Dkt. Rugemeleza Nshala: Nimetishiwa maisha baada ya kutoa maoni kuhusu mkataba wa Bandari na DP World

Dkt. Rugemeleza Nshala: Nimetishiwa maisha baada ya kutoa maoni kuhusu mkataba wa Bandari na DP World

Mimi sina hata nikiita press watajiuliza huyu naye ni nani. Impact ninayo kwa family yangu tu lakini kuna wengine hata kwenye family zao wanaondoka kama hajaondoka mtu.
Basi kama unampact na familia yako mkuu jitahidi kunyamaza maana nchi sio levo ya familia yako.

Waache waliovuka levo za familia na kuweza kuijadili nchi Kwa mapana yake wahoji.

Mtu mwenye akili na busara humtambua pale tu anapofungua mdomo kuongea au kalamu kuandika.tafakari
 
Wahoji kitu gani? wanamwakilisha nani nchi hii? family zao au? Hii nchi inawakilishi waliochaguliwa, ina viongozi waliochaguliwa. Sasa wewe kama unaona una hoja jiunge na siasa sio unakuja kwenye press na unafiki eti mimi sina chama chochote ni mwanaharakati, mwanaharakati alikutuma nani. kapiganie family yako. Kaja na misifa kibao eti nimesoma USA ningelipwa 22k siju bla bla ujinga mtu watu wakimtaka wanamtikia kilema stroke mwisho wa habari.
 
Sasa huyo prof wako fake ndio level yangu maana hatuna impact nchi zaidi kwenye nyumba zetu maisha yamempiga sasa anatafuta sababu ya kuaga dunia eti tukutane paradiso aliyemwambia anaenda paradiso nani? hicho kitabu cha dini alichoshika kinasema heshimuni mamlaka zenu sio anakuja kwenye press na kukosa heshima kwa viongozi hata kama una hoja tofauti sema ila heshimu mamlaka. Mbona kwa JPM aliufyataa
 
Hivi mama samia alikuwa na akili timamu wakati anasaini hii laana(mkataba)?alishikiwa bunduki?nini kiko nyuma ya huu mkataba ambapo SSH haoni mapungufu makubwa?ninapata ukakasi mama samia na Magufuli walikuwa ni hasi na chanya Kwa maslahi ya Tanzania.kama kweli haoni tatizo kwenye hii tuhuma..basi yahitajika kujitafakari.
Laana lazima ipite na uzao SSH

Hii inaonesha mwanamke hawezi madaraka makubwa.
Akisifiwa tu una jicho zuri ameshalegea na kudondosha wino. Ila hii Ni ya kwao sema wanatumia mgongo wa muwekezaji mkuu.
Yaani hii anajilipa Koo yake na watu wake wa karibu,watu wameshajilipa kwenye madini,nishati ,mbuga kilichobakia Ni bandari.
Yaani watu wameshauza ama wamejimilikisha kwa gia ya uwekekazaji Ila Ni wao tu wanajilia matunda ya wajinga waliolala ,wanabakia kuongelea mitandaoni
 
Wewe ndie huna hoja, unaandika upuuzi mtupu. Wasiojulikana wapo na tulishaona walichomfanya Lissu, ana haki ya kutoa taarifa kuhusu uhai wake.

Asipuuzwe.
Yeye alipoamua kumtukana raisi hakujua madhara yake, sisi tumsaidie nini aasa, ameshalikoroga atulie tu aache kulia lia, wakili msomi kweli hajui kua ulimi uliponza kichwa.
 
06 Julai 2023​

🅻🅸🆅🅴 DKT NSHALA ADAI KUTISHIWA MAISHA '' MAISHA YANGU YAKO HATARINI

Mkutano na waandishi wa habari Dr. Nshala athibitisha kupata taarifa kutoka vyanzo vinavyothibitika kuna njama za kuondoa uhai wake Ikiwemo uhai wa wakili Boniface Mwabukusi Prof. Issa Shivji hivyo siwezi kukaa kimya kwani imewahi kutokea kwa Mwangosi, Azori, Ben Saanane kupigwa risasi Tundu Lissu.

Dr. Nshala anasema inasikitisha kuona kuna watu wamejipatia leseni ya kuondoa uhai wa watu kwa kuwa tu kuna wametoa maoni yanayokinzana na wale waliopo madarakani .

Dr. Nshala amesisitiza kuwa mkataba wa bandari unamuhusu rais kutokana na kibali cha rais na mara nyingi mikataba huwa haina muongozo wa rais.

