Tetesi: Dkt. Slaa adaiwa kugomewa kurudi CHADEMA

Alisahau nini Chadema? Si aliapa ameachana na siasa?
Ukitaka kujua siasa za Africa zinavyokwenda jaribu kuangalia siasa za Kenya utaona namna wanasiasa wanavyohama au kusaliti vyama lakini wanarudi, wanahamia chama kile na kile wanaungana na chama tawala kisha chaguzi zingine wanarudi. Muangalie hata Ruto, Mudavadi, Kalonzo nk nk.
Hivyo hata Slaa kurudi Chadema sio suala la ajabu, hata Mashinji au Zito kujiunga Chadema is not an issue. Watu wanachoangalia potentiality. Kwa hivi sasa Dr Slaa anaonekana kuwa na nyota ya kukubalika katika jamii hivyo akirudi Chadema ni dhahiri chama kikanufaika sana. Pia akiachwa akaenda chama kingine tuseme ACT halafu wanasiasa wengine wenye ushawishi wakaamua kumfuata kama vile wale wa Covid nk itaikosesha Chadema kura na wabunge kwa kiasi kikubwa sana katika uchaguzi na kuwapa faida ccm na chama atakachokwenda.

Niseme tu kuwa Dr Slaa kwa sasa ni Mchezaji muhimu sana katika timu yoyote itakayomsajili. Dr ni Chama na Mayele kipindi hiki asichukuliwe kama Morrison au Sawadogo. JAPO ALIFANYA USALITI KAMA FEISAL SALUM
 
Shida ni moja mkuu ,Slaa akirudi CDM ,kuna potential vita ya Urais inaanza ,wengine wanaona inaweza kuwadhoofisha badala ya kuwasogeza mbele
 
Kiongozi, usiamini yanayosemwa na wanasiasa mbele ya camera na mic, ninachokwambia nina uhakika nacho , nimepataje hizi taarifa ?hii itabaki kuwa siri yangu , lakini Lissu ana jua na dhamira yake itamsuta kama atakana, Mnyika na mbowe wanajua , it was a heated talk na exchange ya maneno magumu
 
Wasaliti wote hawapaswi kurejea.
Ni sawa na mwanamke aliyekukimbia ulipokosa pesa
Wanasiasa hawaangalii hayo mkuu, wanaangalia mtaji wa kisiasa ni watu Slaa ana upepo kwa sasa, Lissu kama kazimika hivi ,urais 2025 mwenye mvuto kwa CDM ni slaa ,tatizo hawajamalizana bado
 
King maker wako jana kachachafwa na majaji anajiumauma tuu meno. Mi sikuona kama kulikuwa na umuhimu wa kuongelea jambo ambalo aliongea akiwa anaelewa na anaakili timamu kwani ni kesi ngapi amepiga simu kisutu yeye na maswahiba wake?
Rostam pamoja na madhaifu yake , ni mtu wa mikakati sana. Hata kuomba radhi ni strategy pia
 
Mbowe anaamini atawapa wabunge wengi akigombea urais 2025 ,lakini Lissu anaona kama kuja kwa Slaa kutamfifisha zaidi
 
Nakuunga mkono, sasa hio ni kama watamruhusu maana kuna vita vya urais vimeanza CDM ,Lissu anaona ujio wa Slaa ni nongwa kwake
 
Tunamtaka Dr Slaa Chadema.... Lissu ni muhuni kama wahuni wengine!
 
Porojo za kijinga
 
Hii umejitungia tu ili kuleta mtafuruku Chadema, sakata la DP World limewachanganya kweli kweli
 
CDM kiboko yaani wao zoazoa tu muhimu wafike wanakotaka, chama kiboko hata hujui kinasimamia nini. wabunge 19 tu mapaka watamaliza muda wao wamewashindwa kina mama ahhhhh
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…