Dkt. Slaa Afuatiliwa na watu wasiojulikana kutoka Iringa hadi Dar Es Salaam

Kubwa zima pumbavu, jirekebishe kwa manufaa ya wanao na wajukuu
Yupi kati yangu na mimi anayetakiwa kujirekebisha?. Yule anayerusha matusi bila kujali kama hili ni jukwaa la watu wote bila kujali kama ni watoto au wazee au mimi ambaye naweka hoja za kistaarabu pamoja na kwamba siyo wote watakubaliana na mimi.
 
Chadema punguzeni uoga mh! kila kitu mana tafuta nyinyi tu yani anaetaka kukuzuru kutoka iringa paka dar anakufata nyuma tu mh!!!!!
 
Soma kwa utulivu,wamefuatiliwa na pia "wakatanguliwa" kwa nyakati tofauti.

Pia kudhuriwa kunaweza kuwa kwa namna nyingi,kwa mfano kuwasababishia ajali nk.
 
Spinning at the highest order.

Hivi wewe kwa akili zako kama kweli kuna watu wanataka kuwadhuru viongozi wa CHADEMA watahangaika kwa jinsi unavyoelezea hapa.

Siyo kila jambo ni siasa siasa siasa. Siku hizi mwanasiasa hata akikumbana na vibaka anadai wanasiasa wanamfanyizia.

Jifunzeni kutokuwa wepesi wa kupata majibu kabla ya uchunguzi makini.

Cha kushangaza hao hao watu wa usalama mnaowatuhumu kwa matukio mbali mbali yanayowahusu, ndiyo hao hao mnaotueleza mlienda kulipoti tukio.

Yaani umeamua kuja na ID mahususi kwa ajiri ya SPINNING za kiulinzi.

Kweli tutasikia mengi.
hebu twambie ni njia gani zinazoweza kutumika nje ya hizo unazo kataa.
 
Uko Lumumba unajitahidi sana kupost, wewe unacho pinga ni kipi? so unatakatusikubaliane na mleta maada tukubaliane na wewe? Au wewe ndo mhusika mwenyewe?
Ninatoa mawazo yangu kama ulivyo nawe na uwezo wa kufanya hivyo kwa mawazo yako..

Kama hizi siyo spinning. Huyu huyu mleta mada anaonekana kama alikuwa ndani ya gari na Dr. Slaa pamoja na viongozi wengine na ofisa habari. kwani si wote hawa wana VERIFIED ID hapa. Kwa nini wamtume huyu ambaye inavyoonekana amejiandikisha maksusi leo kwa kazi hii?
 
hebu twambie ni njia gani zinazoweza kutumika nje ya hizo unazo kataa.
Lwakatare anazijua zaidi yangu. unfortunately, bado yuko gerezani lakini pia kama una haraka unaweza kutembelea video yake YouTube kupata maelekezo na njia mbadala
 
Bavicha akili zao vituko sana. Hivi habari sensitive kama hii ni ya kuletwa na ID ambayo siyo verifies kweli?

Kesho utasikia kiongozi mmoja wa chadema anasema hiyo namba ya gari lililotajwa lilikuwa lake na kwamba habari imelengwa kumchafua.

Wewe mleta mada kwa vile unajua mambo tokea Iringa mpaka Dar es Salaam maana yake ulikuwa na Dr. Slaa sasa kwanini usichukue responsibility ya kusema kilichotokea?

Kinachochekesha zaidi vijana wa bavisha hapa washaingia line tayari. Yaani mlaghaika kilaiiiiiiiiini...

Did you write in a hurry? Keep calm boy!
 
Spinning at the highest order.

Hivi wewe kwa akili zako kama kweli kuna watu wanataka kuwadhuru viongozi wa CHADEMA watahangaika kwa jinsi unavyoelezea hapa.

Siyo kila jambo ni siasa siasa siasa. Siku hizi mwanasiasa hata akikumbana na vibaka anadai wanasiasa wanamfanyizia.

Jifunzeni kutokuwa wepesi wa kupata majibu kabla ya uchunguzi makini.

Cha kushangaza hao hao watu wa usalama mnaowatuhumu kwa matukio mbali mbali yanayowahusu, ndiyo hao hao mnaotueleza mlienda kulipoti tukio.

Yaani umeamua kuja na ID mahususi kwa ajiri ya SPINNING za kiulinzi.

Kweli tutasikia mengi.