Kulinda maliasilia ya nchi yetu ni haki ya kila raia iliyotamkwa ndani ya katiba ya Tanzania. Hivyo tunavyopiga kelele tunatimiza haki yetu ya msingi ibara ya 26.1 ya katiba inasema .

Ibara ya 9 (c) ya katiba inaitaka serikali kuwajipika pia kutunza mali za taifa.

Huu mkataba unamilikisha mali zote kwa mtu binafsi yaani kampuni ya DP World ya Dubai.

Juzi kumevuja marekebisho yaani Miscellaneous amendments laws ili kuondoa bandari za maziwa na katika mito ya maji ili DP World waweze kufaidi Mali ya asili ya bandari.

DP World anaendelea kupewa ukiritimba wa kumiliki mali zetu kwa aina ya ajabu kupitia muswaada huu mpya utakaopelekwa bungeni kinyume na sheria ya rasilimali iliyotungwa mwaka 2017 ya kulinda mali kwa vizazi vyetu na vizazi vijavyo.

Dr. Nshala nimepata utaalamu mkubwa katika vyuo vikuu tajwa vya Yale na Harvard vyote vya nchini Marekani kwa miaka 10 1/2 kuelewa mikataba na sheria za wawekezaji vizuri. Hivyo elimu niliyopata siwezi kuacha kuitumia kutetea mali ya nchi yetu Tanzania ambayo imenisomesha.

Ningeweza kubaki Marekani kuajiriwa wakati ule kwa mshahara wa dola za kimarekani 22,000.00 kwa mwezi na bonasi kubwa kila mwaka.

Dr. Nshala amesema sitaweza kutishika kukimbia nchi yangu nitabaki hapa hapa Tanzania na wale waovu wanaotaka kuondoa uhai wangu wakifanikiwa basi wao na vizazi vyao laana hii itawaandama milele na kuwasumbua sana.

Mwandishi John Marwa wa Jambo TV anauliza swali kwa Dr. Nshala kuwa kauli za wakili Dr. Nshala zilikuwa kali kwa maoni ya baadhi ya Tanzania.

Vibaraka wa ndani ya nchi wanajidanganya kupindisha maana ya kauli na maneno utetezi wa mali ya umma. Anasisitiza Dr. Nshala kujibu swali la mwandishi, Lugha ni ya uchungu na siyo kali bali kuwaamsha rais, makamu wa rais, mawaziri, bunge kuwa wanapaswa kukubali makosa yao kwa kuwaambia ukweli ....

Duu, Hizi Kiki zinafanana Kabisaa na za Mpilipili wa Uto FC.
Nb: Kuna Rafiki yake alienda kwa Demu wake Iringa Kutekwa. Haya Maisha yanaenda Kasi.
Yaani ; Mawakili Wenzako hakuna aliyetumia Mbinu hii ya kiki angalau Wametumia Kiki ya Kwenda Mahakamani.
Maoni ni Muhimu lakini Kuichafua nchi na Rais kimataifa Siyo Uzalendo Kabisaa.
Mimi kama King Marafyale nalaani Kauli hiyo Tata Isiyoiheshimisha nchi Yetu###%}{
 
Wahoji kitu gani? wanamwakilisha nani nchi hii? family zao au? Hii nchi inawakilishi waliochaguliwa, ina viongozi waliochaguliwa. Sasa wewe kama unaona una hoja jiunge na siasa sio unakuja kwenye press na unafiki eti mimi sina chama chochote ni mwanaharakati, mwanaharakati alikutuma nani. kapiganie family yako. Kaja na misifa kibao eti nimesoma USA ningelipwa 22k siju bla bla ujinga mtu watu wakimtaka wanamtikia kilema stroke mwisho wa habari.
Hija lini?
 
Napata ukakasi na uwezo wako wa kuchambua mambo.🥂
 
Napata ukakasi na uwezo wako wa kuchambua mambo.🥂
Hata napata ukakasi na wewe. Sasa ukitaka ujue uwezo wangu weka hoja zako na nitakujibu kwa hoja halafu tuone uwezo wangu na wako bila matusi bila dharau.
 
Wameanza kumwaga damu.

This was expected.
 
