Dkt. Slaa: Freeman Mbowe aachane na Maridhiano maana hayafai, Katiba sio mali yake binafsi au mali ya Rais Samia

Dkt. Slaa: Freeman Mbowe aachane na Maridhiano maana hayafai, Katiba sio mali yake binafsi au mali ya Rais Samia

Kwahiyo Mbowe angekufa na CDM ingekufa? Ukiona uhai wa taasisi unategemea mtu fulani ili iendelee kuwepo, kama ni kweli CDM inamtegemea Mbowe ili iendelee kuwa hai, basi ujue hakuna taasisi hapo.

Na kwa taarifa yako nyie ndio mnaochangia hiyo CDM kuonekana ni chama cha mtu, au kikabila kwa utetezi huu. Hata wapambe wa Nyerere walikuwa wanamdanganya kuwa bila yeye kuwa rais, Tanzania haiwezi kuwepo. Leo hii Nyerere hayuko madarakani wala hai, je Tanzania imepotea? Nakushauri, pigania taasisi na sio mtu. Inshort muda wa Mbowe kuendelea kuwa mwenyekiti wa CDM umepita.
Tindo ifikie mahali uwaheshimu wale wanaotaka uwepo wa Mbowe CDM kama mwenyekiti. Hayo ya sijui akifa, situation itadictate. Chadema ilimuhitaji Mbowe hasa kipindi cha awamu ya Tano.
 
Huyu ndio mwanasiasa bora kuwahi kutokea TZ.
Dr Slaa anamisimamo isiyoyumba wala kuyumbishwa. Tumemiss aina ya siasa za huyu mzee.
Kaondoka CDM na chama kimekufa.
Chama kimekufa lakini kila siku watu wanaongelea CDM wakati kuna vyama vingine vingi tu na vipo hai
 
Tindo ifikie mahali uwaheshimu wale wanaotaka uwepo wa Mbowe CDM kama mwenyekiti. Hayo ya sijui akifa, situation itadictate. Chadema ilimuhitaji Mbowe hasa kipindi cha awamu ya Tano.

Sina tatizo na nyie mnaotaka Mbowe kuendelea kuwa mwenyekiti wa CDM, hata mkitaka afie madarakani huo ni utashi wenu. Ila kwangu mimi ni mwiko kiongozi wa kuchaguliwa kukaa nafasi moja zaidi ya miaka 10. Hata hivyo mada hii sio uhalali wa Mbowe kuendelea kuwa mwenyekiti wa CDM, bali upatikanaji wa katiba mpya. Hebu tujikite humo kuliko nafasi ya Mbowe kama mwenyekiti maana tutatoka nje ya mada.
 
Moja ya wanasiasa wanaoiishi na kuisimamia itikadi yao....na kile wanachokiamini....

Pamoja na kwamba ni ngumu kukataa teuzi toka Kwa mkuu wa nchi ...

Linapokuja swala la kuweka wazi kile anachokiamini...huyu mtu Huwa ni straight forward...hamung'unyi maneno
 
Huyu mzee akae kimya, yaliyotokea awamu ya 5 yalisababishwa na yeye la sivyo tungekuwa na awamu nzuri yenye kuwafanya watu kiendelea kupendana nadala yake ilikuwa awamu ya kiwagawa Watanzania kwa Imani, Ukanda, Makabila nk.
The https://jamii.app/JFUserGuide?!
 
Agenda ya KATIBA mpya ni ya wananchi.

Si agenda ya CCM na CDM pekee.
Sikatai ulichoandika, lkn kwanini asilizungumze hili mwenyewe kwa kutoa maoni yake bila kuishirikisha serikali na Mbowe?
 
Akihojiwa na East Africa Radio asubuhi hii Aprili 20, 2023, Dkt Slaa amesema akipata nafasi ya kukutana na mwenyekiti wa CHADEMA Mhe. Freeman Mbowe atamshauri aachane na maridhiano kwa kuwa hayafai.


