Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Dr. Slaa ambaye aliteuliwa na Dr. Magufuli kuwa Balozi na ambaye sasa amestaafu, amejitokeza hadharani kuipinga kamati ya haki Jinai huku akiitupia lawama serikali kwamba inawacheza shere wananchi .
Amedai kwamba kuleta Tume ya Haki Jinai katikati ya Mjadala wa Katiba mpya ni mbinu ya kupoteza muda, kwa sababu yote yanayojadiliwa kwenye Tume ya Haki Jinai ni lazima yawemo kwenye Katiba Mpya , sasa badala ya kujaza Matume yote haya kwanini jambo hili lisingeingizwa tu kwenye Katiba mpya?