Confederate Spy
JF-Expert Member
- Sep 6, 2012
- 426
- 145
WANABODI,
Usalama wa viongozi wa chama kikuu cha upinzani Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) upo hatarini.Akiwa njia ni kutokea Iringa, Dr. Slaa amefuatiliwa na Gari aina ya Landcruiser yenye vioo vya giza (Tinted) lenye namba za usajili T963 ABN. Awali waliokua ndani ya gari la Dr. Slaa hawakushtuka sana japo waliona kuna mchezo wa gari hilo kuwapita kwa kasi na kisha kupunguza mwendo ghafla na kisha gari la Dr. Slaa kuwapita tena.Walichukulia kama vile ni mchezo wa kawaida hadi walipofika Morogoro na kushtuka zaidi na kuanza kuchukua tahadhari kwa kunakili namba ya gari hilo
Walipofika kibaha ilibidi watoe taarifa kwa askari wa usalama barabarani.
Dr. Slaa na maofisa wa chama akiwemo afisa habari walishtuka zaidi walipofika njia panda ya Tamko-Bunju ambayo mara nyingi hutumika kunapokua na foleni kubwa ya maghari(Traffic Jam) na kulikuta gari hilo likiwasubiri
Baada ya kufuata barabara kuingia jijini Dar Es Salaam gari hiyo ghafla ikaingia nyuma ya gari aliyokua akitumia Dr. Slaa aina ya Landcruiser yenye namba za usajili namba T834 BJG. Ndipo afisa wake aliyekua ndani ya gari akapanda juu (Roof Top) na kufanikiwa kulipiga picha gari hilo.
Kuona hilo likifanyika gari hilo likapaki pembeni na ghafla likaondoka na kupotea hadi muda huu walipoingia Ubungo.
Sasa katika mazingira haya taifa linaelekea wapi? Kama watu wanafuatiliwa na kufanyiwa vituko mchana kweupe usalama wa Watanzania na hasa wanaharakati na viongozi wa upinzani Tanzania uko wapi? Mambo haya ni bora yafahamike mapema na watanzania wayajue. Hili ni tukio lisilo la kawaida kipindi hiki ambacho umma umekosa imani (loose confidence) na vyombo vya dola vinavyotumika kwa matakwa ya kisiasa.
Kuna matukio kadhaa yametokea miaka na miezi michache iliyopita yanayotoa taswira mbaya juu ya usalama wa raia na baadhi ya viongozi wanaokosoa utawala. Siku za karibuni Viongozi wa CHADEMA wamekua wakiwindwa sana na tayari chama hiki kikuu cha upinzani kilishatoa tuhuma kwa Usalama wa Taifa na baadhi ya viongozi wa juu serikali kuhusika katika mipango haramu ya kukihujumu chama hicho na hata kufikia hatua ya kuwabambikia kesi viongozi wake.
- Uelewa wangu juu ya kundi la watu wasiojulikana
~ Matukio ya Watu kupotea na wengine kudaiwa kutekwa, nini kinaendelea kuhusu usalama wa raia
- Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana

PIA SOMAWanaJF,
Mimi Dr Slaa ambaye kwa siku 4 nimekuwa na ziara ya mkoa wa Iringa,Mbeya na Njombe nilikuwa narudi Dar jana baada ya kulala Iringa mjini kutokea Njombe.
Tukio linaloelezwa ni la kweli na nimelishuhudia mwenyewe. Nimeingia kwa jina langu na ID yangu ili kuondoa dhana ya Spinning.
Namshukuru sana aliyetoa Taarifa, na kuliwasilisha kama ilivyotokea bila kuongeza wala kupunguza kitu.
Tuliondoka Iringa majira ya saa 3.30 hivi. Kwa mwanzo hatukutambua kitu, ila mara ya kwanza tuliona gari hilo likitupita kwa kasi km kama 20 hivi baada ya kupita junction ya Ipogolo. Tuliona kawaida. katika hatua hiyo tulijua ni wasafiri wenzetu. baadaye tukawa tunawapita, wanatupita kasi na kupotea, lakini baada ya muda tunawakuta na kutupisha. hatukustuka sana, japo kuanzia Ilula tukaanza kuulizana.
Mlima Kitonga wakatipita kwa kasi sana japo mbele yetu kulikuwa na semitrela kama 4 zikiteremka pole pole sana na nabasi 2 kwenye kona moja basi lililpkuwa mbele yetu kikakwaruzwa na lori lililokuwa lunapanda. Tukachukua tahadhari sana.
Tulipovuka daraja la Mtp Ruaha tukalikuta L/cruiser hiyo imesimama pembeni lakini abiria wake wote walikuwa ndani. tulipolikaribia likaondoka kwa kasi. kidogo tulistuka. sisi tukaamua makusudi kusimama na kununua vitunguu. Tulipofika Mikumi mjini tukalikuta tena likienda taratibu. kuanzia hapo tukawa makini sana hasa kwenye kona na au vichaka vikubwa. kimsingi tukajiweka kwenye hali ya tahadhari kubwa.
Moro tuliingia Petrol Station nao pia wakaingia nyuma yetu lakini hawakujaza mafuta. Punda wakaondoka direction ya Dodoma. Ikumbukwe sisi tumetoka Njombe tumetangaza tunaenda Kongwa ,Jimbo la Ndugai. mimi nikakapata dharura nikapaswa kurudi Dar. hivyo baada ya mufuta tukafuata direction ya Dar. Punde likatokeza tena na kutupita. Tukalipita kidogo kabla ya Chalinze. Baada ya Chalinze hatukuliona tena mpaka tulipolikuta Junction ya Tamko limepaka. mata nyibgine huwa natumia hiyo junction badala ya kuingia Jijini. Na kweli driver akapiga indicator nyingie hapo. nikaagiza tuelekee jijini Dar. ndipo ghafla nao wakaingia barabarani nyuma ya gari langu kabisa. ndipp nikaagiza afisa wangu apande juu ya gari letu -roof top na kulipga picha. kuona hivyo ghafla likatoka pembeni na kupaki. sisi tukaendelea, ndipo mbele kidogo tukakuta askari walioko zamu yao ya kawaida wakatusimamisha na tukawapa taarifa ya halu hiyo.
Sasa katika mazingira hayo kuna mtu bado anafikiria ni spinning anaweza kuamini hivyo hatuwezi kumlazimisha.
Natumaini nimefafanua ya kupotosha. Nawashukuru wote waliotupa pole. Tunaanza na Mungu tunabaki na Mungu. Hatumwogopi Binadamu na mapambano ya ukombozo hayatakoma kwa vitisho vya aiina hiyo, ndiyo kwanza vinatupa ari na mori.