Dkt. Slaa amesahau Katiba au anapotosha makusudi?

Dkt. Slaa amesahau Katiba au anapotosha makusudi?

Haki sawa

JF-Expert Member
Joined
Oct 3, 2007
Posts
4,781
Reaction score
3,210
Leo mtandao wa Mwanahalisi umemnukuu Dr. Wilbroad Peter Silaa akisema kwamba wananchi wanaosema kuwa 'Mbowe sio Gaidi' wanamkera Sana kwani hawapaswi kusema hivyo Ila waiachie Mahakama!

Hakusoma lolote kuhusu wale wananchi wengine ambao wao Kutwa kucha wanasema Kinyume chake yaani wanasema kuwa 'Mbowe NI Gaidi' .... hakutaka kuwakemea hao Bali anakemea kundi linalosema Kinyume na Hilo.

Mwambieni Dr Slaa akasome Katiba ya nchi, ibara 13 (6), (b) inayopiga MARUFUKU mtu anayeshtakiwa kutenda 'KOSA' fulani kuhesabika kuwa ana HATIA mpaka pale mahakama itakapotamka. Wananchi HAWAKOSEI wanaposema #MboweSioGaidi na si kuingilia UHURU wa mahakama kama yeye anavyodhani!

Yeye na wenzake ambao wanaona kuwa 'Mbowe NI Gaidi' ndio wanaingilia Uhuru wa Mahakama! Waiachie Mahakama kwani Katiba yetu imeweka wazi na bayana kuhusu MTU kutuhumiwa Kwa kosa Fulani sio kwamba amelitenda kosa Hilo na anahesabiwa Hana Hatia mpaka itakapothibitika Mahakamani.

Dr. Slaa tusimchukulie kuwa ameropokwa la hasha! Huyu amekuja kupima kina cha maji, ametumwa kuandaa UMMA Kisaikolojia, anapima kauli yake itapokelewa vipi na UMMA, anajaribu kuonyesha upande wa mashitaka wanayo hukumu ya Aina gani kabla hata ya kusikiliza utetezi wanajitetea vipi na Kwa ushahidi gani.

Wengine wanafikiria kuwa Dr. Slaa ana msongo wa mawazo kutokana na Mambo ambayo anayapitia sasa kwenye Maisha yake! Huenda ikawa kweli lakini Kwa jinsi nilivyomsikiliza na kumtazama unaona kabisa dimina yake inakuonyesha amamaanisha kitu gani! Asipuizwe Kwa alichokifanya kwani anajua anafanya nini na Kwa malengo gani!

Kuna siku ntakuja kumfunua alivyo, na matendo yake maovu ya Muda mrefu, hamtaamini kuwa huyu ni Yule Dr. Slaa au NI MTU Mwingine anafananishwa Naye kwani sio msafi kama mnavyomfikiria!

Sio muaminifu kwenye ndoa, pesa, kiapo na Pia sio muaminifu Kwa watu wake anaowaongoza au anaofanya nao KAZI!
 
Huyu mzee ni kichefuchefu na kifaduro tupu, anasema mahakama iachwe iamue na hapo hapo ana imply vinginevyo ni jambo la ajabu sana, watu wa namna hii sijui ni kwa nini wasiitwe mbele za haki. Mungu ni wa wakosaji na kama Slaa ni mkamilifu wa kuwashambuliwa watotoa maoni, basi na yeye huko juu, dishi limeyumba.
 
Si tunaambiwa kwamba Mbowe ndiye aliyemjengea nyumba Slaa hadi akamkabidhi funguo zake. Wanasema fadhila mpe mbuzi kwa binadamu atakupa maudhi.

Slaa ni bogus, ajishughulishe na mambo yake aachane na mambo ya Mbowe, yeye aongelee tu mambo ya huko ccm walikofikiana bei.
 
Akibanwa na mavi ndio huongea ujinga ujinga. Yaani mtu aseme Mbowe sio gaidi yeye anakasirika ebo... so anataka watu waseme Mbowe ni gaidi? upumbavu wake ampelekee Josephine. Hao waliomshitaki Mbowe ndio awakasirikie. Mwambieni afikirie kabla hajaongea.
 
Mbona naona wewe ndio unamwekea maneno mdomoni.... mahaba yako kwa Mbowe yamekupofusha... ikiwa si gaidi au ni gaidi tuiache mahakama itoe uamuzi wake hilo ndio muhimu kwa sasa. Kubali kutokukubaliana itakupungizia stress.
Yaani niwe na stress kwamba Babu Slaa ambaye amepoteza mwelekeo na anajisemea vya moyoni na sio vya akilini?

