Dkt. Wilbroad Slaa mwanasiasa mkongwe ambaye pia amewahi kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Septemba 16, 2025 alifanya mahojiano na Televisheni ya mtandaoni
Jambo TV na mtangazaji wake Wilberforce Ngoto yaliyorushwa mbashara kupitia mtandao wa YouTube.
Mnamo mwezi Januari 21, 2025 CHADEMA walifanya
Uchaguzi mkuu ulioanzisha utawala mpya wa Tundu Lissu ambaye alichaguliwa kuwa mwenyekiti akimshinda mshindani wake mkuu Freeman Mbowe aliyekuwa akishikilia kiti hicho.
Januari 22, 2025 Tundu Lissu akiwa kwenye Mkutano wa Baraza Kuu la Chama katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam,
alimteua Katibu Mkuu, Manaibu Katibu Wakuu pamoja na wajumbe wa Kamati Kuu na kuthibitishwa na baraza kuu la chama hicho.
Mwezi Mei 13, 2025 Ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa
ilitengua uteuzi wa wajumbe 8 wa sekretarieti na kamati kuu ya CHADEMA walioteuliwa na Tundu Lissu baaya mmoja ya mwanachama kumuandikia barua msajili akiitaka Ofisi hiyo, kubatilisha viongozi wote waliopitishwa kinyume cha katiba ya chama hicho pamoja na uamuzi uliofanyika Januari 22, 2025.
Madai
Kutoka na mahojiano ya Jambo TV, kipo kipande kidogo cha video kinachosambazwa mtandaoni kikimuonesha Dkt. Slaa na kueleza kuwa amethibitisha kuwa CHADEMA haikufanya uchaguzi huru na haki.
Uhalisia kwa kipande hicho cha video
Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia utafutaji wa maneno muhimu (key words search) pamoja na marejeo ya video umejiridhisha kuwa video hiyo imepotoshwa uhalisia wake kwa kukata na kuunganisha vipande vya video visivyohusiana na kutengeneza ujumbe usiokamilika hatimaye kupotosha uhalisia.
Katika
video halisi Dkt. Slaa alikosoa waliosema uchaguzi wa CHADEMA haukuwa halali, pia alisisitiza uhalali wa viongozi walioteuliwa na Tundu Lissu na kuthibitishwa na baraza kuu la chama hicho akibainisha kuwa taratibu zilifuatwa.
"Kwa uchaguzi ule uliokuwa live, Sisti Nyahoza alikuwepo bado kuna uhalali wowote wa kusema kwamba uchaguzi ule haukuwa halali kiasi kwamba msajili anaenda kuwakataa watu waliochaguliwa halali? Dunia nzima iliuona Sisti alikuwepo ndani lakini anasema kina Mnyika hawakuchaguliwa kihalali kwa sababu amepokea barua ya mtu mmoja. Msajili Francis Mutungi na Nyahoza wanashindwa kusoma kiasi cha kuelewa, kuna tofauti katika katiba ya CHADEMA, kati ya uchaguzi na uthibitisho.
Mimi nilikuwa gerezani, nilisikiliza live Mnyika alisimama hadharani akahesabu kolam ya watu waliokuwepo, akasema katika hatua hii hatufanyi uchaguzi, tunafanya uthibitisho wa walioteuliwa na Mwenyekiti, kazi yake baraza kuu ni kuwathibitisha, na katiba inasema asilimia ya kolam ni 50% na katika uchaguzi kolam ni 75% hii hata mtoto wa darasa la nne hawezi kuelewa? sembuse msajili, sasa huwezi kuona kwamba hapa kuna mkono wadola?"
View: https://www.youtube.com/live/VefpxrjL6JI?si=tYQQR8F6XlGYzJ8K&t=1472