masopakyindi
Platinum Member
- Jul 5, 2011
- 18,207
- 13,839
View: https://www.youtube.com/watch?v=kMc6CYfZzZE
Nikifikiri kizazi cha watanzania wenye jeuri ya nchi yao kiliishia na Mwalimu Nyerere.
Wakati wa Mwalimu, hakuna mwanasiasa wa nje ambaye alikuwa hajitayarishi vilivyo kuongea na mwanadiplomasia wa Tanzania.
Wanadiplomasia wabobevu kama Mzee Mahiga kizazi hicho kilicho pikwa na Mwalimu kimepotea kabisa.
Dr Tulia karudisha heshima ya kujibu hoja kibabe na kujiamini akiwa anajibu ana kwa ana.
Hii ndiyo jeuri ya mtanzania iliyopotea miaka mingi.
Akiwajibu wale wazungu waliohoji kapata wapi kibali cha kuongea na Putin wa Urusi, kimsingi Dr Tulia kawaambia tuheshimiane, hunipangii pa kwenda alimradi nilitaka kuja kwako hukunikaribisha-tuheshimiane!!
Mzungu akalewa za uso!
Pia soma: Tulia Ackson awataka viongozi wa magharibi kumheshimu. Ni baada ya kushambuliwa kuhusu kukutana na Vladmir Putin