Natamani sana zingekuwepo alama za "nzuri" zaidi ya moja, zote ningezimwaga hapa!Kuna msemo wa kiswahili kwamba " Mchawi mpe mwanao akulelee " siyo kwamba sisi hatuoni "delay tactic" ya Samia , bali hatuoni namna atakavyokwepa mitego ya katiba mpya .
Ni hivi , Samia amezungukwa na watu wasiotaka mabadiliko akiwemo Mizengo Pinda , labda kwa kufichua ni hivi , Pinda si kiongozi tu wa chama na serikali , huyu ndio link ya kitengo ndani ya serikali , yeye na wengine (sitawataja kwa sasa) , ndio wanaoamua mambo mengi sana ya nchi , usione analima mananasi ukamchukukia poa .
Sasa juzi Mama kamteua awe mshauri wake kwenye kilimo , hii maana yake ni kumuengua kwenye kikosi kazi , sijui kama unanielewa , hata Bi Mkubwa si kwamba anaitaka Katiba mpya bali kuna shinikizo kubwa kutoka kwa watoa hela , na kimsingi yeye kama yeye hana ujanja , bali hawa wahafidhina ambao hawajali shida za nchi , wao kwao hata wananchi wakiteseka ili mradi ccm ikiwa madarakani kwao haina shida .
Sisi mchezo wote tunaujua (Kumbuka kwamba Lissu alikuwa nje kwa matibabu , lakini pia bado alikuwa Kiongozi wa Chadema na alifanya kazi za chama , sitaingia kwa undani )
bali kuwepo kwa Lissu Ubelgiji ulikuwa mkakati wa chama chake , angeweza hata kutibiwa USA , Bali aliminya ubelgiji (ifuatilie kwa makini ubelgiji)
Kwa kifupi ni kwamba Chadema siyo Mabwege .
Heshima sana mkuu 'Erythro' kwa andiko hili hapa linalopiga penyewe hasa!
Lakini,...
Ninakutahadharisha sana kuhusu hili.Kwa kifupi ni kwamba Chadema siyo Mabwege .
CHADEMA shaondolewa kwenye reli sana. Kuinyanyua na kuipandisha tena kwenye reli ianze tena ilipokuwa imeishia na moto ule uliokuwepo na hadi ifanye kweli, kama "Hichilema wa Zambia...", hiyo itakuwa ni kazi ngumu sana, hata kufikia kuwa haitawezekana kwa muda huu uliobaki.
Mtavurugwa sana ndani ya chama chenu wakati huu hata msione mnakwenda wapi.
Kama ni "mkakati" kama unavyoeleza, basi mkakati huu utawageukia nyinyi wenyewe.