Dkt. Tulia: Nyanda za Juu tumechoka kuwa washangiliaji na sisi tunataka treni ya umeme kama 'Wenzetu'

Mimi sio mwanasiasa,lakini alichosema muheshimiwa Dr Tulia ni sahihi kabisa,maparachichi yanatoka Mbeya,Njombe,Songea,mahindi,chai,kahawa,ndizi,maharage,magimbi nk,lakini miundo mbinu toka uhuru hadi sasa kimya,na huku kodi ikitakiwa sana.Na vilevile ni mkoa uliokaribu na mipaka ya nchi mbili!Iweje iwe na miundo mbinu mibovu huku tunataka kodi?Waziri alione hili bila kigugumizi wala soni.Kazi iendelee.
 
Mfuatilie kaka yake Tulia kuanzia dakika ya 5-13
 
alikuwa wapi siku zote asiongee..anyamaze tuiponye nchi kwanza , angeongea kipindi cha awamu ya tano ndo tunemskiliza vizuri
 
Pamoja na mimi kutoka kanda pendwa lakini Tulia kasema kweli.
 
Msilete hizoo!
Ni Mwalimu aliyewekeza barabara mikoa ya Mbeya na Iringa.
Wengine wote wanapita tu utafikiri mikoa hiyo haipo duniani.
Barabara ya Tanzam ilijengwa 60's na kukarabatiwa miaka inayofuata.
Hii haiwiani na mikoa iliyozungushiwa barabara mpaka wanachoka wenyewe, hasa huko kwa mwendazake.
 
Wakati watu wanalalamika kuwa jiwe linapendelea kanda maalum hawa ndio walikuwa wanatunanga kwa kusema hata chato ni Tanzania na wote waliohoji wakahusishwa na Uchaga/Kilimanjaro. Leo ni nini kimemkuta tena
 
Asante Dr Tulia , at last Mbeya tumepata sauti ya kudai na sisi maendeleo ya Jiji kama ilivyo Mwanza, ARusha na hata Dar es salaam.

Kwa makusudi toka Awamu ya Pili, Tatu na Nne na Tano HAKUNA uwekezaji wa maana ulioingia Mbeya, si barabara , viwanda au hata huduma za kiwango cha kitaifa.
 
Wakati watu wanalalamika kuwa jiwe linapendelea kanda maalum hawa ndio walikuwa wanatunanga kwa kusema hata chato ni Tanzania na wote waliohoji wakahusishwa na Uchaga/Kilimanjaro. Leo ni nini kimemkuta tena
Ndio maana amesema " tumechoka kushangilia"
 
Ahsante bwashee

kny Dr Tulia
 
Salamu zimfikie Sugu ambaye alikuwa anazungusha tu makalio na kutukana watu mle jengoni.
 
Na je ya kati hakuna magofu na majengo kama vibanda umiza lakini wanajengewa treni ya umeme,kumbuka mikoa ya nyanda za juu kusini ndio zamani ikiitwa big 4 na sasa ni big 6, tunawalisha nyie wote, na tunalipa kodi zaidi hata ya hao ambao unawakingia kifua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…