Paschal, sifahamu wewe kama ni practising mwanasheria au umesoma sheria. Najua ni mwandishi wa habari. Ninaheshimu chochote unachokifanya!
Point number 7. Ombi la kupinga kufutwa uanachama liko ndani ya submission iliyokataliwa on technical grounds. Sijui umefikiaje kusema ombi lao halijakataliwa wakati mahakama imeamua kutolisikiliza!! Mahakama haikutoa maelekezo yoyote zaidi ya ku-strike out kesi, jambo ambalo linawapa wadai nafasi ya kukata rufaa au kuleta ombi jipya. Kwa sasa hiivi hakuna hata zuio la mahakama akina Mdee wasiondolewe Bungeni!! Please stop gaslighting readers here. Malice ni kitu kibaya sana na katika nchi nyingine license to practice inaweza kuwa revoked na hata mtu akaadhibiwa kwa fine na prison time kwa kutokuwa mkweli!
Ni Spika alisema hatachukua hatua kwa kuwa kuna kesi mahakamani. Ninaona akina Mdee wakipatiwa nafasi ya kufanya jambo hili kwa namna mpya. Ni haki yao na ni jambo jema! Sababu za kufanya hayo ni za kisiasa, hata hivo! Bunge linawahitaji akina Mdee kwa sasa ili kutimiza matakwa na sheria/taratibu nyingine muhimu. Spika Ndugai, hasa, hakuacha jambo hili lifike hapa lilipofika. Spika Dr. Tulia kaliacha limesonga mbele na sasa linaumbua taasisi! Sasa tutasikia hata ji taasisi gani itamtaarifu Spika kuhusu maamuzi ya mahakama (zingatia ni taasisi ipi ilitoa taarifa ya kuwepo kwa shauri mahakamani).
Kilicho wazi - mihimili iko huru katika muundo tu. Kiutendaji haiko huru!