Dkt. Stergomena Tax akabidhi Ukumbi wa CCM Magu kwa uongozi wa Chama Wilaya baada ya ukarabati

Dkt. Stergomena Tax akabidhi Ukumbi wa CCM Magu kwa uongozi wa Chama Wilaya baada ya ukarabati

DodomaTZ

Senior Member
Joined
May 20, 2022
Posts
197
Reaction score
233
Untitled-3J.jpg

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Stergomena Lawrence Tax (Mb) tarehe 15 Agosti 2025, ameukabidhi Uongozi wa Chama cha Mapinduzi CCM wilayani Magu Mkoa Mwanza, Ukumbi wa CCM baada ya kukamilisha maboresho na ukarabati mkubwa.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo yaliyofanyika Viwanja vya Ofisi ya CCM Magu, Dkt. Tax alieleza kuwa amekamilisha ukarabati huo ikiwa ni utekelezaji wa maombi yaliyowasilishwa kwake na Kamati ya Siasa ya Wilaya ikiwa mchango wake kama Mwana CCM na Mwana Magu.

Aidha, amewakumbusha wana CCM Magu, kuendelea kutoa ushirikiano na kuwatia moyo kwa kuwaunga mkono Viongozi na wanachama wanaojitilea kuchangia katika shughuli za maendeleo katika jamii, ili kuwapa hamasa na kuondokana na mtazamo hasi kuwa wanaojitolea wanataka nafasi za Uongozi, Mitazamo ya aina hiyo hufifisha ari.

Naye Mwenyekiti wa CCM Magu, Komredi Enos Ndobeji Kalambo kwa niaba ya wana CCM Magu, alimshukuru Waziri Tax, kwa moyo wake wa kujitoa na kuainisha kuwa ni aina ya viongozi wachache wa mfano wa kuigwa.
Screenshot 2025-08-18 141936.jpg

Screenshot 2025-08-18 141952.jpg

DSC00864ccm.jpg

Screenshot 2025-08-18 142011.jpg
 
Back
Top Bottom