Hapa kwetu kilimo ni mkombozi pale unapokuwa huna jengine la kufanya au unapostaafu, hawakusomea kilimo popote lakini ni kuamka asubuhi na kuamua leo mimi nitakuwa mkulima. Hao wanaoamua ndiyo wamestaafu wamechoka na maisha ati ndiyo wanakwenda kuwa wakulima. Aidha vijana wanakimbia vijijini kuja mjini kufanya shughuli zisizoeleweka alimradi wamekimbia kilimo.
Wakulima hasa serious ni wachache.
Niliwahi kwenda nchi moja ya Scandinavia kwenye course moja ya kilimo na walituambia moja ya masharti yao ya kuwa mkulima basi lazima uwe umekwenda (enzi zile) course ya kilimo, bila ya hivyo huwezi kuruhusiwa kuwa mkulima.
Ni muda muafaka sasa angalau vijana wahamasishwe kujiunga na kilimo lakini kwanza wapewe mafunzo ya lile zao wanalotaka kulishughulikia ili kumfanya awe mkulima mzuri