BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 706
- 1,716
Kwa niaba ya Dkt. Tulia, tuzo hiyo imepokelewa na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais -Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Zainab Katimba.
Malkia huyu alipata mafunzo ya elimu ya Juu ya sheria katika chuo kikuu Dar sa alaam na baadaye Capetown nchini Afrika ya kusini na kushiriki tafiti nyingi duniani kisha mnamo mwakw 2015 aliteuliwa kuwa Naibu Mwanasheria mkuu wa serikali.
Ukomavu wa kisiasa na uthubutu wake vilimjaza ujasiri na kuamua kujitosa kugombea ubunge kwenye jimbo lilikuwa likiongozwa na mbunge mwenye rekodi ya kuwa idadi kubwa ya kura bungeni.
Malkia Dkt Tulia anaota ndoto kubwa ya kizalendo, akitamani kuona Mataifa mengine duniani yanajifunza kutoka tanzania hasa usawa wa kijinsia kwenye nafasi za maamuzi.
October 2023 Tanzania ilipata heshima kubwa na yakihistoria duniani baada ya Dkt Tulia kushinda kiti cha Urais wa muungano wa mabunge Ulimwenguni IPU akiwa mwanamke wa tatu kushika wadhifa huu.
Tulia analikumbuka sekeseke la kuandamwa na wajumbe wa IPU kule Genever Uswis October 2024 alipokaliwa kooni na wajumbe dhidi ya safari yake ya usuluhishi nchini Urusi na kujikuta akikalipa, tukio lililoitikisa dunia.
Waneni wa mambo hukoleza kuwa Nabii hakubaliki kwao lakini ni tofauti kwa Malkia huyu anayekiri kupewa heshima na mhimili wa bunge na kuhusu jinsia siyo mjadala tena.