Sasa huyo prof wako fake ndio level yangu maana hatuna impact nchi zaidi kwenye nyumba zetu maisha yamempiga sasa anatafuta sababu ya kuaga dunia eti tukutane paradiso aliyemwambia anaenda paradiso nani? hicho kitabu cha dini alichoshika kinasema heshimuni mamlaka zenu sio anakuja kwenye press na kukosa heshima kwa viongozi hata kama una hoja tofauti sema ila heshimu mamlaka. Mbona kwa JPM aliufyataa
Narrow minded people.💔💔💔
 
Hata napata ukakasi na wewe. Sasa ukitaka ujue uwezo wangu weka hoja zako na nitakujibu kwa hoja halafu tuone uwezo wangu na wako bila matusi bila dharau.
Huna uwezo chanya wa kudadavua hoja nzito mkuu.JF si sehemu sahihi wewe kuwepo na hii ni kulingana na comments zako kwenye huu uzi

Kama kupitia huu uzi umedhibitisha uwezo wako wa kufikiri mkuu huoni kama utakuwa unajichosha maana kupitia mwandiko wako nimeshafahamu uwezo wako!!😁😁
 
Habari wasomaji na wananchi wote.

Je, tumekuwa Taifa la ovyo hivi.

Je, hili ni suluhisho la mjadala katika mambo ya Kitaifa?

Akiuawa, tunatuna ujumbe gani.

Pia soma
-
Kwa mujibu wa ibara ya 14 ya katiba ya nchi yetu kila mtu ana haki ya kuishi na kwamba anapaswa kupata hifadhi ya maisha yake kutoka kwenye jamii hiyo.

Maneno yaliyosemwa dhidi yake na watu wengine waliojiita masheikh yalikuwa yanasikitisha kwa mtu ambaye anamfahamu Profesa Issa Shivji kwa uzalendo wake na utumishi wake uliotukuka na kujitoa kwake kwa nchi yetu, wale watu walikuwa wanaongea kana kwamba ni maneno yao bali kulikuwa na watu ambao walikuwa nyuma yao.

Damu yangu kama itamwagika basi ikapalilie mapambano ya kulinda rasilimali za nchi yangu Tanzania.

Mtu hawezi kuishi katika nchi ambayo ni Jamhuri na watu wengine wakawa na leseni ya kuondoa uhai wao. Mwenye leseni, ruhusa na mamlaka pekee ya kuondoa uhai wa mtu hapa duniani ni Mwenyezi Mungu pekee.

Kiukweli kuua watu kupo na watu wamefariki, watu wamejeruhiwa na kupata matatizo makubwa. Kufuatia hilo nimeamua kuja mbele ya umma wa Watanzania kuwaambia kwamba mimi Rugemeleza Nshala maisha yangu yako hatarini. Kuna maagizo kutoka ndani kwamba nitakapopatikana niteketezwe, niangamizwe na kuitwa marehemu.

Mkataba huu wa bandari umesainiwa au umepewa kibali kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kibali hiko kinaonekana katika kiambatanisho kimojawapo katika mkataba huo ambacho kina saini ya Rais Dkt. Samia

===
Wakili wa kujitegemea Dkt.Rugemeleza Nshala amesema amepokea taarifa kutoka vyanzo vya kuaminika ndani ya mifumo kuwa anatakiwa kuuwawa kwa kile alichokieleza kuwa ni kutokana na msimamo wake dhidi ya watu waliojitokeza kumshambulia kwa maneno ya kejeli na kuudhi Prof.Issa Shivji baada ya msomi huyo wa sheria kutoa maoni yake dhidi ya sakata la uwekezaji wa Bandari linaloendelea sasa hapa nchini

Akizungumza na Wanahabari kwenye ukumbi wa Mesuma Hotel, Makumbusho Jijini Dar es Salaam, Dkt.Nshala ambaye pia amewahi kuwa Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) ameeleza kuwa hivi karibuni kupitia jukwaa la 'club house' alitoa maneno makali ambayo kiuhalisia amedai kuwa ndio msimamo wake dhidi ya watu hao ambao anaamini kuwa walichokizungumza si maneno yao bali wanatumiwa na watu wenye mamlaka nchini kutoa lugha za kashfa na kuudhi dhidi ya mtu mwenye umri mkubwa na anayestahiki heshma kubwa dhidi yao kwenye jamii

Dkt.Nshala aliyefika kwenye Kikao hicho akiwa amebeba Vitabu viwili alivyoeleza kuwa anavyoviamini zaidi (Biblia na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania) amesema anawaeleza wenye mamlaka walio nyuma ya mpango huo kuwa yuko tayari kufa kwaajili ya nchi yake

Ikumbukwe kuwa kupitia jukwaa hilo ambalo lilijadili mjadala wa kina kuhusiana na uwekezaji wa Kampuni ya DP World ya Dubai kwenye Bandari, Dkt.Nshala alitoa kauli zolizoonekana kuwashambulia zaidi viongozi waandamizi serikalini akiwemo Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof.Makame Mbarawa nk
---

Ndugu Watanzania!
Dkt. Rugemeleza Nshala ametujulisha kuwa maisha yake yako hatarini. Wakili Dkt. Nshala anasema kuwa ametaarifiwa juu ya mipango ya kutaka kumuua (assassination) inayopangwa dhidi yake! Vitisho dhidi ya maisha ya Wakili Dkt. Nshala vinakuja muda mfupi tu baada ya yeye kutoa maoni yake kwa hisia kali akipinga Mkataba wa Bandari kati Serikali ya Tanzania na Ufalme wa Dubai.