“Nikipata nafasi ya kukutana nitamwambia kwamba fuata principle za siasa safi, simamia, kwa sababu kwa sasa unatakiwa kuwapatia watanzania katiba mpya. Maridhiano hayafai” amesema

Amesisitiza, “Maridhiano hayafai kwasababu yanakaa zaidi ya mwaka, hakuna taarifa kwa wananchi. Maridhiano si mali ya Samia na ya Mbowe. Katiba inayodaiwa ni ya watanzania. Katiba si mali ya watu wawili, wala sio ya CCM na CHADEMA, ni ya watanzania. Watanzania lazima wajue wanataka katiba ya aina gani”
Dkt Slaa amesema amemsikia mara kadhaa Rais Samia akisema kuwa wataangalia katiba ya mwaka 1977 kwa kuwa Rasimu ya Warioba imepitwa na wakati, yeye anasema haya ni makosa makubwa sana.

“Someni preamble pale kwenye katiba mwanzoni imeandikwa nini, imeandikwa sisi watanzania tumeamua, kwenye katiba”

Kuhusu kusubiria uteuzi, amesema kwa umri wake hasubirii tena fursa hiyo, pia amemsfia Freeman Mbowe kuwa mwanasiasa mzuri, mkonge na mpambanaji wa siku nyingi.


Chanzo: East Africa Radio
Ni wazo zuri
 
Wewe unayeelewa ni msomi gani aliyejitokeza kwenye swala la muundo wa nchi,maendeleo ya nchi bila kuwa mwanasiasa?
Zaidi ya robo tatu ya watanzania ni wanasiasa, hakuna anaye kataaa. Shida Iko hivi chama kisiwe ndichokitafute katiba ya wananchi hatakama kinamaprofesa wa katiba. Anayetaka katiba asitumie mgongo wa chama chake Cha kisiasa. Kama anataka katiba aachane kutumia chama chake Cha kisiasa aonekane kama mwananchi wakawaidaa hata kama anachama chake pendwaa.

Mfano CCM waseme wanataka katiba mpya ya wananchi, kitakachojengeka Kwa watu wataaanzakisema labda CCM wanamasilahi Yao ya kichama, vivyo hivyo na chadema au achama chochote Cha kisiasa, hivyo, ili tupate katiba nzuriii wananchi pamoja na vyama vyao, wasimame neutral pasipo na mlengo wa kisiasa ya chama flaniii. Kwani katiba ni Sheria mama itakayooongoza vyama vyote na wananchi wenye vyama na wasio na vyamaaa.

Ndio maana ata akina walioba hawakusimama na kusema sisi wanachama chetu ndio tunaotafuta katiba, lakini pamoja na uanachama wao wa vyama vyao waliweka pembeni wakisimama neutral kuleta rasimu ya katiba ya wananchi.
 
Chama kimekufa lakini kila siku watu wanaongelea CDM wakati kuna vyama vingine vingi tu na vipo hai
Chama gani kingine kilicho hai?
Kwasasa TZ hakuna chama kilicho hai.
 
Sikatai ulichoandika, lkn kwanini asilizungumze hili mwenyewe kwa kutoa maoni yake bila kuishirikisha serikali na Mbowe?
Anayoyaongea Dr Slaa Leo hata sisi humu jamvini tumeyaongelea sana.

Terms za maridhiano hazipasi kuwa Siri kama hili ni suala linalogusa maslah mapana ya nchi.

Terms hizo za maridhiano zingekuwa wazi, AGENDA ya kushughulika UGUMU wa MAISHA ni mfumuko wa Bei za domestic goods ingekuwa namba moja,

BAADAYE ndo yabgefuata masuala ya kugawana vibuyi vya asali na kugawana madaraka😠😠😠

Slaa anabeba HOJA yenye maslah ya wengi.

Abarikiwe.
 
Huna uelewa wowote Kaa kimyaa, kwani wasomi wote ni viongozi wa vya ma vya siasa? Hata ikitokea ivooo, unafikiri washiriki wa katiba ni hao walim na machinga wote kwani nao ni sehem ya wananchi, katiba ya wananchi ni zao na takwa la Kila raia na kuheshim mawazo ya Kila raia mwenye akili timamu, sio wanasiasa na vyama vyao. Au katiba isitokane na takwa la kikundi chochote Cha kisiasa, tukumbuke katiba ni ni Sheria mama Kwa raia wote na Kwa vyama vyao
Mbona rasimu ya Katiba ya Warioba ilitokana na maoni ya kada karibu zote za wananchi lakini hamuitaki?!!!

