Dkt. Slaa: Tukio la Tundu Lissu kupigwa risasi na watu ‘wasiojulikana’ ni jambo la kawaida

Mark your words yes, but so what and who are you? Kwa nini kila mtu anasema kulikuwa na mauaji Kibiti na Sitekisheri kabla Lissu hajashambuliwa? Who will mark their words?
 
Duuh......siku hizi anajifanya haelewi "facts ? " ama kweli ukistaajabu ya Mussa utaona....!!
 
Hata wafiche vipi au kuzungusha vipi lakini MUNGU ni mkubwa lazima lazima siku itafika wooote waliohusika kupanga na kutekeleza tukio la kupigwa risasi LISSU chain nzima kutoka juu mpaka chini watashitakiwa.
 
Nishamtoa katika kundi la watu wenye uelewa kila atakachoongea anakua kamezeshwa huyo wakidhani ana mvuto wa kueleza akaeleweka kumbe hamna kitu...
 
Nishamtoa katika kundi la watu wenye uelewa kila atakachoongea anakua kamezeshwa huyo wakidhani ana mvuto wa kueleza akaeleweka kumbe hamna kitu...
Kweli watanzania wamegundua kuwa Slaa ni mchumia tumbo tu, sasa hivi kichwani hakuna kitu empty, hakuna mwenye muda wa kusikiliza pumba zake hana utu tena zaidi ya kuchumia tumbo.
 
Unajua Martin Luther King aliwahi kusema "Hatari zaidi ya ujinga ni ile ya mtu kujifanya hajui kwa makusudi ili kudhulumu haki" Wewe jamaa unafahamu vizuri CCTV camera zilinyofolewa baada ya lile tukio, serikali haitaki kuruhusu tukio hili lichunguzwe na Mashirika ya kimataifa ya Ujasusi, licha ya kuwa Mashirika haya yalisema yako tayari kutoa msaada wa kiupelelezi bure. Huu ni ushahidi tosha serikali imehusika 99.999%. Kama hawajahusika basi wanawe mikono, warudishe zile CCTV camera na waruhusu mashirika haya yafanye kazi yake.
 
Kwanza watu mnashangaza Sana,
Hivi suala la Tundu lissu Lina uspecial gani Zaid ya
1. Alphonse Mawazo
2. Chacha wangwe
3. Mauaji ya kibiti au
4. Kupotea Kwa Ben saa nane?

Watu hasa wafuasi wa Chadema ni washenzi mno Yan, wanataka kila Jambo kupelekwa kisiasa, mengine hayapelekwi Kwa namna mnayotaka,

Bora suala la Lissu aliyeko kwenye matibabu ubelgiji lakin inasikitisha Saa nane hatujui alipo,

Unadhani family ya Alphonse Mawazo, inajisikiaje kusikia mnasikitikia Tundu lissu wakati mawazo hayupo?

Haimaanishi kwamba tusilaani suala la lisuu, Ila ni la kawaida mno,


Na mtu halazimishwi kwenda kumuona kama ambavyo wengine hawalazimishi kwenda kuwaona,

Cc Dr Willibrod Slaa Mnyika
 
Umesomeka... loud and clear..ila!!
 
Kushambuliwa eneo wanaloishi viongozi lenye ulinzi imara na cctv camera kuondolewa na watu wasiojulikana.. kweli ni kawaida
 
Nionavyo mimi :

Kitendo cha mtu kushambuliwa ndan ya makazi yenye ulinzi na washambuliaji kusepa .... Si jambo la kawaida.

Sent from my TECNO WX3LTE using JamiiForums mobile app
MawAzo alipouawa hapakuwa na ulinzi? Karume je?
Kuna professor wangu mmoja wa UDSM mwakyusa amepigwa Risasi , ukienda Kwa afisa wa jeshi kundichi
 
Sio hao tu hata hoja yako wewe Mimi naona ya kawaida ukilinganisha na ya Lema kuhusu lissu
 
MawAzo alipouawa hapakuwa na ulinzi? Karume je?
Kuna professor wangu mmoja wa UDSM mwakyusa amepigwa Risasi , ukienda Kwa afisa wa jeshi kundichi
Mmh kweli kazi ipo huyo profesa wako alikua anakaa sehemu gani ?
Je kwa huyo mjeshi kulikua na kizuizi cha geti la kuingikia kwake (tofautisha tukio la mauaji na la uporaji)
Je unayaelewa vizuri makazi ya wabunge na mawaziri ?

Unaweza nieleza Mawazo aliuliwa kwenye mazingira gani ? (kwa jinsi ulivyosikia wewe)




Sent from my TECNO WX3LTE using JamiiForums mobile app
 
FikraPevu Huyu mzee kwa hakika ameshuka sana viwango vyake vya ufikiri. Yaani kwake, mtu kumiminiwa risasi 32 tena kwenye maeneo ya serikali yanayolindwa ni jambo la kawaida???? Kwa akili, mshumbusi sasa anamzidi huyu mzee wetu
 
Dr Slaaa kaanza kazi yake ya UBALOZI rasmi!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Dhambi ya kuua Binadamu asiye na hatia inamfanya Muuwaji kuweweseka muda wote wa maisha yake hapa Duniani! Kwa kweli JPM na wauwaji wenzake wako wanaweweseka na kutapatapa namna ya kujinusuru na kashifa ya kutaka kumuuwa Mh.Lissu! JPM hadi anawatafuta watu km wakina Dr.Slaa waende kwenye maTV kueneza propanganda eti kupigwa Risasi kwa Mh.Lissu ni jambo la kawaida, kweli kumuuwa Binadamu mwenzako kwa sbb za kisiasa ni jambo la kawaida!!? Dr.Slaa hana Akili siku hizi, huwezi kutumwa kupunguza machungu ya wananchi kwa propaganda Butu ya aina hii.

Hata kama ni kwa namna ipi, kumuuwa mwanadamu mwenzio kwa sababu yoyote ile, haiwezi kuhalalishwa eti ni jambo la kawaida! Dhambi ni ya kuuwa ni mbaya sana kwani tangu JPM atake kumuua Mh.Lissu, yeye na CCM nzima imejaa taharuki ya namna ya kujinasua na kashifa hii hadi wanatumia gharama kubwa ya pesa kununua wapinzani, kununua vipindi vya TV ili kueneza propaganda za kujinasua na kashifa ya kuuwa, wanatumia hovyo hovyo kodi zetu kwa mambo ya hovyo kwa ajili ya kujisafisha na ujinga walioufanya wenyewe kwa makusudi.

Watu wanakufa njaa kwa sbb ya ufujaji wa pesa, wkt Dhambi ya mauwaji wameitenda wenyewe kwa ukosefu wa weledi wa kuongoza Nchi.

Dhambi hufutwa kwa kuitubu na siyo kwa Propaganda za kitoto namna hiyo. Dunia inajua, Watanzania wanajua ukweli wa nani alitaka kumuua Mh.Lissu, ukweli na kumbukumbu hii imejiandika juu ya Ardhi ya Tanzania mpaka mwisho wa Dunia.

Asiye na Akili, atawaamini wazee wa Propaganda lkn kwa kweli, Mungu alitupatia zawadi nzuri ya Akili inayotuwezesha kupambanua yaliyo mema na mabaya bila kuhitaji msaada wa yeyote! Ni dhambi pia kuwa na Akili tegemezi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…