GE2025 Dkt. Stergomena Tax aonya viashiria vya kuvuruga amani kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

GE2025 Dkt. Stergomena Tax aonya viashiria vya kuvuruga amani kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DogoWaNjombe

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
3,284
Reaction score
7,708
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt Stergomena Lawrence Tax (Mb), tarehe 7 Julai 2025, ameonya na kuwatahadharisha Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi CCM, kuwa macho na kujiepusha na makundi au watu wenye nia ovu na Nchi ya Tanzania, watakaotaka kuutumia mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025, kuleta vurugu.

Dkt. Tax, ameyasema hayo wakati akizungumza na Wajumbe wa CCM kata ya Kandawe, Magu mkoani Mwanza, alipowatembelea katika ziara yake kama Mlezi wa Kata hiyo.

Katika hotuba yake, Waziri Tax amewakumbusha wajumbe hao kujitokeza kwa wingi kupiga kura ili kutimiza haki yao ya kikatiba ya kuwachagua viongozi wanaoamini kuwa watawaletea maendeleo kwa ajili ya Ustawi wao na Taifa kwa ujumla.

Aidha, Ziara hiyo ya kutembelea Kata ya Kandawe, imehudhuriwa pia na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Magu, Komredi Enos Ndobeji Kalambo.
 
NA CHADEMA WASIKIE KABISA WASIJE KUSEMA HAWAKUAMBIWA MAEMA
 
Chama shetani CCM kimeivuruga amani ya Watanzania kuanzia kwenye mioyo yao mpaka kwenye miili na uhai wao.

CCM chama cha kuteka na kuua kila anayekosoa uovu, kimeikosesha nchi amani ya kweli.

CCM ni shetani, jitenge na shetani uiepuke laana ya Mungu. Kuteka na kuua watu, ni matendo ya shetani yenye kumwudhi Mungu wa kweli.
 
Back
Top Bottom