Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Haya si Maneno yangu, ni Maneno ya Dkt Slaa
MWANASIASA mkongwe na Katibu Mkuu wa zamani wa Chadema, Dk. Wilbroad Slaa amesema mabadiliko ya Baraza la Mawaziri yanayofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan kila mara yamedhihirisha kuwa Serikali haijui inataka nini kwa sababu hata viongozi wanaorejeshwa kwenye baraza hilo na katika nafasi nyingine, hawana manufaa yoyote kwa Taifa zaidi ya kujipanga na uchaguzi ujao.
Akizungumza na MwanaHALISI Online leo Jumatatu ametoa mfano namna aliyekuwa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye alivyoikosesha Tanzania uwekezaji mkubwa wa kiteknolojia kutoka kwa Elon Musk ambaye ni tajiri namba mbili duniani.
“Watanzania tutengeneze mshikamano wetu ambao utalenga kujipanga kwenye uchaguzi unaokuja na kushinikiza upatikanaji wa katiba mpya ili haya yanayotokea leo ya rais kubadilisha watu kama anabadilisha gauni lake, sioni kama yanatusaidia kwani gauni analivaa yeye mwenyewe,” amesema Dk. Slaa.
Chanzo: Mwanahalisi Digital
Pia soma > Uteuzi na Utenguzi: Nape, January na Byabato out! Jerry Silaa ahamishiwa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari