Hakuna anayeipenda CCM, hivyo watu walimpenda kikwete sio CCM. Halafu unasema kikwete alishuka umaarufu?. Kikwete aliruhusu maoni, maandamano na mikutano na bunge live kwa hivyo maovu yaliwekwa hadharani na vyama vilipata wasaa wakujijenga ndio maana kura zilipungua mpaka asilimia sittini.
Magufuri alipiga Pini bunge live, mikutano ya siasa, hata mikutano ya ndani kwa miaka mitano na bado aliinfluence Tume. Hivyo Kama angeruhusu vyama viwe huru, maoni yatolewe , bunge liwe live na mauchafu yote yawekwe wazi, hata asimia arobaini asingefikisha.