Kilimo ni uti wa mgongo wa taifa ketu ambapo kilimo pekee kimeweza kutoa ajira kwa 70%. Kilimo ni biashara kwa sababu mkulima anaweza kuuza mazao anayolima kibiashara na kumtengenezea kipato. Na zaidi kilimo kinachangia 27% katika Pato la taifa.
Kwa kipindi kirefu kilimo kimeshindwa kwa namna au nyingine kumheshimisha mkulima lakini kipindi hiki Dkt.Samia amekipeleka kilimo kwenye viwango vya juu sana. Katika hili, mnyonge mnyongeni haki yake mpeni..
Kinavyozungumzwa kilimo ni vema yakaangaliwa maslahi na changamoto za wakulima kwa kuwa ndipo tutajua vilio na vicheko vya wakulima. Ningependa kuangalia upande wa changamoto na namna zilivyofanywa fursa za kumnufaisha mkulima.
Changamoto kuu zinazosemwa sana na wakulima ni ukosefu wa pembejeo(mbolea), ukosefu wa masoko na Bei za mazao kuwa chini, sio tu serikali imezitatua bali sasa kilimo kinafanyika kiushindani na kibiashara zaidi. Hii ni kuonesha ni kwa namna gani Dkt. Samia kadhamiria kukipaisha.
Serikali ya Dkt. Samia imepanga kukuza mauzo ya nje yatokanayo na kilimo kutika dola za kimarekani bilioni 1.2 mpaka kufikia dola bilion 5 mwaka 2030 na hapa serikali imeonesha ni kwa namna gani itavyohakikisha inaboresha kilimo kuweza kumnufaisha mkulima.
Kwa upande wa changamoto, nikianza na changamoto ya ukosefu wa pembejeo(mbolea) serikali katika Mwaka wa fedha 2022/2023 imetenga kiasi Cha shilingi bilion 150 kwa ajili ya kutoa ruzuku kwa mazao yote ya kilimo. Hiki ni kiwango kikubwa sana. Pia, serikali imedhibiti Bei ya mbolea ya kupandia kutoka 140,000 hadi 70,000 na mbolea za kukuzia kutoka 110,000 hadi 70,000 hii itasaidia wakulima kujikitika kwenye kilimo cha kisasa na kupata mazao mengi zaidi.
Changamo nyingine ambayo ni ukosefu wa masoko, serikali imerahisisha utolewaji wa vibali vya kusafirisha mazao nje hivyo wakulima wataweza kuuza mazao yao nje kwenye masoko ya uhakika. Pia, Serikali imerahisisha na kuboresha utambuzi wa masoko ya kimkakati kwa kushirikiana na shirika la chakula na kilimo duniani(FAO) ambapo wauzaji na wanunuaji hukutana. Uwepo wa masoko haya ya kimkakati unasaidia kukuza fursa za uwekezaji kwenye kilimo. Mfano wa masoko hayo ni soko la kibaigwa mkoani Dodoma.
Pia, katika hili la ukosefu wa masoko Serikali kupitia Mamlaka ya Afya ya mimea na viuatilifu(TPHPA) imepata cheti Cha ithibati ya kimataifa ambacho kitasaidia bidhaa kutoka nchini kutambulika kimataifa. Hii itasaidia mazao ya kilimo kupata masoko nje na kumsaidia mkulima moja kwa moja.
Changamoto nyingine ya Bei za mazao kuwa chini, hapa ndipo kilio Cha wakulima kwa muda mrefu kilikuwepo. Bei ni kichocheo kikubwa katika uwekezaji na Bei ya vyakula kupanda ni fursa na kukuza kilimo. Kilio hiki kimepata mfutaji machozi na Dkt. Samia amefanikisha ndoto ya mkulima kunufaika kutokana na kilimo kutimia. Kwa mtazamo wangu, kupanda kwa Bei ya mazao ya kilimo na vyakula sio mfumuko wa Bei ila ni kupanda kwa thamani ya kilimo.
Twendeni mbele turudi nyuma, Mhe.Rais Dkt.Samia amefanya mambo makubwa na mazuri kwenye sekta ya kilimo. Wakulima wanafuraha sana kipindi na ninaamini kilimo kitaajiri watu wengi zaidi kukiendelea kuwa na maboresho kwenye ya kilimo.
Tumuite mama shujaa wa kilimo lakini Mimi namuona Dkt Samia kama mchumi aliyehitajika sana kukinusuru kilimo na kuwafuta machozi wakulima.