Dkt. Slaa: Tukio la Tundu Lissu kupigwa risasi na watu ‘wasiojulikana’ ni jambo la kawaida

Dkt. Slaa: Tukio la Tundu Lissu kupigwa risasi na watu ‘wasiojulikana’ ni jambo la kawaida

Balozi Mteule na aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Wilbroad Slaa amesema tukio la Tundu Lissu kupigwa risasi na watu ‘wasiojulikana’ ni jambo la kawaida na ameitaka jamii kuliacha Jeshi la Polisi kukamilisha upelelezi na kutoa majibu.

Dkt. Slaa ametoa kauli hiyo wakati akihojiwa na kituo cha runinga cha Clouds juu ya hali ya kisiasa ya Tanzania na mustakabali wa maisha yake baada ya kuondoka CHADEMA, amesema hafurahishwi na baadhi ya watu kuwataja hadharani watuhumiwa wa tukio hilo kwasababu linaharibu uchunguzi wa polisi.

“Mimi kinachoniudhi ni hii watu kusema hadharani kwamba kuna hiki na hiki tunasuspect (tunahisi) waliofanya ni fulani. Sheria inasema ukihisi nenda polisi katoe taarifa sio unaenda kwenye vyombo vya habari”, amesema Dkt. Slaa.

Amesema hawezi kuzungumzia kwa undani suala la Lissu kupigwa risasi, ikizingatiwa kuwa watu wengi wamepigwa risasi nchini na kazi ya kuwabaini wahalifu waliomshambulia ni ya polisi sio viongozi wa siasa au wananchi.

“Lakini kama binadamu hakuna anayependa binadamu yeyote aumizwe lakini matukio haya ya kuumizwa yametokea nchi hii kwa watu wengi sana. Na mimi sio chombo cha dola kujua kwamba unanyoosha kidole kwa kitu ambacho hatukiamini; mimi ni msomi”, amesema Dkt. Slaa na kuongeza kuwa,

“Ukitoa taarifa za upelelezi unaharibu upelelezi. Mimi niko Canada mauaji yapo kila siku na watu wanapotea, wanapigwa risasi wakiulizwa polisi wanakwambia suala hilo liko kwenye upelelezi tukifikia hatua nzuri tutatoa taarifa”.
dah njaa mbaya sana
 
Kwa mila za kiafrika ni vibaya kuongea uku unakula
 
Ni jambo la kawaida sana hakuna sympathy hapa hiyo ndio siasa Mzee wangu Slaa uko sahihi wamedunguliwa kina JFK ije kuwa huyo mtaka sifa.
 
Ukisharudi CCM wewe utachanganyikiwa tu. Msimuone Slaa na suti zake, kichwani hakuna kitu ni kijani tuuuuuuu.

Huyu muacheni aendelee kujiharibia.
 
Ni kweli kabisa na kila siku nimeendelea kusema humu JF ya kuwa hakuna ushahidi wa kutosha unathibitisha mtu aliyemdungua Lissu risasi. Nikaendelea kuwapa member walalamishi wasiotaka kuelewa wakereketwa wa upande wa pili kama wana evidence wapeleke polisi haki itendeke washukiwa wafikishwe kortini.

Note;"huna haki ya kuzungumza pasipo kuwa na ushahidi wa kile unachokizungumza"
Hata hao nao ni suspect unawezaje kupeleka kesi ya nyani kula mahindi kwa ngedere?
 
Sikutegemea kusikia haya kwa ndugu yetu Slaa. Kusema tukio la TL ni la kawaida. Kila mtu anaishangaa Tz kwa tukio hili isipokuwa yeye. Shame on him. Asiwe na chuki kama babu yake. Nimemsifu kwa kusema hali ya democrasia ni mbaya. Sasa alishindwa vipi kusema ukweli kwa hili ama limekuwa kubwa mno kumeza.
Ni bora hata angeacha kulijibu swali hilo kuliko huo uduwanzi aliojibu,lakini tusimlaumu sana kama amefikia kushikiwa akili na lile shangingi tusitegemee cha maana toka kwake.
 
Huyu mzee ndo maana urais aliukosa anaonekana angekua rais bwege kuliko marais waliowahi kutokea kama kaweza kudanganyika na ka cheo kaubalozi tu
Mpaka anabadilishwa akili kutoka kua mtetezi wa.wanyonge kama tundu.lisu.mpaka kuwa papet.wa mafisadi
 
Huyu ni msaliti wa Ukatoliki, haaminiki hata kidogo. Achana naye. CCM damu sasa, what else do you expect na ameahidiwa ubalozi, hawezi kulikoroga. Kutoka kuosha vyombo hotelini, leo ni diplomat, hawezi kuuona ubaya wa Lisu kupigwa risasi na huyo anayetuhumiwa.
Ha.ha
Ha
Ha
Alikua.naosa.vyombo na.masinki kanada
 
Yeye mwenyewe alipokuwa katibu wa Chama cha upinzani mke wake alipigwa mapanga na alikaa India kwa kipindi kirefu akitibiwa Polisi walimpa hitimisho la uchunguzi?

Tundu Lissu amepigwa risasi mchana katika makazi ya watumishi waandamizi wa serikali anasema ni tukio la kawaida.
Moja ya wazee wasiokua.na.faida hapa.tz.ni huyu silaha.me namkubali.walioba tu mzee wa katiba
 
Ukishakuwa mnufaika unaangalia maslai yako,yeye alishafulia hivo lzm aimbe nyimbo za kusifu na kuabudu,akienda kinyume na uteuzi utenguliwa,ili uchague ukamanda ukashindie Mihogo, au uimbe kusifu na kuabudu ili usogeze siku.
Kale kakibarua kake.kanada kamuachia nani huyu mzee
 
Waliomfulisha ninakina nani na Kwa sababu gani? Chama kilimuacha aendelee na ustaarab wake, sasa huo ndio ustaarab alouchukua. Tulishangilia sana kusikia kawa muuza bidhaa supamaket, tulitamani apotelee mbali kisa kamkataa Lowassa chamani. Sasa kaibukia kwingine ndio maana kinatuuma sana. Pole yetu sisi
Una undugu.na.nabiii.wa.bia.maana akili.zenu zafanana
 
Back
Top Bottom