Pre GE2025 Dkt. Slaa: Minyukano ya kambi za uchaguzi wa Mwenyekiti (Mbowe & Lissu) CHADEMA, sababu ni Mbowe anataka kugombea Urais 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Ukisikia kumechangamka ndo hii sasa.
Slaa hamkubaligi Mbowe since ahame.
 
Slaa alisema amejiuzulu siasa hajatoa taarifa kama hivi sasa ni mganga wa ramli!
 
Reactions: Tui
Kumbe Mbowe ni msaliti anaitumia chadema kama chimbo la ukwasi
 
Uongo mtupu mnajihami baada ya kuona Tundu anaenda kupotezwa katika ra.mani za kisiasa.
Mimi ni mchunguzi wa matukio, kuyachambua na kutoa maoni yangu tu ndugu. Huna haja ya kununa na kutetemeka...

By the way nimekuwekea mlolongo wa matukio, ya kweli na halisi. Uongo wangu uko wapi? Hayo hayakutokea...?
Ni maoni na mtazamo wako kulingana na ukomo wa ufahamu wako..

Sasa ameamua kupanda juu huko huko aliko boss wako. Acha inyeshe, tuone panapovuja...!
Kuhusu kugombea urais Lissu aelewe hiyo siyo haki yake bali ni favour mtu yeyote anaweza kupewa hiyo fursa akawakilisha chama.
Unasemaje? Ni favour? Nani ampe favour nani..?

Ushauri wangu kwako ni huu..

Hii kauli mwambie Freeman Mbowe maana hili ndilo agano lake na "watesi wetu CCM" kupitia kwa Mama Abdul. Sasa anajaribu kulitekeleza. Lakini unajua nini? HE HAS ALREADY FAILED...!!
Kama anataka sana kugombea urais basi vipo vyama aombe agombee kutoka huko tuone kama atashinda.
CHADEMA ndiyo kwake. Atakuwa mwenyekiti, na ndiye mgombea wetu wa u - Rais 2025 whether you like it or not...!
Hoja yako ya urais ni mufilisi kabisa mtu yeyote timamu anajua CCM hawawezi kuuachia urais uchukuliwe na mtu nje ya CCM na yeyote anayegombea anajua hilo hata Lissu wako analijua hilo.
Akili zako ni za binadamu aliyeumbwa kwa udongo tu. Hawazi ama kufikiri zaidi kisogo chake kinapoishia..!

Pole sana kwa ufinyu wa fikra zako...
Faida pekee ya kugombea urais ni chama kupata ruzuku kubwa na wabunge wa viti maalum wengi kutokana na zile kura za urais atakazopata mgombea.
Historia ya dunia bila shaka inakupiga chenga. Unachoangalia wewe ni leo nimekula na kwenda choo, basi...

Utashangaa na kupigwa bumbuwazi pale utakapojua kuwa kumbe MUNGU SIO RMC...!!
Lissu anajifuta mwenyewe katika siasa kwa kutengeneza uadui na viongozi wenzake ndani ya CHADEMA na option pekee iliyo salama akaanzishe chama chake atoke jasho kukijenga na itamchukua miaka na pengine asifanikiwe sana maana hana fedha .
You are too low my friend..

Fedha? Fedha za kuendesha taasisi kama hii (chama cha siasa) ziko kwetu wapenzi, wafuasi na wanachama..

Hii kauli unaitoa ktk ground ipi hasa? Kwamba CHADEMA hakina wapenzi, mashabiki na wanachama wenye fedha?

Kama unafikiri hivi, basi akili na ufahamu wako ktk mambo haya uko chini ya wastani, unahitaji kubustiwa..
Akijiunga na hivi vyama vilivyopo atapata fursa ya kugombea urais tu lakini cheo hawatampacna baada ya uchaguzi watamtosa.

Lissu amelikoroga mwenyewe.
Mawazo ni mwanafunzi wa kidato cha pili haya..

Pole, karibu tena kwa maoni yako...

Hapa chini ni link ya YouTube. Msikilize Dr Slaa kwa umakini hasa kuanzia dakika ya 34

View: https://youtu.be/XTlnmsgZPRk?si=QISH6D5yf6AeGhZ6
 
Mleta mada Umeandika kirefu tuhuma bila chembe ya ushahidi hakikika hata mmoja

Umejaza umbeya wa uswahilini mwanzo hadi mwisho
Hayo matukio yote hayakutukia?

Sasa unataka ushahidi upi?

Freeman Mbowe hakufanya Interview na Salim Kikeke?

Hakusema naye alishangaa makamu wake kum - challenge kwenye uenyekiti wake?

Au unataka ushahidi wa kilichosemwa na Dr Slaa?

Ok. Fungua link hii👇🏻 ya YouTube kisha specifically, msikilize kuanzia dakika ya 34 na kuendelea

View: https://youtu.be/XTlnmsgZPRk?si=QISH6D5yf6AeGhZ6
 
Yeye ni mwanachama wa chama gani?
Chama kinaitwa Tanganyika au sema Tanzania...

Ni mwananchi na raia wa Tanganyika...

Swali la kichokozi:

Hivi tarehe 9 ya mwezi desemba kila mwaka huwa ni sherehe ya kumbukumbu ya uhuru wa nchi fulani. Unaweza kuniambia jina la nchi hiyo?
 
Kwa agano ambalo Freeman Mbowe ameingia na Mama Abdul/CCM, definitely, amedanganywa na shetani kuwa atapata wabunge wengi...