Dkt. Rugemeleza Nshala, ambaye alikuwa Rais wa Tanganyika Law Society (TLS) ni wakili na mwanasheria mbobevu anayejua vema mipaka yake kikatiba na kwa nafasi yake anao wajibu wa kutoa ushauri na maoni kwa Watanzania katika masuala ya sheria na katiba ya nchi.

Sisi Askofu tumepata muda wa kuomba na Dkt. Nshala na kumtia moyo kuwa asiogope kwani alitoa maoni yake kama raia anayeipenda nchi yake na hakuvunja sheria ye yote ya nchi. Kwa maoni yetu, watu wanaomtisha Dkt. Nshala au wanaotaka kuondoa uhai wake ni watu waoga ambao wanataka kumchafua Rais Dkt. Samia ili dunia ifikiri ameanza kuwaua wakosoaji wake.

Kwa hiyo, sisi Askofu Mwamakula tunatoa wito kwa watu, kikundi, vikundi hata taasisi ambao wanapanga kutoa uhai wa Dkt. Nshala pamoja na wanaharakati wengine wanaotoa maoni yao au hata kuikosoa Serikali kuhusiana na suala la Mkataba wa Bandari waache mara moja. Kama wao wanafikiri kuwa Dkt. Nshala na wenzake wamefanya kosa lo lote kisheria, wawapeleke mahakamani badala ya kuanza kuwatisha.

Kutisha watu na kutaka kuwaondoa au kuwaua watu nje ya mfumo wa kisheria ni uhaini, uuaji, unyama na ujambazi bila kujali mtu anayefanya matendo hayo. Sisi Askofu tunatoa tahadhari hii kama kukinga mapema ili watu hao wajue kuwa wanachokipanga kufanya hakikubariki. Kama Dkt. Nshala na wenzake watadhulika kwa lolote, watu waliowahi kutoa kauli zao kwa lengo la kuwatisha, hao watawajibika. Kukinga ni bora kuliko kutibu! Tumetimiza wajibu wetu!

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Dar es Salaam, 6 Julai 2023; 09:39 am.

View attachment 2680028
dah huyu jamaa muongo sana
 
Huna uwezo chanya wa kudadavua hoja nzito mkuu.JF si sehemu sahihi wewe kuwepo na hii ni kulingana na comments zako kwenye huu uzi

Kama kupitia huu uzi umedhibitisha uwezo wako wa kufikiri mkuu huoni kama utakuwa unajichosha maana kupitia mwandiko wako nimeshafahamu uwezo wako!!😁😁
Ningekujibu vizuri lakini huwezi kuacha tabia za kihaya za kujisifu. Endelea kuandika vizuri kama ndio unadhani mafanikio. Maisha magumu sana wacha sisi tule maisha faida ya nini nikupe.
 
Narrow minded people.💔💔💔
Ni kweli lakini na uhakika mimi ni bora kuliko wewe hilo na uhakika 100% wala sina shaka, nyinyi ndio wale msukuma jana kasema wapiga kelele ni watu wasiokuwa na kazi za kufanya na uhakika wewe mmoja wapo.
 
Huna uwezo chanya wa kudadavua hoja nzito mkuu.JF si sehemu sahihi wewe kuwepo na hii ni kulingana na comments zako kwenye huu uzi

Kama kupitia huu uzi umedhibitisha uwezo wako wa kufikiri mkuu huoni kama utakuwa unajichosha maana kupitia mwandiko wako nimeshafahamu uwezo wako!!😁😁
Nyinyi mnashida sana na kwa kauli yako ndio maana hamuwezi kuja kuchukua nchi hii. Wewe ukiona mtu anadhani yeye ni bora kuliko mtu mwingine basi ujue huyo anashida kama sio kiuchumi basi hayuko stable kifamily. Elimu yako kwangu sio umuhimu ila mtu anayedhani anajuwa kila kitu labda kasoma hii elimu yetu ya kukariri ndio matokeo yake haya. Asubuhi njema tafuta pesa utapata amani.....
 
Back
Top Bottom