POTOSHI Dkt. Slaa amesema Falsafa ya CHADEMA hairuhusu chama kushika dola, inafanya kuwa wahaini

POTOSHI Dkt. Slaa amesema Falsafa ya CHADEMA hairuhusu chama kushika dola, inafanya kuwa wahaini

Uhalisia wa taarifa hii umepindishwa ili kupotosha
Source #1
View Source #1

1758116155899.png
 
Tunachokijua
Dkt. Wilbroad Slaa mwanasiasa mkongwe ambaye pia amewahi kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Septemba 14, 2025 alizungumza na vijana wa chama hicho kwa njia ya mtandao ambapo pia yalirushwa matangazo mbashara kupitia YouTube ya Jambo TV.

Madai

Kumekuwepo na kipande cha video kinachosambazwa mtandaoni kikimuonesha Dkt. Slaa akisema na kuambatanishwa kichwa cha habari kinachosema 'Falsafa ya CHADEMA hairuhusu chama kushika dola, inafanya kuwa wahaini'

Uhalisia

Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia utafutaji wa maneno muhimu (key words search) pamoja na marejeo ya video umejiridhisha kuwa video hiyo imepotoshwa uhalisia wake kwa kukata na kuunganisha vipande vya video visivyohusiana na kutengeneza ujumbe usiokamilika hatimaye kupotosha uhalisia.

Vilevile kichwa cha habari kilichoambatanishwa kwenye video hiyo kinapotosha uhalisia kwani kimeongezewa maneno ambayo hayakutamkwa na Dkt. Slaa. Rejea video halisi hapa na hapa.

Katika video halisi Dkt. Slaa aliwasisitiza vijana wa chama hicho kuacha uoga na kutekeleza majukumu yao kulingana na falsafa ya chama hicho na kuongeza kuwa kama yale yaliyopo katika katiba ya chama hicho hayatekelezwi basi endapo chama kikishika dola pia hawataweza kutekeleza wajibu wao.


View: https://www.youtube.com/live/r2bFo146ZRo?si=3RHZRlW8Da80oGn7&t=2062
​
Back
Top Bottom