Ukitaka kujua siasa za Africa zinavyokwenda jaribu kuangalia siasa za Kenya utaona namna wanasiasa wanavyohama au kusaliti vyama lakini wanarudi, wanahamia chama kile na kile wanaungana na chama tawala kisha chaguzi zingine wanarudi. Muangalie hata Ruto, Mudavadi, Kalonzo nk nk.Alisahau nini Chadema? Si aliapa ameachana na siasa?
Hivyo hata Slaa kurudi Chadema sio suala la ajabu, hata Mashinji au Zito kujiunga Chadema is not an issue. Watu wanachoangalia potentiality. Kwa hivi sasa Dr Slaa anaonekana kuwa na nyota ya kukubalika katika jamii hivyo akirudi Chadema ni dhahiri chama kikanufaika sana. Pia akiachwa akaenda chama kingine tuseme ACT halafu wanasiasa wengine wenye ushawishi wakaamua kumfuata kama vile wale wa Covid nk itaikosesha Chadema kura na wabunge kwa kiasi kikubwa sana katika uchaguzi na kuwapa faida ccm na chama atakachokwenda.
Niseme tu kuwa Dr Slaa kwa sasa ni Mchezaji muhimu sana katika timu yoyote itakayomsajili. Dr ni Chama na Mayele kipindi hiki asichukuliwe kama Morrison au Sawadogo. JAPO ALIFANYA USALITI KAMA FEISAL SALUM