babu bulicheka
JF-Expert Member
- Mar 26, 2021
- 822
- 1,048
Wakumbuke ya Babu SeyaTulia yupo sawa.
Ndipo akili ziwarudi
Watanganyika hovyo sana
Akili za kuimba Iyena iyena na
Tunaimani na.......... Hoya hoya!!!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wakumbuke ya Babu SeyaTulia yupo sawa.
Hii ndio hulka ya ma- dr na ma- propesa wa Tz ni majanga matupu. Ndio maana kuna wakati namuona msukuma ana nafuu kuliko hawa watu 😄
Katiba inasema Rais ni Mkuu wa nchi. Sura ya pili, ibara ya 33, kifungu cha kwanza.
Which means Rais yuko juu ya kila kitu na kila mtu, anaweza kumtaka hata mkeo kinguvu, kama chifu wa makabila. Tulia Ackson yuko sahihi.
Mkenge mwingine huu aliotuingiza Nyerere, u-chifu wa kwao.
Siku ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere mwaka jana mwanae Makongoro alisema babu yake alikuwa chifu, na bibi yake (aliyemzaa Mwalimu) alitakwa kuolewa kinguvu na chifu Burito, kijiji cha mwanamke kikasema binti hataki, Chifu Burito akasema anhaa, nakata huduma zote za kijamii kwenda Busegwe, Busegwe wakaambiana kijiji is bigger than kibinti kimoja, wakamwachia, binti Mgaya akaja kuchukuliwa mzega mzega kwenda Butiama, akamzaa Mwalimu kinguvu. Some serious stuff but typical Makongoro, he was laughing like a drunken sailor.
Ndo huu Urais wa ki-chifu aliotuletea Mwalimu. And he had brass set, anadiriki kusema angetaka angeweza kuwa dikteta, katiba inamruhusu. Mbona hukuibadilisha? Miaka 29. Baba wa Taifa uchwara wa dunia ya tatu.
Kuendelea kumpa lawama mtu aliyepita miaka 50 iliyopita ni kukosa akili. Nchi gani ambayo Ina rais mtendaji kama TZ ambaye hana mamlaka sawa na rais wetu?
Kujaribu kujisahaulisha historia ndio upunguani mkubwa zaidi. Taifa hili by and large limekuwa brainwashed and bamboozled na fikra za Nyerere, watu wanafanya vitu kwa sababu Nyerere alisema.Kuendelea kumpa lawama mtu aliyepita miaka 50 iliyopita ni kukosa akili. Nchi gani ambayo Ina rais mtendaji kama TZ ambaye hana mamlaka sawa na rais wetu?
Mkuu nakuelewa sana nini katiba inasema na pia uko haja kuangalia practice iko kwenye groud.Hata kwa katiba ya sasa serikali inatakiwa ipate kibali cha kukusanya kodi yoyote kutoka bungeni na bunge ndilo linatakiwa liridhie mipango yote ya serikali. Bahati mbaya sana bunge letu limekuwa la kugonga muhuri tu mambo ya serikali badala ya kuwa msimamizi na muwajibishaji wa serikali.
Katiba ya JMT, 1977
136.-(1) Fedha hazitatolewa kutoka Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali kwa ajili ya matumizi ila kwa mujibu wa masharti yafuatayo:- (a) fedha hizo ziwe kwa ajili ya matumizi ambayo yameidhinishwa yatokane na fedha zilizomo katika Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali na idhini hiyo iwe imetolewa na Katiba hii au sheria nyingine yoyote; (b) fedha hizo ziwe kwa ajili ya matumizi ambayo yameidhinishwa ama na sheria ya Matumizi ya Serikali iliyotungwa mahsusi na Bunge au sheria iliyotungwa kwa mujibu wa masharti ya ibara ya 140 ya Katiba hii.
138.-(1) Hakuna kodi ya aina yoyote itakayotozwa isipokuwa kwa mujibu wa Sheria iliyotungwa na Bunge au kwa mujibu wa utaratibu uliowekwa kisheria na uliotiliwa nguvu kisheria na sheria iliyotungwa na Bunge.