Tunaona, tunasikia na tunashuhudia udharimu mwingi sana ukifanyika dhidi ya wanyonge wa Tanzania na watetezi wao. Ninadhani sasa kama ni kusikia na kuona tumesikia na kuona mengi yakipangwa na kutekelezwa kibabe. Hii ni kutokana na serikali kudharau uma wa Watanzania kwamba ni wajinga, waoga na maskini wasiokuwa na uwezo wa kufanya chochote. Ni watu wa makelele lakini hawana vitendo. Tutalendelea kushuhudia mipango dharimu ikitekelezwa hadi lini? Ni kweli kwamba hakuna cha kufanya zaidi ya kupiga kelele ambazo zilishasemwa ni zua chura wala hazimzuii ng;ombe kunywa maji?Naomba sana Watanzania tuungane pamoja na kuliona hili kwamba tatizo letu si vyama vya siasa wala si umaskini na ujinga wetu. Tufugnuke tu kwa hatua hii moja na kuona kwamba kinachotusumbua ni kiongozi mkuu wa serikali ilyoko madarakani. Huyu mtu angekuwa ni binadamu mwenye kujali, asingefurahishwa na kusimamia uharamia huu. Na kama asingekubaliana waliochini yake pia wangefuata nyayo zake hata kama ni kwa unafiki. Viongozi wa vyama vya siasa, bunge, serikali na sekta binafsi wangecheza ndani ya mfumo ule ule wa kuchukia na kukemea ufirauni kwa dhati.Sasa kwa kuwa hali ni kama hivi, nidhahiri kwamba sasa Watz tunamalizwa mmoja mmoja. Na pasipo kufanya jambo mwaka 2015 ni mbali na hadi uchaguzi nchi hii itakuwa imebakia na wale wanafiki kwa jk bila kujali elimu, wala vyama na hivyo kuendelea kwa ubeberu huu wa ki mafia tunaouona.NINANOMBA SASA WATANZANIA TUFIKA MAHALI TUACHE KUPIGA KELELE ZILIZODHARAULIWA NA AMBAZO HAZIATHIRI KITU ZAIDI YA KUSABABISHA MAUMIVU KWA KILA MSEMAJI NA FAMILIA YAKE NA KUACHA NCHI PAISPO WATETEZI.NINAOMBA NDUGU ZANGU TUPASHANE HABARI HAPA KWA SASA NI WAKATI WA KUCHUKUA HATUA ZA VITENDO. NAOMBA TUAMBIZANE KWA KUZINGATIA HAKI ZA KUISHI ZA KILA MTU, NI HATUA GANI SASA TUNATAKIWA TUCHUKUE , HATUA ZA MWANZO. KUSEMA KUMESHINDWA. NA HATUA YA PILI IWE IPI NA NGAZI INAYOFUATA NI IPI ILI KUHAKIKISHA TANZANIA HURU YA WATANZANIA INAPATIAKANA.