Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,362
- 48,879
Sijui kama ni unafiki, ulaghai, akili kidogo au tamaa, ambavyo huweza kumfanya mtu kuwa mtumwa wa ujinga.
Hivi karibuni, Naibu Spika Tulia, mbele ya Rais wakati Rais akiwaapisha mawaziri aliowateua, alitamka wazi kuwa Rais na Serikali, ni kila kitu. Na kwamba, japo Bunge linaweza kuishauri Serikali, lakini Serikali hailazimiki kufuata ushauri wa Bunge.
Kwa maneno haya, maana yake Bunge haliwezi kubadilisha chochote ambacho Rais au Serikali wanataka. Kiuhalisia, hii inamaanisha kuwa uwepo wa Bunge hauna maana. Kila kitu kinaweza kufanywa na Rais na Serikali. Kama ndivyo, kwanini pesa ya walipa kodi iendelee kuhudumia taasisi ambayo haina msaada wowote?
Kama bunge haliwezi kubadilisha chochote ambacho Serikali na Rais wanataka, si aheri Bunge lisingekuwepo, na hiyo pesa inayopotea, Serikali na Rais wakaitumia kuwaletea wananchi huduma muhimu?
Kioja zaidi ni pale Samia aliyesema Bunge si chochote mbele ya Rais na Serikali, anagombea uongozi wa taasisi ambayo, kitafsiri, haina maana yoyote! Kama Bunge halina maana yoyote mbele ya Rais na Serikali, anataka uongozi kwenye chombo kama hicho kwaajili ya nini? Ni uroho na tamaa ya mapato binafsi au kuna kitu kingine?