Dkt. Tulia atakuwa mbunge wa kwanza Tanzania nzima kutangazwa mshindi wa kiti cha Ubunge 2025

Kama ni kweli itakua jambo jema! Ni vizuri wasitishe ugawaji wa hilo jimbo ili kupunguza gharama kwa serikali.

Wapinzani wanasema serikali inataka kuligawa jimbo ili kumlinda Dk Tulia.
Dr Tulia anakubalika sana na wana Mbeya. hata kama mkoa mzima wa Mbeya lingekuwa ni jimbo moja la uchaguzi basi Dr Tulia ndiye angempita na kushinda kwa kishindo maana kila utakakokwenda ndani ya mkoa wa Mbeya Dr Tulia anakubalika.
 
Viongozi wa CCM mkoa wa Mbeya , mchangieni pesa kidogo mdogo wenu Lucas mwashambwa apunguze njaa. Hana uwezo kielimu wa vyeo vya kuteuliwa lakini kwa uwezo wake mdogo anajitahidi kuwapigia debe japo hakuna anayemsikiliza
Mimi ni mkulima na sina njaa maana nakula kwa jasho langu kwa kazi ya mikono yangu kwa kushika jembe kwa nguvu ,bidii na maarifa.
 
Dr Tulia anakubalika sana na wana Mbeya. hata kama mkoa mzima wa Mbeya lingekuwa ni jimbo moja la uchaguzi basi Dr Tulia ndiye angempita na kushinda kwa kishindo maana kila utakakokwenda ndani ya mkoa wa Mbeya Dr Tulia anakubalika.
Hivi kwa nini huwa unaweka namba za simu? mwisho wa posts zako? ili kusudi viongozi wa CCM wanaozurura humu wakuone na kukupa teuzi? posts zako zimekaa kinafiki sana na uongo mwingi na ukweli unaujua.
 
Dr. Tulia Akson ni Nyota na Nuru ya Mbeya mjini kimaaendeo. Ni nyota inayong'ara Tanzania yote, Africa na Dunia nzima.

Ameweza, anaweza, anapendwa na wana Mbeya na kwa hakika atapata ushindi mkubwa wa kishindo kikuu Mbeya mjini endapo atagombea tena, uchaguzi ujao.
 
Upande wa chama kazi ilishakwisha na hakuna atakayechukua Fomu ya ubunge zaidi ya Dr Tulia mwenyewe. Kila mwana CCM ameridhishwa na utekelezaji wa ilani ya CCM Katika Jimbo la Mbeya na namna Dr Tulia alivyofanya kazi kubwa ya kuwatumikia wananchi na kugusa maisha yao ,hali iliyokiheshimisha na kukipatia sifa na heshima kubwa sana chama pale Mbeya mjini. Kwa hiyo kila mtu ameridhika kuendelea kwa Dr Tulia kwa awamu nyingine zaidi.

Pia mimi sijaandika kwa kujipendekeza bali nimeandika ukweli na uhalisia wa mambo unaoendelea katika jimbo la Mbeya mjini.
 
Akikujibu nishtue😂😂😂😂
Kwa sasa alishapoteana sana hasa baada ya kuona hata chama chake chenyewe kimepoteza mvuto kwa watanzania ,hakikubaliki wala kuaminika na watu,maana kila mtu anajuwa kama ni gari basi wakati wowote mnaweza mkashushwa au kubadilishiwa gia mteremkoni na hivyo kuwapeleka na kuwamwaga korongoni.
 
Unaongea kama vile wewe ndiyo Katibu Mkuu wa chama! Au ndiye mratibu wa hilo zoezi la kuchuja wagombea kabla ya uchaguzi. Kumbe you are just a nobody.
 
Unaongea kama vile wewe ndiyo Katibu Mkuu wa chama! Au ndiye mratibu wa hilo zoezi la kuchuja wagombea kabla ya uchaguzi. Kumbe you are just a nobody.
Inaonekana wewe ni mtu unayependa kupewa majibu ya uongo au utapeli .hupendi kuambiwa ukweli kama huu nao kupatia mimi hapa.
 
Tulia atafute kazi nyingine au labda apewe ubunge wa viti maalum.
 
Tulia atafute kazi nyingine au labda apewe ubunge wa viti maalum.
Dr Tulia atazoa kura zote pale Mbeya mjini,maana hakuna mtu aliye na ubavu wala uwezo wa kushindana naye katika sanduku la kura,kwa kuwa kila utakakokwenda unakuta ni Dr Tulia akipewa sifa na pongezi kwa kazi kubwa aliyoifanya ndani ya muda mfupi wa uongozi wake.
 
Hata kama anakuhonga lakini muambie ukweli kuwa Mbeya ni Ngome ya Sugu na Mwabukusi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…