Dkt. Shelukindo aongoza ujumbe wa Tanzania kushiriki mkutano wa Kamati ya Siasa na Diplomasia ya SADC

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo ameongoza ujumbe wa Tanzania kushiriki Mkutano wa Kamati ya Siasa na Diplomasia (Inter-State Politics and Diplomacy Committee — ISPDC) ya SADC uliofanyika kwa njia ya mtandao tarehe 09 Februari, 2024.

Mkutano huo umeongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Jamhuri ya Zambia, Bi. Etambuyu Gundersen ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Makatibu Wakuu ya Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC.

Mkutano huo uliitishwa kujadili masuala ya kisiasa na diplomasia katika kanda. Aidha, Mkutano umetoa salamu za pole kwa Serikali na wananchi wa Jamhuri ya Namibia kufuatia kifo cha Hayati Dkt. Hage Geingob, Rais wa Jamhuri ya Namibia na Mwenyekiti aliyemaliza muda wake wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama kilichotokea hivi karibuni.

 
Kuna faida gani? Ishu, gani anaenda kuongelea? Manufaa gani ya kiuchumi, diplomasia tutapata?
Machawa wa CCM na kupenda kiki, mnaongelea vimambo vidogo vidogo tu, hamsemi jinsi tunavyoendelea kupopolewa kwenye mahakama za kimataifa, Jana tumeangukia pua tena, tunatakiwa kulipa bilioni 300!
Niki angalia hii clip, profesa wetu,
Anavyogalagazwa, inatia aibu!
Your browser is not able to display this video.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…