Magazetini
JF-Expert Member
- Aug 16, 2014
- 593
- 1,712
Mwanasiasa mkongwe, Dkt. Wilbroad Slaa akiwa kwenye kongamano la kusheherekea urithi wa falsafa ya hayati Magufuli ameongelea mambo kadhaa ikiwemo serikali kuwanyima taarifa na fursa ya kumuombea Magufuli.
Pia Dkt. Slaa amewapongeza watanzania kwa walivyoonesha upendo wao na kushikamana kama sisimizi na kila aliyemwambia alikuwa na maadui wengi, alimwambia afungue TV yake zilizorekodi umati wa watu katika vituo vyote ambavyo mwili wake ulipita.
========
Dkt. Slaa: Mama Samia tunakupa pole sana lakini hili pia linikumbushe uchungu mkubwa kidogo niliupata na labda Serikali kwenye hili mtusikilize, Serikali mmetunyima watanzania nafasi ya kumuombea baba yetu tunaempenda kwa mwenyezi Mungu katika kipindi kigumu cha maisha yake alipokuwa anaumwa kwa kutuficha taarifa.
Msiogope nikitamka hivi, kama nitakamatwa nitakamatwa mimi. Serikali ni ya kwetu. Wakristo kama kuna wakati tunatakiwa kumuombea mtu ni wakati wa mwisho wa maisha yake.
Tunakuja kuambiwa amefariki lakini tunajua alikuwa anaumwa kabla ya pale na kile ndio kipindi tulitakiwa tujulishwe, huyu ambae alipenda madhehebu ya dini kila siku ya Mungu alienda, kanisani au msikitini.
Kwanini unawanyima watanzania hao fursa na nafasi ya kuwaombea kwa kadiri ya imani zao. Hii iwe ni fundisho limetokea hatuwezi kurudisha nyuma lakini tunaomba Serikali muwe makini, hamuwezi kuhodhi imani ya binadamu.
Dkt. Slaa: Siku hizi ni rahisi hata utafiti hauhitaji kufanya publication, kutafuta hata hela. Chapisha iingie kwenye mtandao online. Haiitaji hata hela siku hizi, mbona mengi ya matusi tunayaingiza kwenye mitandao na yanazunguka bure, kwanini professional article well said ishindwe kuchapishwa iweze kufikia watu kwasababu karibu kila mtu kwa takwimu tulizonazo watanzania takriban milioni 25 wana smartphone.
Ukiwafikia watanzania milioni 25 umefikia critical mass ambao unahitaji kuwapelekea information, hiyo naacha kama challenge.