Pre GE2025 Dkt. Slaa: Minyukano ya kambi za uchaguzi wa Mwenyekiti (Mbowe & Lissu) CHADEMA, sababu ni Mbowe anataka kugombea Urais 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kuna uongo kidogo ila ukweli ni mwingi
 
Tarehe 21 Jan ni wiki mbili toka sasa subiri ifike tuone. Ninacho foresee ni kuwa baada ya kushindwa mtakuja kulialia humu kuwa Lissu ameporwa ushindi maana kwenu uchaguzi halali ni pale Lissu akishinda tu.
Nani asiyejua Mbowe ana wajumbe wengi kuliko Lissu? Na ndio maana tunapiga kelele mitandaoni kuwa maoni ya sisi wanachama (ambao wengi tunamuunga Lissu) yaheshimiwe na wajumbe. Sababu akishinda Mbowe chama ndio kinaenda kufa.

Hivi niambie tu Mbowe na Wenje kweli ni sura ya opposition? Kuna kutegemea mabadiliko au upinzani imara? Hakuna mtu makini atawahi pigia kura chadema tena.

Kwahiyo option ni mbili, Lissu ashinde upinzani uamke au Mbowe ashinde chadema ife irrespective ya Lissu kufa kisiasa or not.
 
Katiba ya CDM isifuatwe kwa sababu ni mwiba mchungu kwa Lissu? Hilo haliwezekani na halitafanyika.


Hao wanachama wanaomtaka Lissu ilipigwa kura ya maoni lini na wanachama wote walijulishwa ili washiriki?

Wacha Lissu ashindwe aondoke CHADEMA kama ni asset basi hao wanaomtaka watampigia kura huko huko atakakotimkia sio lazima iwe ndani ya CHADEMA.
 
Reactions: Tui
Hao wanachama wanaomtaka Lissu ilipigwa kura ya maoni lini na wanachama wote walijulishwa ili washiriki?
Kuna kitu kinaitwa survey hata wewe unaweza kufanya tu ukapita mtaani au social media usome upepo unaendaje. Wanachama wengi wanamtaka Lissu kama walivyomtaka 2020 hadi Mbowe akaogopa kurudisha fomu ya kugombea urais. Kule Twitter mpaka mbowe anaogopa kupost chochote kwa hofu ya kukataliwa says a lot.

Sasa kama wao watafumba masikio ya maoni yetu wanachama wakaamua kuhonga hao wajumbe 1200 akashinda kwa kishindo basi ndio wajue chadema inakufa hapo hakuna mtu makini atapigia kura chadema ya wenje na mbowe.

So sad after all the sweat tumeweka, chadema inatufia hivi hivi tunaona sababu ya uroho wa mtu mmoja.
 
Wacha Lissu ashindwe aondoke CHADEMA kama ni asset basi hao wanaomtaka watampigia kura huko huko atakakotimkia sio lazima iwe ndani ya CHADEMA.
Lissu ameshasema hatoondoka coz he has more relevance and longevity than mbowe unless afukuzwe uanachama.

Hivi huyo Mbowe wenu amesema atafanya nini akichaguliwa? Hana hata alichopanga zaidi ya kusema astaafu akiwa na 68 kma mtei!!
 
Andishi refu lakini pumba tupu.
Lusu ni zaidi ya mbowe na ukitaka kulijua hilo leteni kura ya maoni tupige huku mashinani muone jinsi mbowe alivyochokwa na haaminiki tena
 
Huo ndio ukweli, wasijifanye mbuni kuficha kichwa huku kiwiliwili chote kikiwa nje
 
Lissu ameshasema hatoondoka coz he has more relevance and longevity than mbowe unless afukuzwe uanachama.

Hivi huyo Mbowe wenu amesema atafanya nini akichaguliwa? Hana hata alichopanga zaidi ya kusema astaafu akiwa na 68 kma mtei!!
Kiufupi hana agenda yoyote atakayoisimamia akishinda.
Yaani tuchague kiongozi asiye na maono wala agenda ya kukifanyia chama?
 
Mbowe au Lissu hawana sifa kwa sasa kugombea urais kupitia Chadema ila wanashauriwa kwa dhati ya moyo wamteue John Wegesa Heche agombee au yeyote kutokea Dodoma, Singida au Manyara watakuja kushukuru
 
Mbowe au Lissu hawana sifa kwa sasa kugombea urais kupitia Chadema ila wanashauriwa kwa dhati ya moyo wamteue John Wegesa Heche agombee au yeyote kutokea Dodoma, Singida au Manyara watakuja kushukuru
Kwanini hawana sifa..?

Una vigezo gani unavyovitumia kuwa - disqualify..?

Huko CHADEMA ili mtu awe mgombea u - Rais anapaswa kukidhi vigezo gani..?
 
Kiufupi hana agenda yoyote atakayoisimamia akishinda.
Yaani tuchague kiongozi asiye na maono wala agenda ya kukifanyia chama?
Inawezekana kuna fedha zake (za madai yenye mashaka au yasiyo halali ya kipajipigaji) bado hayajalipwa na "CHADEMA YAKE..."

Anaogopa akiondoka atakuwa amepoteza connection na influence yake ya kushinikiza alipwe..

Anaogopa uongozi mpya unaokuja unaweza kuyachunguza madai na kugundua kuwa hayana sifa ya kulipwa...

Hakuna jingine ni hilo tu...

Huu uongo tunaoambiwa ni tajiri mwenye biashara kubwakubwa ndani na nje ya nchi ni mbinu tu za kupigia fedha za chama...

Huchukua fedha kiaina ndani ya chama na kisha baadae kuzileta kwa lugha "nakikopesha chama" na baadae kuzidai na riba juu...

Wenzake wanajua haya yote. Kwa kuwa ameshindwa kujiheshimu mwenyewe, obvious mazingira nayo pamoja na wanaomzunguka hawatamheshimu pia...!
 
Kuna mtu alisema Lissu akishinda chama hakiwezi kumaliza hata miezi miwili, kitakufa.

Baada ya uchaguzi aliingia mitini na mbowe, pengine labda kwa kuona aibu. Chadema ya leo ni vibrant kama ile ya 2010 kuelekea 2015 kabla ya ujio wa lile tapeli lowasa. 😀 😀 😀
 
Mkuu p anzia leo ni marufuku muuliza lissu maswali mepesi , kama uliyouliza majuzi, lissu sio saizi yako
 
Kwa umri nakubali , ila sasa kwingine lissu anabaa sio la nchi hii
Japo nimemtangulia darasa na vidato,ila amenizidi akili,TAL ni akili mingi ila maarifa ni issue kidogo!,mimi nimemzidi kidogo maarifa!。 Mfano,juzi kati nilikuwa US kuangalia uchaguzi wao mkuu,kuna kitu nime observe,ambacho unashabihiana na Uchaguzi。wetu wa 2025 TAL,akikijua, ni bonge la fursa kwake kuichangamkia na kuachana na hayo ma utopia yao,ila yeye mwenzangu hajaiona hiyo fursa, Chadema hawajaishtukia, they are simply mypic due to having myopia,just too blind to see!。
P
 
Kusema Lissu ni myopic ni kumkosea heshima. Si lazima yeye na wewe myaone mambo yote katika mtazamo unaofanana.

Unapoona kuna maeneo anaweza kufanya vizuri zaidi si vibaya ukitoa ushauri kama mzalendo, japo wewe ni wa upande mwingine kichama (sijasema kiitikadi, siku hizi vyama vyetu havina itikadi). 😀 😀
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…