Dkt. Tulia Ackson alamba kura zote asilimia 100, aapishwa kuwa Spika wa Bunge

Dkt. Tulia Ackson alamba kura zote asilimia 100, aapishwa kuwa Spika wa Bunge

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,681
Reaction score
8,887
Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, Dkt. Tulia Ackson, ameshinda uchaguzi wa nafasi ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kupata kura 376 kati ya 376 zilizopigwa sawa na asilimia 100.

Hii inamaanisha na wabunge 19 wa chama cha CHADEMA waliohudhuria leo kura zao zimo kwenye jumla hiyo.

Dkt. Tulia Akckson ameapishwa kuwa Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akimrithi mtangulizi wake aliyeng'atuka, Job Yustino Ndugai.
 
Aliyekuwa Naibu wa Spika wa Bunge, Dkt Tulia Ackson ambaye leo alisimama kama mgombea wa Uspika amepata kura 376 za wabunge wote

Dkt. Tulia alikuwa akichuana na wagombea wengine nane ambao wote hawakupata hata kura moja, aidha hakukuwa na kura iliyoharibika

Nafasi ya Spika iliachwa wazi baada ya aliyekuwa Spika, Job Ndugai Kujiuzulu
 
Dr. Tulia Ackson amechaguliwa kuwa spika 7 kwa kupata kura zote 376 za wapiga kura. Tutalajie bunge imara kushinda la mtangulizi wake? au ataweza kweli kuhimili mikiki mikiki ya kukosolewa na wapinzani na wanaharakati nje ya bunge.

Kwa sasa yeye ndiye kiongozi mkuu wa bunge tofauti na wakati uliopita, alivyokuwa chini ya kivuli cha Ndugai, kwahiyo ukosoaji wote utakuwa unaelekezwa kwake moja kwa moja kama ilivyokuwa kwa mtangulizi wake.

Je, atahimili mikiki mikiki ya siasa za ukosoaji na kuimarisha utendaji wa bunge?
 
Kwa Mh.Tulia kuwa speaker hakukuwa ni kitu cha kushangaza ila muda mwingine shirikisha ubungo wako na be yourself not pretending,hao unaowaita ni wabunge wa upinzani je wanawakilisha chama gani?honestly mkuu unataka kuniambia hujui wasifu wa kuwa mbunge?

Sometimes middle class nyie mnanishangaza mno.
 
Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, Dkt. Tulia Ackson, ameshinda uchaguzi wa nafasi ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kupata kura 376 kati ya 376 zilizopigwa sawa na asilimia 100.

Hii inamaanisha na wabunge 19 wa chama cha CHADEMA waliohudhuria leo kura zao zimo kwenye hiyo jumla.

Spika Tulia Akckson ameapishwa kuwa Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akimrithi mtangulizi wake aliyeng'atuka, Job Ndugai.
Jobu maskini hakutegemea kilichotokea mpaka kuukosa uspika wake ambao ulikuwa ushaota mizizi tena kuukosa kwa kiwango hiki, Rais wa nchi inabidi tu aheshimiwe hakuna namna nyengine, mama akiwa nyumban lakini kazini ni mkuu wa majeshi yote.
 
Back
Top Bottom