Dkt. Tulia: Kama wasingeenda Mahakamani ningetangaza nafasi kuwa wazi

Dkt. Tulia: Kama wasingeenda Mahakamani ningetangaza nafasi kuwa wazi

Iweje wabunge wa CUF walipovuliwa uanachama wao, papo hapo, wakafukuzwa na ubunge wao, kwa kuwa Bunge lilieleza wazi kuwa haliwezi kuendelea na wabunge wasiotokana na chama chochote cha siasa!
1. Wabunge wa CUF nao walienda Mahakamani?

2. Akina Halima walienda mahakamani lini? Chances are walienda huko mapema kabla hata Baraza Kuu halijakaa maana walianticipate matokeo

CHADEMA wala wasiwe na hofu na waweke ushahidi wao vizuri. Bila shaka kesi ikianza tu, Mahakama itataka kujua uhalali wa ile barua ya kwanza iliowateua na kama kweli ilikuwa forged ama la. Mzizi wa kesi utaanzia pale

Then watataka kucheck kama kufukuzwa kwao na kile kikao cha awali cha CC kulifuata natural justice (kumsikiliza kwanza mtuhumiwa kabla ya kuissue adhabu). Haya mambo hayahitaji kutoa povu na lawyers wenye utulivu kama Kibatala ndio wanaoweza kupambana

Hii game kwa msaada wa nguvu ya Serikali litaishia kwa akina Mdee kubakia Bungeni until 2025 then wanatimkia CCM ambapo wanaweza kupewa tena Ubunge wa chee after 2025
 
Wale wa cuf sababu za kufukuzwa kwao hazikuwa na adhari kwenye utendaji wa Bunge

Chadema iligoma kupeleka wabunge viti maalum, Jambo la viti maalum ni Jambo la kisheria

So wakina mdee walivuliwa uanachama wao Kwa kutiii sheria ya viti maalum

Hapo sasa ndio chadema watafeli hata mahakamani
Faida ya kujua kusoma na kuandika ndiyo hii sasa.
 
Je ikionekana wamefukuzwa kihalali hizi Siku watakazoingia bungeni Hadi uamuzi huoni Kodi yetu itakua imeenda bure Kwa malipo yao

Wewe una hoji kuhusu kodi,mbona hauoji kuhusu chama cha upinzani tena kikuu kinapewa Ruzuku ila hawajengi ata Ofc wamebaki na kimgahawa pale ufipipa,mbona hauoji kuhusu hela walipewa na Sabodo 400mln na bado hawajenga Ofc,vipi kuhusu michango ya wanachama wanayochanga kila mara Mbowe anaishia kuitumbua kwenye mikutano hisiyo kuwa na Tija?.
 
Madaktari wa falsafa,wanafeli wapi? Hata sisi tusiowabobezi wa Sheria tunaona kuwa Kiti kimefanya maamuzi kisiasa.
Waandishi wanauliza, mbona Kuna double standards, halafu jibu linakuwa usiniulize masuala ya nyuma,tujielekeze kwenye suala lililopo mezani.
Hukumu ya Mahakama Kuu au Rufaa,huwa inakuwa presedence kwa maamuzi ya mbeleni.
 
MIMI KAZI YANGU NI MOJA TU - SPIKA TULIA AKSON

Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Tulia Ackson Tulia Ackson amezungumza na wanaHabari kuhusu uamuzi wa kuwafukuza Bungeni Wabunge 19 wa CHADEMA Halima Mdee na wenzake. Amesema yeye anasubiri Maamuzi ya Mahakama.

View attachment 2227166
Mpuuzi huyo.Kwenda mahakamani ni jambo moja,sawa.Je,mahakama imeshasikikiza na kumpa jibu kwamba wasiondolewe bungeni?Au huo ujingaujinga aliousomea ndiyo umemtuma tu afanye hivyo?Bogus!
 
