Huwezi ukasema kuwa hiyo ni spinning kama wewe hukuwepo! Inawezekana kweli hao watu walikuwa wanamfuata au inawezekana walikuwa hawamfuati. Hata hivyo, viashiria tulivyoonyeshwa hapo juu, vinaonyesha kuwa hao watu kwenye LCruiser walikuwa na kamchezo fulani. Katika hali ya siku hizi iliyopo Tanzania, kuna haja ya kila mwananchi kuwa macho kwa vile imedhihirika kwamba usalama wa raia hauna uhakika (Rejea kutekwa kwa Dr. Ulimboka, Kibanda, kifo cha Mwangosi n.k.)
Kuna methali ya Kiswahili isemayo, 'Aliyeumwa na nyoka, akiona nyasi hustuka'!