Hii ndiyo inayoleta shida ndani ya CHADEMA sasa. Freeman Mbowe kuingizwa mkenge kirahisi na ma - CCM...

Wenzake wamemchoka na sasa wanamwambia kwa macho makavu kabisa kuwa, NO WAY....!
Very funny, looh...!

Wewe umeelewa maudhui ya andiko hili...
Hapa tutatofautiana...

Tundu Lissu is not a liability. He's always a valuable asset...

Kwa mfumo wa kisheria na kikatiba unaosimamia na kuongoza ufanyikaji wa chaguzi zetu, hata ulete asset ya thamani kiasi gani ktk soko la uchaguzi chini ya mfumo huu, itaibiwa tu na wakora wa CCM..

2020 Tundu Lissu huyu huyu alimpiga John P. Magufuli kwa kura halisi zaidi ya 75% lakini majambazi yaliiba...!

That's why, we say NO REFORMS - NO 2025 GENERAL ELECTION ...
 
Mleta mada mjinga fulani hivi kaweka Dr Slaa ili kuvuta attention watu wasome lakini alichoandika upumbavu mtupu na
Una hasira sana eti eeh...?

Mimi ni mjumbe tu ndugu. Tunaleta, kuchambua na kujadili yaliyopo ndani ya jamii sasa..

Mimi sio mpumbavu. Mpumbavu ni yule asiyetaka kuhoji, kuchambua na kutaka kujua kila tukio lina maana gani na kile kilicho nyuma ya kila tukio...!
Kwa hiyo ni kosa kikatiba kuandika barua, au siyo..?

Kwenye ibara au kipengere gani cha katiba au hata kanuni basi..?

Hizi ni pure mawazo na akili za wana CCM wajinga. Na wewe uko huko siyo..?

Ninachoweza kukushauri ni hiki:

Waambie watu wako au wewe mwenyewe wamwekee pingamizi la kuwa "amekosa sifa ya kuwa mgombea" na sababu iwe "aliandika barua badala ya kwenda tu kuchukua fomu ya kuomba kugombea"

Ukifanya hivi, utaona jinsi utakavyo expose ujinga na upumbavu wako..!
Lisu kichwani hamna kitu hata sijui walimpaje hata huo umakamu mwenyekiti mtu asiyejua hata taratibu tu za kugombea uraisi eti ooh nimeandika barua !! Ugombea uraisi unaombwa kwa kuandika barua ? Hopeless kabisa
Aisee..

Kwamba Tundu Lissu hana kitu kichwani mwake...!!!???

Looh, kwa kauli hii, sasa natambua kuwa kumbe nasoma na kujibu maandishi ya mtu confused asiyeweza kutofautisha JEMA na BAYA...

I feel pity for you Mr Shotocan !!
 
Mbona huko kenya kina Musyoka huacha kugombea kwa ajili ya Odinga. Hata RFK Jr aliacha ugombea na kumuunga Trump. Cha msingi ukihakikishiwa maslahi either teuzi serikalini au "ahsante" nzuri basi unaachia.
 
Heeheeee imebidi nicheke tu, kwahiyo unategemea Lissu akishindwa ndio atakufa kisiasa na Huyo Mbowe ndio atakua relevant? Ni hivi Lissu akishindwa, wapiga kura wa upinzani (wengi kuliko wenye kadi za uanachama) wataacha kupiga kura wala kuhudhuria shughuli yoyote ya chadema na tutakua irrelevant kama CUF ya sasa.
 
Kama ulichoandika ni kweli, basi Tundu Antipass Lissu bye bye Chadema, bye bye siasa.
 
Kwamba Lissu alimshinda Magu Kwa 75%?

Wewe ulifanikiwa kuzitofautisha kura fake na kura halali ndani ya Sanduku la kura na kumjua mshindi wa kura halali kati ya Lissu na Magu?
 
Mkaribisheni ACT Wazalendo kama mnamvalue sana Lissu tuone hiyo impact nje ya yale niliyoyasema kumhusu.

Tarehe 21 Jan ni wiki mbili toka sasa subiri ifike tuone. Ninacho foresee ni kuwa baada ya kushindwa mtakuja kulialia humu kuwa Lissu ameporwa ushindi maana kwenu uchaguzi halali ni pale Lissu akishinda tu.

Nchi hii nimekuwa nikisema mara nyingi kuwa wanasiasa wote hawana watu nyuma yao wana mashabiki wa key board tu. Hivyo Lissu akitoka CHADEMA sio mwisho wa wananchi wa nchi hii kupiga kura, kwani huyo Lissu alkiwa CHADEMA je ACT haikupata kurs wakati wa uchaguzi? Kana nyinyi ACT mlipata kura wakati Lissu akiwa CDM vivyo hivyo CDM itapata kura hata baada ya Lissu kuondoka.

Kuhusu kushinda uchaguzi mimi binafsi najua fika sio CDM wala ACT Wala chama chochote kinaweza kushinda uchaguzi hapa Tanzania, kwa sababu CCM wameishaamua hawataki ushindani ila wanagawa nafasi kidogo jinsi wanavyotaka kwa vyama vingine. Hata huyo Zitto wako anajua mfano uchaguzi ukiwa wa haki CCM haiwezi kupata kiti hata kimoja Pemba na kama kushindana watashindana Unguja sio Pemba ambapo napo wanaweza kugawana nusu kwa nusu na ACT .

Katika mazingira haya ya ubabe wa CCM na unyumbu wa watanzania hakuna mwanasiasa wa upinzani atafanikisha kuiondoa CCM kwa kizazi chetu labda MUNGU aingilie kati.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…