Huwezi ukasema kuwa hiyo ni spinning kama wewe hukuwepo! Inawezekana kweli hao watu walikuwa wanamfuata au inawezekana walikuwa hawamfuati. Hata hivyo, viashiria tulivyoonyeshwa hapo juu, vinaonyesha kuwa hao watu kwenye LCruiser walikuwa na kamchezo fulani. Katika hali ya siku hizi iliyopo Tanzania, kuna haja ya kila mwananchi kuwa macho kwa vile imedhihirika kwamba usalama wa raia hauna uhakika (Rejea kutekwa kwa Dr. Ulimboka, Kibanda, kifo cha Mwangosi n.k.)

Kuna methali ya Kiswahili isemayo, 'Aliyeumwa na nyoka, akiona nyasi hustuka'!
 
Naona kwa sababu Dk Slaa aliwachana sana TISS Pamoja na ikulu kwa ujumla, pale kwenye mkutano mkubwa wa hadhara Mbeya.
 
Huwezi ukasema kuwa hiyo ni spinning kama wewe hukuwepo! Inawezekana kweli hao watu walikuwa wanamfuata au inawezekana walikuwa hawamfuati. Hata hivyo, viashiria tulivyoonyeshwa hapo juu, vinaonyesha kuwa hao watu kwenye LCruiser walikuwa na kamchezo fulani. Katika hali ya siku hizi iliyopo Tanzania, kuna haja ya kila mwananchi kuwa macho kwa vile imedhihirika kwamba usalama wa raia hauna uhakika (Rejea kutekwa kwa Dr. Ulimboka, Kibanda, kifo cha Mwangosi n.k.)

Kuna methali ya Kiswahili isemayo, 'Aliyeumwa na nyoka, akiona nyasi hustuka'!
Viashiria vinavyoonyesha hapo juu ndiyo viashiria vinanifanya nipate dokezo hili.

Huyu mleta thread, amejuaje kama aliyekuwa anafuatiliwa ni Dr. Slaa wakati anadokeza pia kuwa gari lilikuwa na maofisa wengi wa CHADEMA. Huoni kama anataka kuileta habari yake kwenye centre stage kwa kulihusisha jina la Dr Slaa as a main character na ndiyo iwe Heading ili jamii iguswe na habari yake. THIS IS PURE SPINNING.
 
You seem to be too desperate for power!!

Uongozi mwanana wa kuongoza jamii unakuja automatically kwa mapenzi ya waongozwa. Mwl. Nyerere alisema kiongozi mzuri ni yule asiyetaka kuongoza. Ninyi kwa sasa inavyoonekana mnataka kuongoza kwa hali na mali.

Hizi spinning mnazozianzisha zitakuja kuwarudieni ninyi wenyewe. Historia ya chaguzi nyingi za nchi za Afrika imebainisha hili. You're setting the spinning bar very high kiasi kwamba hata mkiingia madarakani hamuwezi kuwapa wananchi kile mnacho spin kucha kutwa kama kinawezekana. otherwise, tunaanza kuona kama mko na mission za kutaka kujinufaisha kibinafsi

kachukue ujira wako lumumba,ukakojoe ulale MwanaDiwani
 
Last edited by a moderator:
WANABODI,

Usalama wa viongozi wa chama kikuu cha upinzani Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) upo hatarini.Akiwa njia ni kutokea Iringa, Dr. Slaa amefuatiliwa na Gari aina ya Landcruiser yenye vioo vya giza (Tinted) lenye namba za usajili T963 ABN. Awali waliokua ndani ya gari la Dr. Slaa hawakushtuka sana japo waliona kuna mchezo wa gari hilo kuwapita kwa kasi na kisha kupunguza mwendo ghafla na kisha gari la Dr. Slaa kuwapita tena.Walichukulia kama vile ni mchezo wa kawaida hadi walipofika Morogoro na kushtuka zaidi na kuanza kuchukua tahadhari kwa kunakili namba ya gari hilo

Walipofika kibaha ilibidi watoe taarifa kwa askari wa usalama barabarani.

Dr. Slaa na maofisa wa chama akiwemo afisa habari walishtuka zaidi walipofika njia panda ya Tamko-Bunju ambayo mara nyingi hutumika kunapokua na foleni kubwa ya maghari(Traffic Jam) na kulikuta gari hilo likiwasubiri

Baada ya kufuata barabara kuingia jijini Dar Es Salaam gari hiyo ghafla ikaingia nyuma ya gari aliyokua akitumia Dr. Slaa aina ya Landcruiser yenye namba za usajili namba T834 BJG. Ndipo afisa wake aliyekua ndani ya gari akapanda juu (Roof Top) na kufanikiwa kulipiga picha gari hilo.

