Patriot missile
JF-Expert Member
- Jun 16, 2024
- 280
- 423
Mpeni nafasi agombee urais
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mzee Slaa na wengine humu wanaokosoa wasome hadi kupatikana Putin, Boris Yeltsin aliteua na kutengua mawaziri wakuu wangapi na kwa muda gani hadi akampata Putin. Tuiache mamlaka ya Rais ifanye kazi yake. Inajua kuliko sisi.🙏🙏🙏Haya si Maneno yangu, ni Maneno ya Dkt Slaa
MWANASIASA mkongwe na Katibu Mkuu wa zamani wa Chadema, Dk. Wilbroad Slaa amesema mabadiliko ya Baraza la Mawaziri yanayofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan kila mara yamedhihirisha kuwa Serikali haijui inataka nini kwa sababu hata viongozi wanaorejeshwa kwenye baraza hilo na katika nafasi nyingine, hawana manufaa yoyote kwa Taifa zaidi ya kujipanga na uchaguzi ujao.
Akizungumza na MwanaHALISI Online leo Jumatatu ametoa mfano namna aliyekuwa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye alivyoikosesha Tanzania uwekezaji mkubwa wa kiteknolojia kutoka kwa Elon Musk ambaye ni tajiri namba mbili duniani.
“Watanzania tutengeneze mshikamano wetu ambao utalenga kujipanga kwenye uchaguzi unaokuja na kushinikiza upatikanaji wa katiba mpya ili haya yanayotokea leo ya rais kubadilisha watu kama anabadilisha gauni lake, sioni kama yanatusaidia kwani gauni analivaa yeye mwenyewe,” amesema Dk. Slaa.
Chanzo: Mwanahalisi Digital
Pia soma > Uteuzi na Utenguzi: Nape, January na Byabato out! Jerry Silaa ahamishiwa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari
Mmmmmmhkwani yeye aliefukuzwa upadre na alikua anabadilisha vyama vya siasa na wanawake alikua anawabadili kama gauni au soksi?🐒
kwanza yeye yupo chama gani saivi kama sio tamaa tu zimemjaa hajui hata ajiunge chama gani kote anataka awepo 🐒
Kama nyumba yako inavuja hata ukipanguwa vipi furniture, bado iatavuja tu.Haya si Maneno yangu, ni Maneno ya Dkt Slaa