Dkt. Slaa akamatwa kwa kufanya mkusanyiko usio halali huko Busokelo Rungwe

Dkt. Slaa akamatwa kwa kufanya mkusanyiko usio halali huko Busokelo Rungwe

Nakiri wazi kwamba Mimi ni miongoni mwa Watanzania wanaokupenda Sana na ambao wanavutiwa Sana na wajihi wako.

Nilianza kukupenda wakati ukiwa mbunge na wakati huo nilikuwa mwanafunzi wa level ya secondary. Nilivutiwa Sana hoja zako bungeni Na namna ulivyokuwa ukitetea raslimali za nchi kwa serikali kuingia mikataba mibovu.
Kwa mantiki hiyo niligundua kwamba wewe ni moja ya Watanzania wachache waliojaliwa akili na mwenyezi Mungu.

Umesimama imara kutetea bandari zetu,umesimama imara kuwaelimisha Watanzania kuhusu katiba, umesimama imara kuwatetea Watanzania. Mwenyezi mungu akubariki Sana. Wewe ndiye mzalendo wa kweli,wewe ndiye kiongozi wa kweli.

Hawa wanaokukamata leo watapita tu kama walivyopita wajinga wengine. Dr.Slaa nikuhakikishie tu kwamba kabla ya kuwa askari Hawa ni Binadamu kwanza hivyo kama wamejisahau kwamba wao ni Binadamu kabla ya uaskari ,mungu analojibu na mwisho wao.

Naamini mungu amechukizwa na watu wanaokamata Watanzania hivyo hasa wale wanaotetea na kuipigania nchi. Hawa siyo Askari Bali ni watesi. Hawa siyo viongozi ni mafisadi. Kumbe wanaimba wimbo wa taifa "mungu ibariki Tanzania" kinafiki. Kumbe wanaimba "dumisha uhuru na umoja "kinafiki leo wanaligawa taifa.

Dr.Slaa,pamoja na kwamba wamekuondolea hadhi ya ubalozi,wewe Bado ni balozi na kumbukumbu zipo na zitabaki kwamba umewahi kuiwakilisha Tanzania nchini Sweden. Uliteuliwa na Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania wa awamu ya Tano na kuapishwa.

Mimi naamini kwamba Rais Magufuli alikupenda Sana na alikuamini Sana. Na alikupenda kwa uwezo wa akili yako na uzalendo wako. Moja ya sifa ya Rais Magufuli ilikuwa ni akikuona una akili alikuwa anakuamini na kukupenda mno.

Mungu hawezi kushindwa na mafisadi analo jibu kwao,tafadhali usirudi nyuma ipiganie nchi yako na nchi itakuhifadhi katika makazi yako ya milele. Ni udongo huu huu wa Tanzania ndiyo utakuzika. Hawa watesi walikuja na watapita lakini nchi itawahukumu siku za mwisho wa uhai wao.

Sisi Watanzania wenye akili tunawaona na tunayo maamuzi yetu huko mbele.

Dkt. Slaa aluta continua. Wewe ni shujaa misri ya samora machel,wewe ni mzalendo wa kweli kama Julius Nyerere. Wewe ni mwamba kama Magufuli.

Enyi watesi maisha ni mapito,kaburi ni tajiri.

Zidumu fikra za Dkt. Slaa.🇹🇿
 
Lowassa ndo aliwavunja moyo vijana Kwa kuwahakikishia kuwa hatoibiwa kura sababu ye ndo alikuwa engineer wa wizi,

Walipotangaza mshindi mwingine, hakutokea.

Slaa asisingiziwe.
Wilbroad Slaa ni mwasisi wa siasa chafu Tanzania alihamasisha UKAWA na baada ya hapo alikuwa anatamani yeye ndiye awe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania huku ndani ya huo huo UKAWA kulikuwa mtu mwingine mashuhuri Ibrahim Lipumba ambaye naye kwa namna yoyote ile hakutaka mtu mwingine agombee Urais.Baada ya Mwenyekiti wa UKAWA kulitambua hilo waliweka kikao na kumtambulisha Lowasa kama mgombea halali wa Urais ndani ya UKAWA na wote akiwemo Slaa na Lipumba walibariki.Lakini baada ya hayo kwa kuwa ni Mungu walimhukumu Lowassa moja kwa moja na wakajitoa kwenye UKAWA na kujiunga na Chato mla watu.
 
Lowassa na Slaa nani msaliti?
 
kwi kwi kwi ! wakiweza wamfunge kabisa huyu, kama sio yeye na Lipumba leo hii tungekua mbali sana kidemokrasia, matokeo yake sasa tunaanza tena upya!
Mngekuwa mbali kwa kusogezwa na lowasa? Akili zingine hizi!
 
Safi sana, ndiye aliyesababisha mpaka sasa Chama changu kuwa madarakani.
 
Back
Top Bottom