Mimi hili suala hata silielewi. Hivi kwa nini Spika hakuwaita wakina Halima na NEC ili watoe uthibitisho kuwa barua waliyompa ni halali? Maana kama kweli walimpa barua basi Spika ndio injured party na ni yeye ndie aliyepaswa kuchukua hatua dhidi ya waliomdanganya kwa kumpa nyaraka za kughushi. Ukimya wake kwenye suala hii ndio unanitia wasiwasi kuwa hamna nyaraka iliyowasilishwa kuwatambulisha wakina Halima kuwa wateuliwa wa Chadema. Hii ndio inayonifanya nione tuhuma za kughushi hazina mashiko. Labda sasa Chadema watumie Mahakama kumlazimisha NEC atoe nakala za barua alizopokea kutoka Chadema.

Amandla...
 
Hii nchi imejaa wapumbavu wengi z sana!
Ulitaka raisi akae hotel ya uswahilini huko new York?

Halafu nyie washamba mnateseka sana for nothing. Hapa Tanzania tu kuna hotel zina bei kubwa kuliko hiyo. Kuna ubaya gani?
Watu kuhoji matumizi ya kodi zao si upumbavu kama unavyotaka kutuaminisha.
Ingekua rais anatumia fedha zake mfukoni wala Hamna mtu angejisumbua kuhoji.
Jaribu kuficha ujinga wako
 
Wakati ule ulikuwa mkakati wa kumzoofisha seif Shariff Hammad na kumpa nguvu Prof.Lipumba
Na wakati huu ni mkakati wa kudhoofisha CHADEMA na kuwapa nguvu Covid19, CCM bado inaendelea na mikakati.
Hili la "mkakati wa kudhoofisha Seif Sharif Hamad na kumpa nguvu Prof Lipumba" hakuna supporter wa CCM aliyekuwa akilisema wakati ule lakini sasa wanalisema, hivyo huko 'mbele ya safari' hata hili la hao Covid19 watafunguka na kusema ukweli.
 
Na wameanza kwa kushangilia,vicheko,kugonga meza,kugonga mikono ya kujipongeza na hata kurukaruka kule bungeni.
 
  • Thanks
Reactions: Qwy
Na wakati huu ni mkakati wa kudhoofisha CHADEMA na kuwapa nguvu Covid19, CCM bado inaendelea na mikakati.
Hili la "mkakati wa kudhoofisha Seif Sharif Hamad na kumpa nguvu Prof Lipumba" hakuna supporter wa CCM aliyekuwa akilisema wakati ule lakini sasa wanalisema, hivyo huko 'mbele ya safari' hata hili la hao Covid19 watafunguka na kusema ukweli.
Kuna jambo zuri sana limetokea kuhusu COVID19.

Spika katoa kauli kwamba suala lipo mahakamani. Mahakama ikatoa uamuzi mchana.

Swali, Spika aliwasiliana na nani? Lini na saa ngapi? Lini alipokea barua pepe, saa ngapi?

Kuna watu waliokuwa na shaka, Spika Tulia na Jaji Mgeta wameondoa wasi wasi

COVID wana 'mawakili' na serikali, unajiuliza nani mwenye kesi mahakamani dhidi ya nani?

Kila kitu kitakuwa wazi kama ile kesi, naogopa sijui watachomoa vipi!
 
Ungekuwa ndugu yangu wewe ningebadilishana na gunia la ufuta.Hopeless kabisa
Wale wa cuf sababu za kufukuzwa kwao hazikuwa na adhari kwenye utendaji wa Bunge

Chadema iligoma kupeleka wabunge viti maalum, Jambo la viti maalum ni Jambo la kisheria

So wakina mdee walivuliwa uanachama wao Kwa kutiii sheria ya viti maalum

Hapo sasa ndio chadema watafeli hata mahakamani
 
Tulia ukilala unasali kwa roho na kweli? Hujajifunza tu ya Job? Cheo ni dhamana na WAKATI SI MILELE!
Yuko wapi Job leo hii
Yuko wapi Sabaya
Yuko wapi Bashite....
Yako wapi mafirauni yote yaliyotamba kwa nyakati zao?
Dah....Profesa....Hilo Somo linamuhusu na mwenyekiti wetu? Au double standards zinaendelea? 🤣🤣🤣🤣🤭
 
Hoja ya Spika ipo kisheria
Kama yupo anayeamini kuwa Spika amekiuka Sheria ni vema aje na nukuu ya vifungu vya sheria
 
Back
Top Bottom