Dkt. Samia, Mchumi aliyehitajika kukinusuru kilimo na kuwafuta machozi wakulima

Dkt. Samia, Mchumi aliyehitajika kukinusuru kilimo na kuwafuta machozi wakulima

Samia huyuhuyu Hangaya the chief of Sukumaland ni Mchumi? Kaanza lini?[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Kilimo cha kutegemea jembe la mkono na mvua zisizo tabirika kwenye karne hii ya 21, nacho ni cha kupongezana!

Kisa tu mmetoa vimbolea vyenu vya ruzuku, basi hatunywi maji!!
Itakua hauna taarifa za kutosha kuhusu kilimo mzee Tanzania inazidi kuendelea katika kilimo sasa hatuna kilimo cha kutegemea mvua tunalima kilimo cha umwagiliaji na ili kukamilisha mpango huu serikali inampango wa kuchimba visima 110 ili vitusaidie katika kilimo cha umwagiliaji na kingine usichokijua ukiachilia mbali mbolea ya ruzuku iliyosaidia kupunguza gharama za kilimo mkulima anapata faida zaidi akiuza mazao yake ukilinganisha na awali mkulima alikuwa hadhaminiki hii ndio maana halisi ya kilimo biashara
 
Hapa kwetu kilimo ni mkombozi pale unapokuwa huna jengine la kufanya au unapostaafu, hawakusomea kilimo popote lakini ni kuamka asubuhi na kuamua leo mimi nitakuwa mkulima. Hao wanaoamua ndiyo wamestaafu wamechoka na maisha ati ndiyo wanakwenda kuwa wakulima. Aidha vijana wanakimbia vijijini kuja mjini kufanya shughuli zisizoeleweka alimradi wamekimbia kilimo.

Wakulima hasa serious ni wachache.

Niliwahi kwenda nchi moja ya Scandinavia kwenye course moja ya kilimo na walituambia moja ya masharti yao ya kuwa mkulima basi lazima uwe umekwenda (enzi zile) course ya kilimo, bila ya hivyo huwezi kuruhusiwa kuwa mkulima.

Ni muda muafaka sasa angalau vijana wahamasishwe kujiunga na kilimo lakini kwanza wapewe mafunzo ya lile zao wanalotaka kulishughulikia ili kumfanya awe mkulima mzuri

Hayo yote yamefanyiwa kazi na Serikali ya Rais Samia Suluhu vijana wataenda kuongeza ujuzi kilimo ni ajira pia kilimo ni biashara vijana inatakiwa wachangamkie fursa zipo kwenye kilimo
325348179_1880860828925276_2017386258683486860_n.jpg
 
Back
Top Bottom