Dkt. Samizi akomaa na mradi wa maji uliokwama wa Kifura, sasa kuanza kutoa huduma Agosti 31

Dkt. Samizi akomaa na mradi wa maji uliokwama wa Kifura, sasa kuanza kutoa huduma Agosti 31

BWANKU M BWANKU

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2019
Posts
377
Reaction score
435
DKT. SAMIZI AKOMAA NA MRADI WA MAJI ULIOKWAMA WA KIFURA, SASA KUANZA KUTOA HUDUMA AGOSTI 31.

Mbunge wa Jimbo la Muhambwe mkoani Kigoma Mhe. Dkt. Florence George Samizi anaendelea kusimama kidete kuwasemea wananchi wake pamoja na kutatua kero zao ili kusukuma maendeleo yao ambapo sasa amekomaa kufuatilia upande wa Serikali kuhakikisha mradi wa Maji katika kijiji cha Kifura kata ya Busagara unakamilika na kufanya kazi baada ya kutelekezwa na mkandarasi ukiwa asilimia 43 tu.

Mradi huo uliofikia asilimia 43 unatekelezwa na Nangali contract umetelekezwa kwa zaidi ya mwaka sasa baada ya kuwekewa jiwe la msingi na Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa.

Dkt. Samizi ameuliza swali bungeni leo Jumanne Mei 02, 2023 kwa Waziri wa Maji akitaka kujua ni lini mradi huo wa Kifura utakwamuliwa baada ya kukwama ukiwa asilimia 43 ili sasa wananchi wapate huduma ya maji.

Waziri wa Maji, Juma Aweso amesema Serikali imekaa na Mkandarasi wa mradi pamoja na Shirika la Enabel waliokuwa wanatekeleza mradi huo kutatua mgogoro wao na sasa wameshaelekeza kwa mkandarasi mradi huo aukabidhi Agosti 31 mwaka huu 2023 ili wananchi wapate huduma ya maji.
 

Attachments

  • VID-20230502-WA0017.mp4
    10 MB
Back
Top Bottom