Dkt. Tulia: Nyanda za Juu tumechoka kuwa washangiliaji na sisi tunataka treni ya umeme kama 'Wenzetu'

Dkt. Tulia: Nyanda za Juu tumechoka kuwa washangiliaji na sisi tunataka treni ya umeme kama 'Wenzetu'

Mbunge wa Mbeya Mjini Dr. Tulia amemtaka Waziri wa Ujenzi kuangalia namna ya kuiwezesha TAZARA kuwa na treni ya umeme.
Dr. Tulia amesema Tanzania ni moja na Wananchi wa pande zote wanahitaji maendeleo hivyo Kanda ya Nyanda za Juu Jusini wamechoka kuwa washangiliaji.

Kadhalika Dr Tulia amelalamikia Jiji la Mbeya kutopewa hadhi na Huduma stahiki kama ilivyo katika majiji mengine na badala yake Mbeya imekuwa kama Halmashauri.

Tulia amesema miundombinu ya Mbeya ni mibovu sana na miaka yote wamekuwa wakipewa bajeti ndogo isiyokidhi chochote.

Dr. Tulia alikuwa akichangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Ujenzi.

Source: Bungeni
Ata sisi wa unguja tunataka sgr ipite.
 
TUlia si ungekaa na madiwani wako japo mpime viwanja ule Mji ni squatter tupo kwasasa hata Bajaj hazipati njia nyie mnataka tren...Pimeni Mji angalau kidogo...
 
TUlia si ungekaa na madiwani wako japo mpime viwanja ule Mji ni squatter tupo kwasasa hata Bajaj hazipati njia nyie mnataka tren...Pimeni Mji angalau kidogo...
Mbeya wana kazi kubwa kubadilisha mentality ya ujenzi wa nyumba mijini.

Lakini bado miundombinu ya msingi lazima iboreshwe kama alivyopendekeza Dr Tulia.
 
Kipindi jiwe anapeleka miradi isiyo na idadi chato wala hakuyasema haya.

Zaidi walishangilia na kuunga mkono.

Kweli enzi ya JIWE waliufyata ,leo naona wana nguvu za kusemea majimbo yao!! Tulia vuta maji toka Kiwira kuja Mbeya ama sivyo huyo ubunge utausikia kwenye bomba 2025!!!
 
Mbunge wa Mbeya Mjini Dr. Tulia amemtaka Waziri wa Ujenzi kuangalia namna ya kuiwezesha TAZARA kuwa na treni ya umeme.
Dr. Tulia amesema Tanzania ni moja na Wananchi wa pande zote wanahitaji maendeleo hivyo Kanda ya Nyanda za Juu Jusini wamechoka kuwa washangiliaji.

Kadhalika Dr Tulia amelalamikia Jiji la Mbeya kutopewa hadhi na Huduma stahiki kama ilivyo katika majiji mengine na badala yake Mbeya imekuwa kama Halmashauri.

Tulia amesema miundombinu ya Mbeya ni mibovu sana na miaka yote wamekuwa wakipewa bajeti ndogo isiyokidhi chochote.

Dr. Tulia alikuwa akichangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Ujenzi.

Source: Bungeni
mmh kwa nini asiombe enzi za mwendazake? mnafiki tu
 
Mimi ni mwanakanda ya nyanda za juu kusini, lakini naona huyu dogo naye hamnazo, kumbe kuwa na PhD hakumaanishi una akili, diplomasia, uzalendo na uelewa mpana, miongoni mwa maeneo yaliyonemeka huko mapema hapa nchini ni Nyanda za juu kusini, walipata TANZAM na TAZARA, Kanda ya Magharibi na Ziwa walikuwa na reli ya kati tu barabara za vumbi kwa muda mrefu, sasa leo hawa wengine wanapelekewa sgr hata kabla haijaisha na yeye tulia anataka... "aibu sana"
Kwa jinsi ulivyooanza wewe sio. Hutoki Mbeya.🤨
 
Na sisi huku Namtumbo tunataka treni ya umeme pia.
Seriously, na sisi huku kusini inainabidi tukumbukwe kwenye kugawana hiyo keki ya taifa.
Mkuu Majaliwa (PM), tupiganie na sisi kuhu Nkotokwiyana (Makonde plateau) tupate kipande cha hiyo keki. Wakaskazini wametusahau kwa muda mrefu sana.
 
Nyie mpate treni ya nini, nyie kazi yenu ni kuwapa chama cha majizi kura tu basi. kipindi cha dhalimu ulikuwa unasifia uwanja wa ndege huko porini, mbona hukudai hiyo treni?
 
kwa hiyo resources ziko kwa ajili ya mikoa fulani na mingine hakuna resources.hiyohiyo keki ndogo igawanywe kwa usawa.mamikoa mingine ni mizigo tu lkn inatengenezwa vizuri why not kusini mikoa ambayo ina kila aina ya rasilimali isitengenezwe.

Raslimali gani ziko kusini boss?
 
Nyie mpate treni ya nini, nyie kazi yenu ni kuwapa chama cha majizi kura tu basi. kipindi cha dhalimu ulikuwa unasifia uwanja wa ndege huko porini, mbona hukudai hiyo treni?
Sasa njomba, kwani mambo yote hufanyika kwa wakati mmoja? Ndiyo maana tunamwambia mfalme mbowe atafute angalau kiwanja, kwa kuanzia, kwa ajili ya ujenzi wa ofisi kuu ya chama, mambo mengine yatafuata baadae.
 
Dr Tulia amelalamikia Jiji la Mbeya kutopewa hadhi
susp.png
 
Ahaaa ahaaa ule uchafu ndio treni? Ile treni wanapanda wazee na watu waliopoteza ramani. Bilionea Sabaya alipokuja kwenye kipindi na clous hapa Dar alikuja na hiyo treni?
Sabaya alitua na Chopa pale kwa Mwamposya kisha akaelekea Clouds!
 
Raslimali gani ziko kusini boss?
Halafu wewe una n'ndomo nchafu sana, umesahau kwamba unaotudharau hivyo ndiyo wapiga kura. Tutaonana wakati ukifika; labda mjitoe moja kwa moja kwenye chaguzi zote.
 
Halafu wewe una n'ndomo nchafu sana, umesahau kwamba unaotudharau hivyo ndiyo wapiga kura. Tutaonana wakati ukifika; labda mjitoe moja kwa moja kwenye chaguzi zote.

Wakati wa kura tunaenda popote Tanzania hii tukitaka na watu ni kibao, sana sana muendelee kutumia vyombo vya dola na sio box la kura la halali.
 
Back
Top Bottom