Dkt. Sebi kielelezo cha Waafrika kukataliwa Tiba zao. Alikufa kifo chenye utata baada ya ugunduzi wa Dawa ya UKIMWI

Nimesoma mpaka mwisho nikitarajia orodha ya vyakula vyenye Alkali lakini wapi, nimeambulia limao tu.
Vitamin B3 ni supplement ya vyakula vyote hivyo unavyotafuta. Wagonjwa wa HIV wanaotumia dawa hizi wana mafanikio makubwa ya kudhibiti au kupona.

Uzuri wa vitamini B3 unatumia na RAV pamoja.
 
Kwanini wewe / sisi ambao lengo letu sio kama lao tusitumie ? Nadhani swali langu ni hili hakuacha hizo formula zake ?
Sababu wengi wetu hatuamini hizo tiba shauri ya kuwa brainwashed kuwa sii tiba sahihi. Na ndio point ya mleta mada ilipo
 
Sababu wengi wetu hatuamini hizo tiba shauri ya kuwa brainwashed kuwa sii tiba sahihi. Na ndio point ya mleta mada ilipo
Kwahio hizo formula zipo ?

Hivi unajua watu wangapi wanaamini hizi mambo mbadala (rejea kikombe cha babu), kwahio any pharamaceutical ambayo ni worth its salt (making money for its shareholders) hawawezi wakaacha hii fursa..., ila ndio hivyo dawa yoyote inahitaji research (long term) na kuhakikisha na kuhakikisha tena na tena na tena (mbali na kufanya hivyo unaweza ukawa sued na ukafirisiwa ukauza mpaka picha za ukutani)
 
Kuamini ama kutoamini kitu hutegemea na taarifa ulizopewa/ulizonazo juu ya kitu husika
 
Dr. Sebi ni Mmarekani Mweusi wala sio Mwafika. Alafu mitishamba haipo Afrika pekee bali ni dunia nzima.

Najua utaanza kusema porojo za kujikubali ila ngoja nikwambie tu kuwa Tiba asili za kiafrika bado zipo nyuma sana kwanza nyingi ni over dose.

Wenzetu wamejikita wanafanya tafiti ya tiba kulingana na mabadiliko ya tabia nchi na mwanadamu mwenyewe. Sasa sisi dawa ni ile ile tangu 1960 unafikiri ni sawa?, mwanadamu wa 1960 sio sawa na wa leo 2021.

Labda useme tujikite maabara tuje na kitu kinachoendana na dunia ya sasa. Mtu unakunywa alovera glasi ya nusu lita wakati kitu icho icho unakipata kwenye kidonge kidogo

Tiba asili ni nzuri ila ni sumu moja mbaya sana sababu haina tafiti na vipimo maalumu vya utumiaji hili lipo wazi.

Huyu huyu Dr. Sebi aliwaponda wachina kwa kula wali wakati ni chakula chao, alisahau jamii hazifanani.
 
....Acid kwa kiswahili ni tindikali....magonjwa mengi yanasababishwa na kula vyakula vyenye tindikali Acid....Limao ni mfano wa vyakula vyenye tindikali nyingi ingawa wengi tunadhani lina acid!!!! Limao ni msaada mkubwa kwa ini kwani husaidia kuondoa masumu mwilini......Total confusion!
 
"Mei 28, 2026 alikamatwa na kosa la utakatishaji pesa baada ya kumkamata na dola 37,000 mkononi bila maelezo kazipata wapi huku wakijua kabisa alikuwa anaingiza dola 3,000 kwa siku."

USIKU MWEMA WADAU
...Au mimi nimesoma vibaya..mbona ameandika Mei 28, 2006!
 
True that na kule juu kuna sehemu amesema Dr. Sebi alikamatwa mwaka 2026 ni makosa tu ya kiuandishi ila good observation kwakua si kila mtu anaweledi huo.
...Hapana amesema alikamatwa 2016!
 
Historia imekuacha kidogo hapa mjomba siyo Thabo mbeki ni Jacob Zuma ndiyo aliyepoteza madaraka yake akiwa madarakani kupitia panga la ANC
 
Historia imekuacha kidogo hapa mjomba siyo Thabo mbeki ni Jacob Zuma ndiyo aliyepoteza madaraka yake akiwa madarakani kupitia panga la ANC
Hebu fuatilia vizuri tena. Aliyepoteza ni Thabo mbeki kipindi hicho Jacob Zuma alikuwa makamu wake
 
Kuna siku nilikaa kuanzia saa 4 usiku mpaka saa 9 usiku naangalia interviews zake na lectures zake youtube. Sebi kweli alikua tishio kwa big pham companies. Kuna interview moja aligusia kuwa alialikwa na Rais Kikwete aje kutembelea Tz.
 
Dr sebi .
 
Kwanini wewe / sisi ambao lengo letu sio kama lao tusitumie ? Nadhani swali langu ni hili hakuacha hizo formula zake ?
Hakuacha Kwa sababu waliomuua walihakikisha hata familia wanaiogopesha
 
Hakuacha Kwa sababu waliomuua walihakikisha hata familia wanaiogopesha
Kwahio hatuna concrete evidence kwamba zilifanya kazi ?

Unajua mpaka dawa yako ikubaliwe kila mtu apewe lazima ufanya testing za kufa mtu na uweke data ili kujua side effects (kuponyesha pekee haitoshi) kwahio kama haliacha makabrasha hekima sio kulalamika ni kuyaendeleza na kufanya research; big pharamaceuticals badala ya kukuua watanunua formula zako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…