Kuona hilo likifanyika gari hilo likapaki pembeni na ghafla likaondoka na kupotea hadi muda huu walipoingia Ubungo.

Sasa katika mazingira haya taifa linaelekea wapi? Kama watu wanafuatiliwa na kufanyiwa vituko mchana kweupe usalama wa Watanzania na hasa wanaharakati na viongozi wa upinzani Tanzania uko wapi? Mambo haya ni bora yafahamike mapema na watanzania wayajue. Hili ni tukio lisilo la kawaida kipindi hiki ambacho umma umekosa imani (loose confidence) na vyombo vya dola vinavyotumika kwa matakwa ya kisiasa.

Kuna matukio kadhaa yametokea miaka na miezi michache iliyopita yanayotoa taswira mbaya juu ya usalama wa raia na baadhi ya viongozi wanaokosoa utawala. Siku za karibuni Viongozi wa CHADEMA wamekua wakiwindwa sana na tayari chama hiki kikuu cha upinzani kilishatoa tuhuma kwa Usalama wa Taifa na baadhi ya viongozi wa juu serikali kuhusika katika mipango haramu ya kukihujumu chama hicho na hata kufikia hatua ya kuwabambikia kesi viongozi wake.
Karibu sana mkuu. Ila siku nyingine ukitumwa kuandika propaganda waambie wawe makini na wanachukutuma. Hiyo namba uliyoandika ni namba ya gari la chadema ambayo hutumika maalum wakatiwa misafara ya viongozi wa chama hicho. Ni namba ambayo hubadilishwa pindi safari ikifika. Aghalabu hutumika kwa nadara sana hasa pale ambapo kunajengeka hisia kuwa viongozi wapo hatarini
 
WANABODI,

Usalama wa viongozi wa chama kikuu cha upinzani Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) upo hatarini.Akiwa njia ni kutokea Iringa, Dr. Slaa amefuatiliwa na Gari aina ya Landcruiser yenye vioo vya giza (Tinted) lenye namba za usajili T963 ABN. Awali waliokua ndani ya gari la Dr. Slaa hawakushtuka sana japo waliona kuna mchezo wa gari hilo kuwapita kwa kasi na kisha kupunguza mwendo ghafla na kisha gari la Dr. Slaa kuwapita tena.Walichukulia kama vile ni mchezo wa kawaida hadi walipofika Morogoro na kushtuka zaidi na kuanza kuchukua tahadhari kwa kunakili namba ya gari hilo

Walipofika kibaha ilibidi watoe taarifa kwa askari wa usalama barabarani.

Dr. Slaa na maofisa wa chama akiwemo afisa habari walishtuka zaidi walipofika njia panda ya Tamko-Bunju ambayo mara nyingi hutumika kunapokua na foleni kubwa ya maghari(Traffic Jam) na kulikuta gari hilo likiwasubiri

Baada ya kufuata barabara kuingia jijini Dar Es Salaam gari hiyo ghafla ikaingia nyuma ya gari aliyokua akitumia Dr. Slaa aina ya Landcruiser yenye namba za usajili namba T834 BJG. Ndipo afisa wake aliyekua ndani ya gari akapanda juu (Roof Top) na kufanikiwa kulipiga picha gari hilo.

Kuona hilo likifanyika gari hilo likapaki pembeni na ghafla likaondoka na kupotea hadi muda huu walipoingia Ubungo.

Sasa katika mazingira haya taifa linaelekea wapi? Kama watu wanafuatiliwa na kufanyiwa vituko mchana kweupe usalama wa Watanzania na hasa wanaharakati na viongozi wa upinzani Tanzania uko wapi? Mambo haya ni bora yafahamike mapema na watanzania wayajue. Hili ni tukio lisilo la kawaida kipindi hiki ambacho umma umekosa imani (loose confidence) na vyombo vya dola vinavyotumika kwa matakwa ya kisiasa.

Kuna matukio kadhaa yametokea miaka na miezi michache iliyopita yanayotoa taswira mbaya juu ya usalama wa raia na baadhi ya viongozi wanaokosoa utawala. Siku za karibuni Viongozi wa CHADEMA wamekua wakiwindwa sana na tayari chama hiki kikuu cha upinzani kilishatoa tuhuma kwa Usalama wa Taifa na baadhi ya viongozi wa juu serikali kuhusika katika mipango haramu ya kukihujumu chama hicho na hata kufikia hatua ya kuwabambikia kesi viongozi wake.

watakuwa ni waumini wake hawamuoni church!!!!
 
Back
Top Bottom