Kamanda Asiyechoka
JF-Expert Member
- Sep 13, 2020
- 3,315
- 5,058
Mwambata wa 'SAUTI YA WATANZANIA' na Mwanaharakati Dkt. Wilbroad Slaa, ameshindwa kufanya mkutano wake na waandishi wa habari uliotakiwa kufanyika mapema Jumatatu hii (Oktoba 09.2023) jijini Mbeya baada ya kuchukuliwa na maofisa wa Jeshi la Polisi kutoka hotelini alipofikia kwenda Ofisi ya upelelezi (RCO) mkoani humo kwa ajili ya mahojiano kwa tuhuma za kufanya mkusanyiko usio halali huko Busokelo Rungwe mkoani Mbeya mnamo Oktoba 08, 2023.