uliyo soma 2000 wakati a lot has changed in between.

Social sciences sio hard science ambazo theories zinaweza kukaa muda mrefu, huko kwenye social science na biashara global policies mpya kila kitu kinabadilika kifikra na kwenye utekelezaji siku ya pili; we unajisifia kusoma environmental issues 2000’s, akili zake sio sawa.

Hii ndio shida yetu watanzania tunaweka sana imani kwa wasomi as if ni miungu watu, sisi wenyewe Binafsi ni wavivu wa kujifunza mambo. Matokeo yake we are vulnerable to their statements, wakiamua kupotosha tunaamini non-the-wiser on the merit of their statements.

Huyo bwana amepotosha sana kwenye IGA sio hivyo tu along the way amewapa watu shutuma za uongo, ametoa seditious statements dhidi ya nchi; halafu anatoka hapo anasema uhuru wake wa maoni.

Nyofoa kucha tu hakuna namna
 
Wa wivu mtoto wa kike ndo maana huolewi yaani joja zoote hizi zinazoongelewa hapa we umeona joho tu! Sijui akili za wapi au umelewa uji wa magimbi
 
mimi nilichokuja kugundua katika harakati zangu ni kwamba kusoma na kua na akili ni vitu viwili tofauti.

hivi kweli msomi wa sheria unanyoosha tai yako kabisa eti unaenda kushitaki Seriakali kwenye Mahakama zake yenyewe ?

ili ugundue nini yaani na akili zako zote na usomi wako wote ?

ndio maana nikasema kusoma na kua na akili havihusiani …

mimi mwanzo kabisa nilisema hivi:

mngeenda kushtaki kwenye Mahakama za nje ya Africa kidogo mngenishawishi.

ila kumshtaki Baba yako na bado unaishi kwake huo ni ujinga wa kiwango cha rami …
 
Back
Top Bottom