GE2025 Dkt. Tulia: Serikali ya CCM itaendelea kutoa Ruzuku kwenye Pembejeo za Kilimo

GE2025 Dkt. Tulia: Serikali ya CCM itaendelea kutoa Ruzuku kwenye Pembejeo za Kilimo

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

PAYE

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2025
Posts
459
Reaction score
644
Mgombea Ubunge wa Jimbo jipya la Uyole Dkt. Tulia Ackson amesema ili kuinua secta ya kilimo ndani ya Kata ya Iganjo jijini Mbeya watahakikisha Mbolea za Ruzuku na Pembejeo zote za kilimo zinapatikana kwa wingi ili kuongeza tuja katika uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara kwa wakazi wa kata hiyo na jimbo la Uyole.

Dkt. Tulia amesema anafahamu kwamba ndani ya kata hiyo Kuna kilimo cha umwagiliaji hivyo atahakikisha skimu zote za umwagiliaji zinaboreshwa zaidi ili wakulima Wafanye kilimo Bora hivyo ifikapo 29 Oktoba 2025 Wananchi wakapige Kura nyingi kwa CCM ili wakulima wa Jimbo la Uyole wanufaike.

Naobaadhi ya wananchi wanaofanya shuguli zao za kilimo cha umwagiliaji ndani ya kata ya Iganjo wameeleza namna watakavyo nufaika na uboreshwaji wa skimu za umwagiliaji ikiwa ni pamoja na kuongeza kiwango cha maji ndani ya mashamba huku wakiomba serikali kuharakisha pembejeo za ruzuku ili kuingeza uzalishaji na kukuza uchumi wao.

 
Yaani haka kadada kananikera mimi. Wanambeya hatufaidiki na ukubwa wa uongozi wake. Wangekua wengine tungekua hata na uwanja wa michezo wa kisasa.

Amekua spika wa bunnge na raisi wa wabunge duniani lakini hatuoni chochote cha maana
 
Back
Top Bottom