Dkt. Slaa akatalika kila mahali na kutengwa na kila mtu

Kumbuka alikuwa padri wa kikatoliki, sio mnafiki ila mkweli. Ukweli ndio unaomfanya aonekane mbaya. Siku akishika dola mtashangaa na maneno yenu yasiyokuwa na ukweli.
Siyo kila mtu anaweza kuwa Rais .Dr Slaa Hawezi kuwa Rais wa Nchi yetu
 
Hawezi mzidi yule anayeuza bandari za nchi hii kwa wapwa zake Dubai.
Wewe ni mwana kwaya wa kanisa katoliki eeh?

Mitaani huku wimbo umebuma huo.

Sasa hivi umebaki kuwa pambio la kanisa katoliki kila Jumapili.
 
Naamini kila litokalo kwako lina mrengo wa udini
Kama kwa "udini" unamaanisha Uislam, hujakosea kabisa. Uislam ni mfumo kamili na bora kabisa wa maisha - usisahau.

Unataka niwe kama wewe usiye na dini?
 
Hakuna binadamu aliye mkamilifu, ila DR. Slaa leo hii ana HOJA ya msingi sana kuhusu uwekezaji wa hovyo ndani ya nchi yetu, ASIKILIZWE.
 
Hivi nyie watu hamchoki na udini? Kila siku ni chokochoko kwa kanisa katoliki? Hamjazuiwa, mnaweza kubatizwa.

Alfu ndugu yenu huyu Lucas kila siku anaandika pumba. Nilimsoma kwa Tulia, mtu asiyefuatilia siasa za Tanzania angedhani huyo Tulia anapedwa mithiri ya Malaika, kumbe ni mwanasiasa aliyebebwabebwa kufikia ngazi aliyopo. JPM hayupo tena, huyu mwenzetu anajitolea kumubeba badala yake jpm, Ila ni bahati mbaya, tofauti na Magufuli yeye ni chawa wala hawezi kumubeba sanasana azidi kumuaribia.

Amemgeukia Slaaa, ambae alipokuwa Barozi, huyuhuyu Chawa halikuwa hasemi mabaya ya huyo Slaa. Leo kapingana na baadhi ya maamuzi mabaya ya serikali, kaja na takwimu za Slaa kutokupendwa. Huo utafiti aliufanya lini? Siasa za majungu na kujikomba kwa baadhi ya viongozi kwasasa hazilipi, vijana someni alama za nyakati, mnajidharirisha.
 
Wanaopitia wakati mgumu ni CCM viranja wa kuuza rasilimali za Taifa. Kwa Sasa CCM Wana wakati mgumu, wamekuwa wapole kupisha upepo wa kisurisuri upite, na Kwa taarifa yao upepo huo wa kisurisuri haupiti mpaka ung'oe paa la nyumba yao.
 
Wanaopitia wakati mgumu ni CCM viranja wa kuuza rasilimali za Taifa. Kwa Sasa CCM Wana wakati mgumu, wamekuwa wapole kupisha upepo wa kisurisuri upite, na Kwa taarifa yao upepo huo wa kisurisuri haupiti mpaka ung'oe paa la nyumba yao.
CCM Bado ipo imara sana na hakuna chama cha Kuitetemesha hata kidogo.
 
Slaa ana hoja za msingi kila anapopita,tatizo ni kwamba hoja zake zimemfikia nani?au zinamhusu nani? Kiufupi slaa yuko mbele ya muda katika nchi yenye wasomi wajinga 99%. ..kila hoja iliyomharibia slaa hakika ilikuwa hoja ya msingi ila "hoja bora kwa hadhira jinga".....binafsi natilia shaka hata wewe mtoa uzi uwezo wako wa kureason .
 
Nina uhakika asilimia 100% haujawahi kuwa hata monitor wa chekechea na kamwe hatutakuja kuwa kiongozi. Pdf utazisoma tu, idara ya vetting iko vizuri. Unafiki ulionao ukizeeka lazima uwe mlozi🤣🤣🤣🤣
 
Mwandishi alieleza vizuri lakini mwisho ukaonesha rangi yake. Pamoja na hayo matusi si mazuri tujaribu kuyaepa
 
Duh!! Yaani
Duh! Yaani inaelekea unamfaham saana Slaa. Hayo yote uloandika kuh. yy na jinsi unavof
Inaelkea unamfaham kw xana. La kujiuliza, kakukosea nin! Sjawahi ona mtu anafrahia shda z binadam mwenzake kama nlivokusoma. Kakukosea nn! Na inaelkea unamwombea mabaya yamkute! Kna nn baina yenu unaingia kwny vichwa vya watu mblmbl na kusoma wanavofikiri! Ama kweli we ni mtaalam...duh!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…