Tatizo ni chama tawala. Kimeteka Katiba ya wananchi na kuifanya mali yake kwa maslahi yake binafsi!!!
 
Mtanzania wa kawaida anapata faida gani kwenye haya maridhiano ambayo wala hayasongi mbele?
CCM inaweza kweli kuleta katiba ambayo itaiondoa madarakani bila pressure ya wananchi bali pressure ya Mbowe?
Yaani CCM ikupe Tume huru ambayo itawatangaza wameshindwa kwa pressure tu ya Lissu bila wananchi kuamua?

Mbowe na other elites CDM wanajidanganya sana,CCM haitakupa katiba mpya wwla tume huru ya uchaguzi,wana nunua muda tu ifike 2025
 
Yy harakati zake zimeishia wapi...mbona anapakazia wenzake, anaona amekula hela za embassy zimeisha anarudi kuangalia alipotokea, ajiulize alitokatokaje
 
Sina tatizo na nyie mnaotaka Mbowe kuendelea kuwa mwenyekiti wa CDM, hata mkitaka afie madarakani huo ni utashi wenu. Ila kwangu mimi ni mwiko kiongozi wa kuchaguliwa kukaa nafasi moja zaidi ya miaka 10. Hata hivyo mada hii sio uhalali wa Mbowe kuendelea kuwa mwenyekiti wa CDM, bali upatikanaji wa katiba mpya. Hebu tujikite humo kuliko nafasi ya Mbowe kama mwenyekiti maana tutatoka nje ya mada.
Nashukuru umegundua kuw si vizuri kuchomekachomeka kuhusu uenyekiti wake hata ktk mada zisizohusika.
 
econonist zitto junior JokaKuu Tindo idawa MTAZAMO Pascal Mayalla ...nadhani ni wakati muafaka wa Chadema kumrudisha kundini Mzee Slaa asaidie kudai katiba kwa niaba ya Cdm na raia maana Mbowe hamna imani naye.

..vyama au wanaharakati walioko nje ya maridhiano hawajazuiwa kudai Katiba.

..pia sio sahihi kwa Dr.Slaa na wengine wasio Chadema au Ccm kusubiria maridhiano.

..Vyama tofauti na Chadema na Ccm viende kwa wananchi vikauze sera na mikakati yao ya kujenga Tanzania.
 
Tindo ifikie mahali uwaheshimu wale wanaotaka uwepo wa Mbowe CDM kama mwenyekiti. Hayo ya sijui akifa, situation itadictate. Chadema ilimuhitaji Mbowe hasa kipindi cha awamu ya Tano.
Nakazia ✍️✍️
Ukiacha CDM, vyama vingine vyote vilinunuliwa!
 
Hakuna mtu kamzuia Slaa kutafuta katiba mpya, Kama Mbowe anatafuta na mariziano, yeye atafute ya ugomvi, hakuna kupangiana, kila mtu na department yake.
Huyu mzee ni snitch tu.
Badala amwandame Rais mwenye mamlaka anamshushua Mbowe, sasa mbowe kazuia vip wananchi akiwemo huyo slaa kudai katiba mpya? Yeye slaa katoa mchango gani kwenye kupatikana katiba mpya? Kwa sababu ya kupigania utawala bora, ikiwemo katiba mpya, Mbowe kafungwa mpaka gerezani, mali zake zimeharibiwa na serikali ya ccm(akiwemo mshiriki balozi Slaa), sasa slaa anataka mbowe afanyeje labda ndo ajue kuwa anapigania katiba?!!!!!! Anataka mpaka afe?!!
Wewe mzee slaa acha usnitch, toa mchango wako, hamasisha wananchi wadai katiba mpya, ongoza maandamano na wewe balozi mstaafu, achana na Mpiganaji Mbowe, yule siyo saizi yako, yule yupo viwango vingine kabisa katika kuwapigania wananchi na ni mtu mwenye misimamo isiyoyumba, siyo kama wewe slaa kesho ukipewa uteuzi lugha inabadilika unarudi upande wa waonevu
 
Back
Top Bottom