Ogopa Sana MTU anaongozwa kufanya uamuzi Kwa kutii moyo na tumbo badala ya akili!

Slaa ana stress za kumtosha .......
 
Mbona naona wewe ndio unamwekea maneno mdomoni.... mahaba yako kwa Mbowe yamekupofusha... ikiwa si gaidi au ni gaidi tuiache mahakama itoe uamuzi wake hilo ndio muhimu kwa sasa. Kubali kutokukubaliana itakupungizia stress.

Mahakama ipi labda, hizo zinazochukua wazi wazi maagizo ya Muhimili uliojichimbia chini? Au mnadhani hatujui udhaifu wa hiyo mahakama?
 
Hakusoma lolote kuhusu wale wananchi wengine ambao wao Kutwa kucha wanasema Kinyume chake yaani wanasema kuwa 'Mbowe ni Gaidi' ....hakutaka kuwakemea hao Bali anakemea kundi linalosema Kinyume na Hilo.
 
Mwambieni Dr Slaa akasome Katiba ya nchi, ibara 13(6)(b) inayopiga MARUFUKU mtu anayeshtakiwa kutenda 'KOSA' fulani kuhesabika kuwa ana HATIA mpaka pale mahakama itakapotamka. Wananchi HAWAKOSEI wanaposema #MboweSioGaidi na si kuingilia UHURU wa mahakama kama yeye anavyodhani
 
Yeye na wenzake ambao wanaona kuwa 'Mbowe NI Gaidi' ndio wanaingilia Uhuru wa Mahakama! Waiachie Mahakama kwani Katiba yetu imeweka wazi na bayana kuhusu MTU kutuhumiwa Kwa kosa Fulani sio kwamba amelitenda kosa Hilo na anahesabiwa Hana Hatia mpaka itakapothibitika Mahakamani.
 
Kuna siku ntakuja kumfunua alivyo, na matendo yake maovu ya Muda mrefu, hamtaamini kuwa huyu ni Yule Dr.Slaa au NI MTU Mwingine anafananishwa Naye kwani sio msafi kama mnavyomfikiria!

Sio muaminifu kwenye ndoa, pesa, kiapo,na Pia sio muaminifu Kwa watu wake anaowaongoza au anaofanya nao KAZI!
 
Yeye na wenzake ambao wanaona kuwa 'Mbowe NI Gaidi' ndio wanaingilia Uhuru wa Mahakama! Waiachie Mahakama kwani Katiba yetu imeweka wazi na bayana kuhusu MTU kutuhumiwa Kwa kosa Fulani sio kwamba amelitenda kosa Hilo na anahesabiwa Hana Hatia mpaka itakapothibitika Mahakamani.
Hakuna majibu hapo
 
Mbona naona wewe ndio unamwekea maneno mdomoni, mahaba yako kwa Mbowe yamekupofusha, ikiwa si gaidi au ni gaidi tuiache mahakama itoe uamuzi wake hilo ndio muhimu kwa sasa. Kubali kutokukubaliana itakupungizia stress.
Mbona Sirro kila mara anasema Mbowe ni gaidi?Kwa nn yy hajaichia mahakama ifanye kazi yake?Hili Dr Slaa hajaliona kaona la wanaosema Mbowe sio gaidi?Nikujuze tu kua Mungu hakosei.Ashaona hiyo shida haifai ktk kumtumikia ndio maana akaamua kumuacha akapambane na lile shangingi ili adhihirishe ukuu wake.Ona sasa mzee wa watu hana mke,hana mshahara,nyumba karudi aliyojengewa na CHADEMA na hata CCM haimtaki.Mwisho wa siku atajinyonga kwa stress.
 
Huyu mzee mwacheni tu apumzike! Anaweza kutokwa neno lolote kwa maana yeye ana uadui na CHADEMA hivyo kwa kila hali anataka kuona anguko la chama hicho ambacho kilimhifadhi alipokimbia kutoka CCM, lakini akaona bora arejee alikotoka ambako baada ya kumtumia tena wamemtosa huku "mkewe" na yule "shemeji" yake nao wakiwa hawako upande wake tena!!! Sasa hajui ashike wapi...
Kweli dunia haina urafiki!!
 
Back
Top Bottom