Dkt. Tulia: Nyanda za Juu tumechoka kuwa washangiliaji na sisi tunataka treni ya umeme kama 'Wenzetu'

Dkt. Tulia: Nyanda za Juu tumechoka kuwa washangiliaji na sisi tunataka treni ya umeme kama 'Wenzetu'

Bora hata wangeililia watu wa kutoka Tanga, Kilimanjaro na Arusha! Ila siyo Nyanda za Juu Kusini! Maana hao wamejengewa treni ya kisasa kabisa ya TAZARA! Lakini wameshindwa kuishawishi Serikali kuiboresha ili iwe na tija.

Leo hii ukisafiri na treni ya TAZARA, utashuhudia tu magofu ya majengo kwenye stesheni zake, na huduma mbovu! Huku abiria na mizigo ikiwa ni ya kutosha tu.
Tanga - Moshi - Arusha comrade Polepole aliwapelekea treni!
 
Hata sisi mtwara tunataka treni ya umeme.
Huyu naibu ni [emoji706] kipindi cha mwendazake hakuongea haya..kutwa kushadadia chato...leo kiko wapi.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mmeshaletewa meli!
hahahaaa hiyo meli cjui kama ina viwango vya kutembea kwenye ziwa hilo sababu ni juzi kimepigwa mawimbi kikalala chali pale matema.ziwa nyasa linahitaji meli zenye ustahimilivu sababu hilo ziwa lina mawimbi makubwa sana.na barabara ya kitai,ruanda,paradiso,ndongosi hadi lituhi je?
 
Mimi ni mwanakanda ya nyanda za juu kusini, lakini naona huyu dogo naye hamnazo, kumbe kuwa na PhD hakumaanishi una akili, diplomasia, uzalendo na uelewa mpana, miongoni mwa maeneo yaliyonemeka huko mapema hapa nchini ni Nyanda za juu kusini, walipata TANZAM na TAZARA, Kanda ya Magharibi na Ziwa walikuwa na reli ya kati tu barabara za vumbi kwa muda mrefu, sasa leo hawa wengine wanapelekewa sgr hata kabla haijaisha na yeye tulia anataka... "aibu sana"
Ndiyo maana Msukuma anawadharau sana wasomi wa CCM, wako kiboya zaidi.
 
hahahahaaaa na nyasa pia tunataka.huku kwetu ruvuma naona tunachezewa madini yetu yananufaisha wengine tu.tuna ziwa lkn serikali haiwekezi kwenye hilo ziwa hata maji ya kunywa tunakosa.
Wasalimie kingelikiti mkuu...
 
Kadhalika Dr Tulia amelalamikia Jiji la Mbeya kutopewa hadhi na Huduma stahiki kama ilivyo katika majiji mengine na badala yake Mbeya imekuwa kama Halmashauri.

Tulia amesema miundombinu ya Mbeya ni mibovu sana na miaka yote wamekuwa wakipewa bajeti ndogo isiyokidhi chochote.

Dr. Tulia alikuwa akichangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Ujenzi.
Mwendazake alikuwa mtu wake wa karibu, alishindwa nini kumwambia hayo wakati anafanya Chato
 
Ndiyo maana Msukuma anawadharau sana wasomi wa CCM, wako kiboya zaidi.
Hayati Mwl. Nyerere alisema kuna watu tabia yao ni kudai tu, wanadai, wanadai hata bila ku reason, ni kudai na kudai hata bila kuangalia resources kama zinakidhi hayo wanayodai.

Sasa huyu tulidhani angekuwa mhubiri na mwelimishaji kwa wananchi kujifunza kuwa na subira, lakini ndiye huyo!!!
 
Mbunge wa Mbeya Mjini Dr. Tulia amemtaka Waziri wa Ujenzi kuangalia namna ya kuiwezesha TAZARA kuwa na treni ya umeme.
Dr. Tulia amesema Tanzania ni moja na Wananchi wa pande zote wanahitaji maendeleo hivyo Kanda ya Nyanda za Juu Jusini wamechoka kuwa washangiliaji.

Kadhalika Dr Tulia amelalamikia Jiji la Mbeya kutopewa hadhi na Huduma stahiki kama ilivyo katika majiji mengine na badala yake Mbeya imekuwa kama Halmashauri.

Tulia amesema miundombinu ya Mbeya ni mibovu sana na miaka yote wamekuwa wakipewa bajeti ndogo isiyokidhi chochote.

Dr. Tulia alikuwa akichangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Ujenzi.

Source: Bungeni
As long as kuna treni inatosha kwa kuwa matatizo ya Mbeya siyo kuchelewa kufika Dar au Moro bali ni miundombinu ya ndani ya Jiji.

Dada Tulia amekosea PRIORITY ya Mbeya kwa vile siyo mwana Mbeya na HAKUCHAGULIWA na wana Mbeya. Bali alichaguliwa na Mwendazake.

Usijute naye Mwendazake na huyu alikuwa ana .....
 
Hayati Mwl. Nyerere alisema kuna watu tabia yao ni kudai tu, wanadai, wanadai hata bila ku reason, ni kudai na kudai hata bila kuangalia resources kama zinakidhi hayo wanayodai.

Sasa huyu tulidhani angekuwa mhubiri na mwelimishaji kwa wananchi kujifunza kuwa na subira, lakini ndiye huyo!!!
kwa hiyo resources ziko kwa ajili ya mikoa fulani na mingine hakuna resources.hiyohiyo keki ndogo igawanywe kwa usawa.mamikoa mingine ni mizigo tu lkn inatengenezwa vizuri why not kusini mikoa ambayo ina kila aina ya rasilimali isitengenezwe.
 
Back
Top Bottom